James RicardoKieran Gibbs (alizaliwa26 Septemba1989) ni mchezaji wa kandanda waUingereza ambaye huchezea timu yaArsenal kama mchezaji wa nyuma. Yeye alihudhuria Shule ya Upili ya Riddlesdown katika eneo laPurley,Kusini mwa London.
Gibbs alianza kazi yake katika shule yaWimbledon lakini akahamia Arsenal ,pamoja na Abu Ogogo na James Dunne, Wimbledon ilipoachishwa kazi katika mwaka wa 2004 na ikawaMilton Keynes Dons. Yeye alicheza katika nafasi ya kati na pia kwenye upande wa kushoto. Yeye alihusika mara kwa mara katika timu ya Arsenal ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18 na timu hifadhi.Alicheza pia mechi za kirafiki dhidi yaBarnet naInter Milan. Mnamo Septemba 2007, Gibbs alitia saini mkataba na Arsenal, na alikuwa mmojawapo katika timu iliyotajwa kucheza katika msimu wa 2007-08 Ligi ya Mabingwa ya UEFA na akapewa jezi nambari 34.
Yeye alichezea timu rasmi ya Arsenal kwa mara ya kwanza alipoashiriki katika mechi ya Shindano la Kombe la League dhidi yaSheffield United mnamo 31 Ktoba 2007.Alicheza tena ,kwa mara ya pili, alipoingia kama mchezaji mbadala waEduardo da Silva katika robo fainali dhidi yaBlackburn Rovers,18 Desemba 2007.
Tarehe 31 Januari 2008, yeye alikubali mpango wa mkopo ambao angeenda kucheza katika timu yaNorwich City hadi mwisho wa msimu wa 20007-08. Yeye alirudi Arsenal mwanzoni mwa mwezi wa 29 Aprili 2008 na akachukua nafasi yake katika timu hifadhi ya Arsenal> Yeye alikwenda na kuchaguliwa kama mchezaji mbadala wa kuingia kucheza katika mechi dhidi yaEverton mnamo 4 Mei 2008 lakini hakucheza.
Alicheza katika mechi za kabla ya msimu wa 2008-09,mara nyingi akicheza kama difenda kule nyuma, na akawa mchezaji ambaye hakutumiwa katika mechi dhidi ya Fulham walioshindwa 1-0,24 Agosti 2008, na pia hakutumiwa katika ushindi wao dhidi yaBolton Wanderers wa 3-1(Septemba). Gibbs aliendelea kucheza katika Shindano la Kombe la League na akacheza dakika 90 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Sheffield United katika raundi ya tatu ya mechi,23 Septemba 2008. Yeye,pia, alicheza waliposhinda 3-0 dhidi ya Wigan Athletic na vilevile alicheza katika mechi ya kushindwa dhidi ya Burnley katika hatua ya robo fainali. [14] [15] [16] Yeye alicheza kwa mara ya kwanza katika Shindano la Ligi ya Mabingwa ya UEFA mnamo 10 Desemba 2008 dhidi yaPorto FC akiwa mchezaji mbadala waAbou Diaby.
Gibbs alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Ya Uingereza dhidi yaTottenham Hotspurs mnamo 8 Februari 2009 akiingia kama mchezaji mbadala waGael Clichy aliyeumia katika mechi hiyo.
Gibbs katika mazoezi
Clichy akiwa ameumia, Gibbs alianza mechi yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa katika robo fainali dhidi yaVillareal mnamo 15 Aprili 2009,Arsenal ilishinda 3-0. Gibbs alianza kucheza mechi ya Shindano la Kombe la FA dhidi yaChelsea na akamsaidiaTheo Walcott kufunga bao. Alihusika ,pia, wakati Arsenal na Liverpool walipotoka sare dhidi yaLiverpool, 21 Aprili, hukoAnfield.Aliokoa timu yake kwa kupiga mpira ulipokuwa karibu kuingia goli.
Baada ya kucheza mechi mingi katika timu rasmi kwa kuwa Clichy alikuwa ameumia, Gibbs alicheza katika nusu fainali ya Shindano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United,Arsenal walishindwa 1-0. Hata hivyo, katika mkondo wa pili wa mnusu fainali hiyo, Gibbs alifanya kosa lililomwezeshaPark Ji-Sung kufunga bao muhimu sana baada ya dakika 7. [21]
Alianza katika mchuano wa kwanza wa Arsenal wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Portsmouth na akacheza dakika 90. Clichy alipojeruhiwa na kutoweza kucheza kwa wiki kadhaa,Arsene Wenger alimpa Gibbs nafasi katika timu. Hata hivyo,mnamo tarehe 24 Novemba, Gibbs alivunjika mfupa mguuni katika mechi dhidi yaStandard Liege na jeraha hili likamtoaa kwa mchezo kwa wakati usiojulikana,Arsenal ilishinda 2-0.
Yeye alikuwa katika timu ya Uingereza ya vijana wa chini ya umri wa miaka 19 ambayo ilishindwa katika mkondo wa vikundi katika Shindano la UEFA la 2008 la vijana wa chini ya umri wa miaka 19.Hata hivyo, walihitimu kucheza katika Shindano la Kombe la Dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 20 nchiniMisri lililoandaliwa na FIFA.
Gibbs aliitwa kujiunga na kikosi cha Uingereza cha vijana wa chini ya umri wa miaka 21 akiwa pamoja na mwenzake kutoka Arsenal ,Theo Walcott.Walichaguliwa ili wacheza katika shndano la Uropa la 2009 la vijana wa chini ya umri wa miaka 21 nchinUswidi. Yeye alifunga mabao mawili katika mchuano wa kirafiki naAzerbaijan kabla ya shindano mnamo 8 Juni 2009,walishinda 7-0.Alifunga mkwaju wake wa penalti katika nusu fainali ya shindano hilo dhidi yaUswidi.
Stuart Pearce alimworodhesha Gibbs katika mechi za kuhitimu kucheza katika shindano la Mabingwa wa Uropa ya 2011. Yeye alifunga bao la kwanza katika ushindi wao wa 6-3 dhidi yaMasedonia hapo 9 Oktoba.