Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kenya
Republic of Kenya (en)
Kaulimbiu: "Harambee"
Wimbo wa taifa: "Ee Mungu Nguvu Yetu"
Mahali pa KenyaMahali pa Kenya
Ramani ya KenyaRamani ya Kenya
Mji mkuu
na mkubwa
Nairobi
1°16 S 36°48 E
Lugha rasmi
Lugha ya taifaKiswahili
Kabila (2019)
Dini (2019)
UraiaMkenya
SerikaliJamhuri ya kiraisi
 Rais
 Naibu Rais
 Spika wa Seneti
 Spika wa Bunge
  Jaji Mkuu
William Ruto
Kithure Kindiki
Amason Kingi
Moses Wetangula
Martha Koome
Uhuru Kutoka Uingereza
Karne ya 8
  Jamhuri
1963
  Katiba ya sasa
2010
Eneo
  Jumlakm2 580 367[1]
  Maji (asilimia)2.3
Idadi ya watu
  Kadirio la 202452,428,290[2]
  Sensa ya 201947 564 296[3]
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  JumlaOngezeko $401.97 bilioni[4](ya 59)
  Kwa kila mtuOngezeko $7,530[4]
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  JumlaOngezeko $131.67 Bilioni[4]
  Kwa kila mtuOngezeko $2,470[4]
HDI (2025)Ongezeko 0.628[5](ya 143)
kati
SarafuShilingi ya Kenya
Majira ya saaUTC+3
(Afrika Mashariki)
Muundo wa tarehesiku/mwezi/mwaka
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+254
Msimbo wa ISO 3166KE
Jina la kikoa.ke

Kenya , rasmiJamhuri ya Kenya ninchi iliyopoAfrika Mashariki katikaikweta, kando yaBahari ya Hindi. Kenya imepakana naEthiopia upande wa kaskazini,Somalia upande wa kaskazini mashariki,Tanzania upande wa kusini,Uganda naZiwa Viktoria upande wa magharibi, kishaSudan Kusini upande wa kaskazini magharibi.Mnamo 2024 Kenya ina watu milioni 54 na kuwa nchi ya 26 kubwa duniani kwa Idadi ya watu.Mji mkuu wake mkuu na mkubwa niNairobi, lakiniMombasa ni mji mashuhuri pia. Ukiwa kama mji kongwe zaidi nabandari kuu iliyopo katikaKisiwa cha Mombasa. Miji mingine ni pamoja naNakuru,Eldoret, naKisumu.

Kenya inamandhari mbalimbali kuanzia maeneo yajangwa la Chalbi kaskazini, nyanda za juu zenye rutuba katikati, hadimisitu napwani yenye mandhari ya kuvutia kusini mashariki.Mlima Kenya, mlima wa pili kwa urefu baraniAfrika baada yaMlima Kilimanjaro, uko katikati ya nchi na ni kivutio kikubwa cha utalii. Zaidi ya hayo, mbuga za wanyama kamaMaasai Mara,Amboseli,Tsavo, naSamburu huvutia watalii kutoka kote ulimwenguni kwa sababu ya wanyama pori kamasimba,tembo,vifaru, na pundamilia.

Kiuchumi, Kenya ni nchi iliyoendelea zaidi katika eneo laAfrika Mashariki, ikiwa na uchumi unaotegemea sekta zakilimo, huduma,utalii, na teknolojia. Kilimo, hasa uzalishaji wachai,kahawa,maua na mboga, ni uti wa mgongo wa ajira na mapato ya kigeni.Teknolojia ya habari na mawasiliano pia imekua haraka, huku jiji la Nairobi likiitwa "Silicon Savannah" kwa mchango wake katika ubunifu wa kidijitali na kampuni za teknolojia kamaSafaricom na huduma yaM-pesa.Kiswahili naKiingereza ndizo lugha rasmi za Kenya, ambapoKiswahili hutumika kama lugha ya mawasiliano baina ya makabila tofauti, naKiingereza hutumika katika mandhari rasmi kamaShule,bunge n.k

Jiografia

Mlima Kenya ni kilele cha juu kabisa nchini. Kenya imepata jina lake kutoka mlima huo.

Kenya ina eneo lakilomita za mraba 580,367 (maili mraba 224,081).

Kutokapwani ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo laBonde la Ufa; sehemutambarare yenyerutuba upande wamashariki. Milima ya Kenya ni kati ya iliyofaulu kwakilimo barani Afrika.

Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika[6]Mlima Kenya, unaofikiaurefu wamita 5,199 na ni eneo lenyemito yabarafu.

Kusini masharikimilima ya Taita ndiyo mwanzo watao la Mashariki,safu za milima zenye miaka zaidi yamilioni 100 ambazo zinaenea hasa nchini Tanzania.

Upande huohuo wakusiniMlima Kilimanjaro (m 5 895 (ft 19 341)) huweza kuonekana ukiwa ng'ambo ya mpaka wa Kenya na Tanzania.[7]

Halihewa

Kenya ni nchi yenyejua kali nanguo zamajira ya joto huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa nabaridiusiku na piaasubuhi na mapema.

Hali ya hewa inajoto naunyevu sehemu za pwani, joto kiasi sehemu zabara na nikame katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kunamvua nyingi kati yaMachi naAprili, na mvua ya kadiri kati yaOktoba naNovemba.Halijoto huwa juu zaidi miezi hii yote.

Mvua yamasika hunyesha kuanzia Aprili hadiJuni. Mvua yavuli nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadiDesemba. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati waalasiri najioni. Majira ya joto jingi ni kuanziaFebruari hadi Machi nayo ya baridi niJulai hadiAgosti.

MjiMwinuko

(mita)[8]

Wastani wa Halijoto

(°C)[9]

Upeo wa juu

(°C)[9]

Upeo wa chini

(°C)[9]

Mombasa5026.430.422.5
Nairobi1 79519.7525.713.9
Eldoret2 11117.323.611.1
Lodwar50929.635.324
Mandera54029.434.624.3

Mazingira

Kenya ina maeneo makubwa wanapoishiwanyamapori likiwemoMasai Mara, ambaponyumbu nawanyama wengiwalanyasi hushiriki katikauhamaji kilamwaka. Uhamaji huo, hasa uhamaji wa nyumbu, hutokea Juni hadi Septemba na hushirikisha mamilioni ya wanyama. Tukio hili huwavutia sana wapigajipicha zasinema. Takribani nyumbu 250,000 huangamia kila mwaka katika uhamaji huu wa kutafutalishe wakati wakiangazi.

Wale wanyama wakubwa watano wa Afrika wanapatikana Kenya:simba,chui,nyati,kifaru nandovu. Wanyama wengine wengi wapori nandege hupatikana katikambuga za taifa nahifadhi za wanyama hawa nchini. Mazingira ya Kenya yanahatarishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na athari zake.

Twiga katika Mbuga ya wanyama ya Kitaifa ya Nairobi, na upeo wa macho wa Nairobi nyuma yake.
Njia katikaHifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki.

Historia

Historia ya awali

Mabaki yamamba mkubwa ajabu wa zamani za Mesozoic Era, ambayo ni miakamilioni 200 iliyopita, yaligunduliwa nchini Kenya katikachimbo zilizochimbwa nawataalamu kutokaChuo Kikuu cha Utah naMakavazi ya Kitaifa nchini Kenya miezi ya Julai hadi Agosti2004 katikabonde laLokitaung, karibu naZiwa Turkana.[10]

Mabaki yaliyopatikana Afrika Mashariki yaonyesha kuwa miakamilioni 20 iliyopitaviumbehai mfano wasokwe waliishi eneo hili.Uchunguzi wa juzijuzi karibu na Ziwa Turkana waonyesha kuwa viumbe aina yaHomo habilis (walioishi miaka milioni 1.8 na 2.5 iliyopita) naHomo erectus (walioishi miaka milioni 1.8 na miaka 350,000 iliyopita) huenda ndio wazazi wa watu wa kisasahomo sapiens walioishi Kenyaenzi za barafu kuu kuisha barani.

Katika mwaka wa1984,uvumbuzi uliofanywa namtafiti maarufuRichard Leakey naKamoya Kimeu huko Ziwa Turkana ulikuwa wamifupa yamvulana iliyohusishwa naHomo erectus wa miaka milioni 1.6 iliyopita. Utafiti wa awali wa viumbe hawa unahusishwa naMary Leakey naLouis Leakey, ambao ndio waliofanya uchunguzi wa mwanzo wa kiakiolojia hukoOlorgesailie naHyrax Hill. Baadaye utafiti wa Olorgesailie uliendelezwa naGlynn Isaac.

Historia kabla ya ukoloni

Msikiti mkuu waGedi ambao ni wa kutokakarne ya 13.

Wakazi wa kwanza wa eneo linaloitwa Kenya walikuwa wa jamii yaWakhoisan: hadi leo kuna makabila matatu madogo yenye asili hiyo, ingawa yanatumialugha za Kikushi:Waata,Waawer naWadahalo.

Wakushi kutokakaskazini waliingia Kenya kati yamiaka ya 3200 KK na1300 KK[11]. Mwaka500 KK hivi wazungumzaji walugha za Kinilo-Sahara na katikamilenia ya kwanza KK wale walugha za Kibantu waliingia katika eneo hili, na sasaWaniloti ni 30% ya Wakenya wote.

WafanyabiasharaWaarabu walianza kufikapwani ya Kenyakarne ya 1BK. Ukaribu wa Kenya na Uarabuni ulirahisishaukoloni, hivyo Waarabu naWaajemi walianza kuishi eneo la pwanikarne ya 8. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa machotara, Waafrika-Waarabu.

Pwani ya Kenya imekuwa makao ya jamii yawahunzi na jamii yawakulima wadogowadogo,wawindaji nawavuvi ambao walikuwamhimili wauchumi kwa kushiriki katika kilimo, uvuvi, utengenezaji chuma, nabiashara na nchi za kigeni.[11]

Kuanziakarne ya 6 aukarne ya 9, Kenya ilijihusisha nashughuli za ubaharia kukuzauchumi ikaanza kutengenezameli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenyebandari kamaKilwa naShanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.

Mombasa ulikuwamji wenye bandari wa nchi ya Kenya katikakarne za kati. Bandari hiyo ilitumika kuendelezabiashara na miji mingine yenye bandari Afrika,Uajemi, na wafanyabiashara Waarabu,Yemeni na hataBara Hindi.[12]

BahariaMrenoDuarte Barbosa wakarne ya 15 alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi,mashua nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutokaSofala na nyingine kutokaCambay,Melinde na nyingine zinazoabiri hadi kisiwaniUnguja."[13]

Karne kadhaa kabla ya ukoloni,upwa wa Kenya wanakoishiWaswahili ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa yawatumwa napembe za ndovu na Waarabu naWahindi. Inasemekana kwambakabila laWameru lilitokana na watumwa waliotoroka utumwaUarabunimiaka ya 1700. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitokeamilki za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatokea Unguja (kamaTippu Tip).[14]

Kiswahili, ambacho nilugha yaKibantu iliyokopamisamiati yaKiarabu,Kiajemi na mingine kutokaMashariki ya Kati naAsia Kusini, baadaye ilikua ikawalingua franca ya biashara kwa jamii mbalimbali.[11]

Kwakarne nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya , mji waMalindi umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangukarne ya 14 na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwaserikali nyingine. Mwaka wa1414,Sultani Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala waUchina waMing, wakati wa safari zamchunguziZheng He.[15] Katika mwaka wa1498, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri namvumbuzi maarufu kutoka Ureno,Vasco da Gama.

Chini ya ukoloni

Seaport Mombasa, chini ya Malindi, ina reli ya Nairobi (kituo), kusini ya Naivasha& Nyeri. (bonyeza ramani ilu kuipanua)

Wareno walikuwaWazungu wa kwanza kuzuru eneo la Kenya ya sasa:Vasco da Gama alikuwa amezuru Mombasa mwaka wa1498. Safari ya Vasco da Gama ilifaulu alipofikia hukoIndia, na jambo hilo liliwawezesha Wareno kufanyabiashara moja kwa moja naMashariki ya Mbali kupitiabahari na hivyo kutatiza mitandao ya kibiashara ya awali yanchi kavu na baharini kama njia za biashara yaviungo zilizotumiaGhuba la Uajemi,Bahari Nyekundu na misafara iliyofika hadi eneo la mashariki yaMediterranea.

Jamhuri ya Venisi ndiyo iliyotawala maeneo ya biashara kati taUropa naAsia. Baada ya njia za kawaida za nchi kavu hadi India kufungwa naWaturuki waOttoman, Ureno ulitarajiwa kutumia njia ya baharini iliyotumiwa kwanza na Vasco da Ghama ili kuvunjaukiritimba waVenice.

Utawala wa Wareno huko Afrika Mashariki ulijihusisha hasa na pwani iliyokaribia Mombasa. Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kulianza rasmi baada ya mwaka wa1505, wakatimanowari za Wareno, zikiongozwa na DonFrancisco de Almeida, zilipokishindaKilwa,kisiwa kilicho katika eneo ambalo sasa niTanzania kusini.

Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kuliwawezesha kudhibiti biashara katikaBahari ya Hindi, na kulinda njia za baharini zinazounganisha Uropa na Asia. Manowari zao za kivita zilikwamisha biashara za maadui wao magharibi mwa Bahari ya Hindi na walitozakodi juu yabidhaa zilizosafirishwa kupitia eneo hilo kwani walitawalabandari zote na njia kuu zameli.

Kujengwa kwangome iliyoitwaFort Jesus Mombasa mwaka wa1593 kulikusudiwa kuimarisha utawala wao katika eneo hilo, lakiniushawishi wao ulikatizwa na kuja kwaWaingereza,Waholanzi naWaarabu waOmani katika eneo hilokarne ya 17.

Waarabu kutoka Omani ndio waliokuwatishio kuu la utawala wa Wareno Afrika Mashariki na waliizingira ngome ya Wareno, wakazishambulia meli zao za kivita, kisha kuwafukuza Wareno waliobaki kutoka pwani ya Kenya na Tanzania mwaka wa1730. Kufikia wakati huo, ufalme wa Ureno haukuwa nahaja na njia ya bahari ya biashara ya viungo kwanifaida yake ilikuwa imepungua sana. Utawala wa Wareno ulibakia tu katika bandari na maeneo ya kusini mwaMsumbiji hadi mwaka wa1975.

Kutawaliwa kwa pwani ya Kenya na Tanzania na Waarabu kutoka Omani kuliifanya miji hii iliyojitawala hapo awali iwe chini ya uangalifu mkali wa wageni kuliko ilivyokuwa katika enzi za utawala wa Wareno. Waarabu wa Omani, kama Wareno waliowatangulia, waliweza kutawala eneo la pwani tu, si eneo la bara. Hata hivyo, kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya mikarafuu, kuongezeka kwabiashara ya utumwa na kuhamishwa kwamakao makuu ya Waomani hadiZanzibar mwaka wa1839 naSeyyid Said kulisababisha Waomani kuimarisha utawala wao katika eneo hilo.

Utawala wa Waarabu katika bandari kuu zote za pwani ya Afrika Mashariki uliendelea hadiUingereza ilipoamua kumaliza biashara ya utumwa na uanzishaji wautaratibu wa kufanyakazi kwamalipo ukaanza kushinikiza utawala wa Waomani.

Kufikia mwisho wakarne ya 19, biashara ya watumwa katika bahari zote kuu ilikuwa imeharamishwa na Waingereza: Waarabu wa Omani hawakuwa na uwezo wa kupingana najeshi la wanamaji la Uingereza lililokuwa likitekeleza amri hiyo. Waomani waliendelea kuwepo visiwaniUnguja naPemba hadimapinduzi ya mwaka wa1964, lakini kuwepo kwa Waarabu wa Omani nchini Kenya rasmi kulisitishwa wakati Wajerumani na Waingereza walipozidhibiti bandari zote kuu na kuanzisha mahusiano ya kibiashara na viongozi mashuhuri waliokuwa wenyejimiaka ya 1880. Hata hivyo,urithi waliouacha Afrika Mashariki ungali unaonekana kupitia kwa vizazi vyao vipatikanavyo pwani ya Kenya na ambavyo vinaona kuwa asili yao ni Oman. Vizazi hivi hata leo humilikiutajiri mwingi na ndio wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa katika jamii za pwani ya Kenya.

Reli ya Kenya-Uganda karibu na Mombasa,1899 hivi

Hata hivyo,wanahistoria wengi hushikilia kuwahistoria yaukoloni nchini Kenya ilianza wakati Wajerumani walipoanza kutawalamali yaSultani wa Unguja iliyo pwani mwaka wa1885, ikifuatwa na kuja kwakampuni ya Imperial British East Africa Company mwaka wa1888.

Uhasama wa kwanza baina ya mabepari ulikatizwa wakati Ujerumani ulipouachia Uingereza sehemu ya pwani iliyomiliki. Hii ilifuatia kujengwa kwareli iliyounganisha Kenya naUganda. Baadhi ya makabila ya Kenya yalipingaujenzi huo, hasaWanandi wakiongozwa naOrkoiyot Koitalel Arap Samoei kwa miaka kumi, kuanzia1895 hadi1905 – lakini hatimaye Waingereza waliijenga reli hii.

Inaaminika kuwa Wanandi walikuwa kabila la kwanza kuwekwa kwenye maeneo yaliyotengewaWaafrika ili kuwazuia kutatiza ujenzi wa reli. Wakati huoWahindi wengi wenyeujuzi waliingia nchini ili kuchangia ujenzi. Wakati wa ujenzi wa reli kupitiaHifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi, Wahindi wengi na wenyeji Waafrika walivamiwa nasimba wawili waliojulikana kama “wala watu wa Tsavo”. Wahindi hao na vizazi vyao baadaye walibakia nchini Kenya na kuundakitovu chajamii za Wahindi zijulikanayo kamaIsmaili Muslim naSikh.[16][17]

Mnamo Agosti1914,Vita vya Kwanza vya Dunia vilipoanza, magavana waBritish East Africa (kama eneo hilo lilivyojulikana) naGerman East Africa walifikia makubaliano ili kuepusha makoloni yao machanga na uhasama. Hata hivyo,Luteni KanaliPaul von Lettow-Vorbeck alichukuamamlaka ya majeshi ya Ujerumani, akiwa na kusudi la kutwaaraslimali nyingi iwezekanavyo za Uingereza. Jeshi la Uingereza likiwa limemtenga na Ujerumani, von Lettow aliendeshakampeni iliyofaulu yavita vya kuvizia, wakila walichopata, wakiteka bidhaa za matumizi za Uingereza, na kuepuka kushindwa. Mwishowe alisalimu amri na akajisalimisha nchiniZambia siku kumi na moja baada ya mapatano ya kusimamisha vita kutiwasahihi mwaka wa1918. Waingereza walitumia jeshi la Wahindi kumfukuza Lettow na walihitajiwachukuzi wengi ili kubeba vifaa vya matumizi hadibara kwamiguu na hivyo kutatuashida kuu ya uchukuzi. Kundi la wanajeshi wachukuzi liliundwa na kuwajumuisha Waafrika 400,000, na kuchangia katikauhamasishaji wao wa muda mrefu kisiasa.

Hadi mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya lilijulikana kama Himaya ya Uingereza ya Afrika Mashariki.[18] Mwaka huo,koloni la Kenya liliundwa na kupatiwa jina linalotokana na Mlima Kenya[19]Waingereza walilitamka jina hilo kamapronounced/ˈkiːnjə/[20] ingawa matamshi ya wenyeji na yaliyokusudiwa katika maendelezo asili,Kenia yalikuwa ˈkɛnja.[21] Enzi yaJomo Kenyatta kuwarais wa Kenya miaka ya1960-1969, matamshi yaKiingereza, yaani/ˈkɛnjə/ yalikubalika na kutumiwa sana kwa sababu jina lake lilidumisha matamshi asilia ya wenyeji.[22] Kumbe saa ya uhuru, mwaka1963,Jomo Kenyatta alichaguliwa kama rais wa kwanza.[23] Awali alikuwa alishika jina hili kutafakari ahadi yake ya kuikomboa nchi yake na matamshi yake ya jina lake ulisababisha katika matamshi ya Kenya katika Kiingereza kubadilisha nyuma ya makadirio ya awali uliotokea matamshi,pronounced/ˈkɛnjə/

Mwanzoni mwakarne ya 20,wakulima Waingereza na Wazungu wengine walituama katikanyanda za juu katika eneo la kati walikoondokea kuwa matajiri kwa kulimakahawa nachai.[24] Kufikia mwaka1930, takribaniwalowezi 30,000 waliishi katika maeneo hayo na walikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa sababu ya uwezo wao wa kiuchumi.

Maeneo hayo yalikuwa makao ya watumilioni moja wa kabila laWakikuyu, na wengi wao hawakuwa naithibati ya kumiliki mashamba kwa mujibu wa Waingereza (ingawa mashamba hayo yalimilikiwa na kabila hilo kabla ya Wazungu kufika), na waliishi kama wakulima wanaohamahama. Ili kuendeleza matakwa yao, walowezi waliwakataza kilimo cha kahawa na kuwalazimisha kulipa kodi yanyumba, na maskwota walipewa mashamba madogo baada ya kuwafanyia kazi. Wakikuyu wengi walihamia mijini kwani mashamba yao hayangeweza kutosheleza mahitaji yao.

Mwaka wa1951,Horace Hector Hearne akawamkuu wa sheria nchini Kenya (alitokaCeylon alikoshikiliawadhifa huohuo) na alifanya kazi katikaMahakama Kuu mjiniNairobi. Alihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka1954 alipoteuliwa kamaHakimu wa Rufaa katikaMahakama ya Rufaa yaAfrika Magharibi.Usiku wa tarehe5 Februari1952, wakatiMfalmeGeorge VI alipoaga dunia, Hearne alimsindikizaMalkiaElizabeth II namumewe Filipomwanamfalme waEdinburgh, kwa dhifa ya kitaifa hotelini Treetops, ambayo sasa ni kivutio maarufu cha watalii. Hapa ndipo alipouanzia umalkia.[25] Alirudi Uingereza mara moja akiandamana na Hearne.

Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba1959, Kenya ilikuwa katikahali ya hatari kufuatiauasi waMau Mau dhidi ya utawala wa Uingereza. Gavana aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Waingereza na Waafrika, pamoja naKing's African Rifles. Mnamo Januari1953,Meja Jenerali Hinde aliteuliwa kuwa mkuu wa oparesheni ya kuzima uasi. Hali hii haikuimarika kwa kukosa uchunguzi, kwa hivyoJeneraliGeorge Erskine aliteuliwa kuwakamanda msimamizi wa majeshi ya kikoloni mnamo Mei 1953, akiungwa mkono hasa naWinston Churchill.

Kutiwa mbaroni kwaWarũhiũ Itote (akaGeneral China) tarehe15 Januari 1954, na kuhojiwa kwake kulipelekea Waingereza kuuelewa vyema usimamizi wa Mau Mau.Oparesheni Anvil iliyoanzishwa tarehe24 Aprili 1954 ilipangwa najeshi kwawiki kadhaa baada ya kukubaliwa na kamati kuu ya vita. Wakati wa oparesheni hiyo, mji wa Nairobi ulidhibitiwa na wanajeshi na wakazi wake walihojiwa huku wafuasi wa Mau Mau wakikamatwa na kupelekwa vizuizini.

Mnamo Mei 1953, walinzi wa nyumbani walitambulika rasmi kamaaskari wa usalama. Askari hao wa nyumbani ndio waliounda kikosi cha kupambana na mikakati ya Mau Mau kwani walikuwa Waafrika waaminifu, na si majeshi ya kigeni kama Jeshi la Uingereza na King's African Rifles. Kufikia mwisho wa hali ya hatari, askari hao walikuwa wamewaua Mau Mau 4886, ambao ni asilimia 42% ya waasi wote. Kukamatwa kwaDedan Kimathi hukoNyeri tarehe21 Oktoba1956 kuliashiria kushindwa kwa Mau Mau kukamaliza vita.

Baada ya uhuru

Sanamu ya Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Utawala wa Kenyatta

Waafrika walichaguliwa moja kwa moja katikabunge la uwakilishi kwa mara ya kwanza mwaka wa1957. Licha ya Waingereza kutamani kuwakabidhimamlaka wapinzani wasio nasiasa kali ya Kiafrika, nichama chaKenya African National Union (KANU) kilichoongozwa naJomo Kenyatta kilichoundaserikali punde tu kabla ya Kenya kupatauhuru tarehe12 Desemba1963. Tarehe 12 Desemba1964, Kenya ilipotangazwa kuwajamhuri, Kenyatta akawarais wa kwanza.

Mwaka huohuo,jeshi la Kenya lilipigana naVita vya Shifta dhidi ya kabila laWasomali waliokusudia kuiona NFD imejiunga naJamhuri ya Somalia.Mashifta walililemea jeshi la Kenya lakini baadaye walishindwa mwaka wa1967.

Kenya ilitiasainimkataba na nchi yaEthiopia mwaka wa1969 unaodumu mpaka leo kwa kuhofia mashambulizi kutoka kwajeshi la Somalia lililokuwa na nguvu zaidi.[26] Eneo la NFD nchini Kenya halijaendelea kutokana nakiangazi namafuriko. Hata hivyo,wakimbizi wafanyabiashara wa Kisomali waliotajirika wamebadilishamtaa wa Eastleigh uliokuwa wa mabanda na kuufanya kuwa ngome ya kibiashara katika sehemu kubwa ya mashariki mwa mji wa Nairobi.[27]

Utawala wa Moi

Mwaka wa1978, Kenyatta alifariki naDaniel Arap Moi akawa rais. Moi alidumishaurais kwa kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi za mwaka wa1979,1983 (uchaguzi wadharura) na1988, zote zikiwa zilifanyika chini yakatiba yachama kimoja. Uchaguzi wa 1983 ulifanyika mwaka mmoja kabla ya wakati kutokana nanjama yakupindua serikali iliyokosa kufaulu tarehe1 Agosti1982.

Mapinduzi hayo yaliyotibuka yalipangwa naaskarimwanahewa wacheo cha chini, BwanaHezekiah Ochuka na kuendelezwa hasa na wanahewa.Jaribio hilo lilizimwa kwa haraka na wanajeshi waaminifu wakiongozwa naJeshi la Nchi Kavu, General Service Unit (GSU) - kikosi chapolisi wenyehadhi ya kijeshi - na baadaye polisi wa kawaida. Hata hivyoraia kadhaa walijeruhiwa na wengine kuuawa.Tukio hilo lilisababisha kuvunjwa kwa kikosi chote cha wanahewa, huku wengine wakiachishwa kazi na wengine wakishtakiwa kwenyemahakama ya kijeshi.

Katika uchaguzi wa 1988kura za mlolongo zilianzishwa, ambapo wapigakura walitakiwa kupigafoleni nyuma yawagombea wanaowapenda, badala ya kutumiakura ya siri[28] Jambo hilo lilionekana kamakilele cha enzi yaukiukaji mkubwa wademokrasia likasababishamsukumo mkuu wamageuzi ya kikatiba. Vipengele vilivyokuwa na utata, kikiwemo kile kilichoruhusu chama kimoja pekee cha kisiasa, vilibadilishwa miaka iliyofuata.[29]

Katika uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi wa miaka ya1992 na1997, Daniel Arap Moi alichaguliwa tena.

Utawala wa Kibaki

Kulingana na katiba, mwaka2002 Moi hakuruhusiwa kuwania urais tena, naMwai Kibaki wachama cha upinzani cha "National Rainbow Coalition" — NARC akachaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huo ulitambulikana kuwa wa kidemokrasia nawachunguzi wa humu nchini na wa kimataifa na hivyo kuwa chanzo cha mageuzi makubwa ya kidemokrasia nchini Kenya.

Mnamo Desemba2002, Wakenya walifanya uchaguzi uliokuwa wa kidemokrasia na uwazi ambao kwa kiasi kikubwa uliamuliwa kuwa huru na wa haki na wachunguzi wa kimataifa. Uchaguzi wa mwaka huo ulikuwa mwanzo mpya na uliiletea Kenya mabadiliko makuu ya kisiasa yaliyowezesha chama cha Kenya African National Union (KANU), kilichokuwa kimeitawala nchi tangu uhuru, kukabidhi kwa amani mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARK), uliokuwa muungano wa vyama vingi.

Chini ya uongozi wa Rais Mwai Kibaki, muungano wa vyama tawala ulihahidi kushughulikia ukuaji wa kiuchumi, kumaliza ufisadi, kuimarisha elimu na kuandika katiba mpya. Baadhi ya ahadi hizi zimeshatimizwa. Kuna elimu ya msingi ya bure. Mwaka wa 2007 serikali ilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2008 gharama ya masomo ya shule za upili itapunguzwa huku serikali ikilipia gharama zote za mafundisho.

Uchaguzi wa 2007

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 Desemba 2007, Rais Kibaki wa chama cha Party of National Unity (PNU) aliwania uchaguzi dhidi ya chama kikuu cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM). Kulingana na wachunguzi wa kimataifa, uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na hivyo kutofikia kiwango kinachokubalika kimataifa. Chama cha ODM kilisambaratika na kupoteza 8 % ya kura zake kwa chama kipya cha Orange Democratic Movement-Kenya (ODM) - kikiongozwa naKalonzo Musyoka. Kinyang’anyiro kilikuwa kikali kati ya mgombea wa ODM,Raila Odinga na Kibaki wa PNU. Kuhesabiwa kwa kura naTume ya Uchaguzi ya Kenya kulionyesha Raila akiongoza kwakura chache na baadaye kwa kura nyingi. Hata hivyo, kura zilipoendelea kuhesabiwa na Tume ya Uchaguzi, Kibaki alimkaribiampinzani wake kwa kura, kisha akamshinda. Matokeo hayo yalisababishamaandamano na kulaumiwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kumpendelea Kibaki, hivyo Oginga akajitangaza “rais wa watu” na kutaka kura zihesabiwe tena.[30]

Maandamano hayo yalibadilika kuwaghasia zilizosababisha kuharibiwa kwamali.[31]. Viongozi mashuhuri wa Afrika, wakiongozwa na aliyekuwakatibu mkuu wa Umoja wa MataifaKofi Annan walisuluhishamzozo huo wa kisiasa. Kundi la Annan liliungwa mkono naUmoja wa Mataifa,Jumuia ya Ulaya,Muungano wa Nchi za Afrika, Serikali ya Marekani na nchi nyingine maarufu ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi rejeleaGhasia nchini Kenya (2007-2008).

Annan aliomba usaidizi kwakamati yake yaupatanishi kutoka kwa shirika la kushughulikia mizozo laUswisi lijulikanalo kama Kituo cha Mazungumzo ya Kihisani yaani Centre for Humanitarian Dialogue.

Serikali ya muungano

Tarehe12 Februari 2008 Kibaki na Odinga walitia sahihi mkataba wa kuundaserikali ya muungano ambapo Odinga angekuwawaziri mkuu wa pili nchini Kenya. Kulingana na mkataba huo, rais angeteuabaraza la mawaziri kutoka pande zote mbili za PNU na ODM kulingana na wingi wa wabunge wa kila chama bungeni. Mkataba huo ulieleza kuwa baraza la mawaziri litajumuishaMakamu wa Rais na manaibu wawili wa Waziri Mkuu. Baada ya majadiliano bungeni ilipitishwa kuwa muungano huo utadumu hadi mwisho wa kipindi cha bunge, ama chama kimoja kikijitoa kwenye muungano kabla ya kipindi cha bunge kuisha.

Wadhifa huo mpya wa waziri mkuu utakuwa na nguvu na mamlaka kuratibu na kusimamia shughuli za serikali. Vilevile itaongozwa na mbunge aliyechaguliwa ambaye pia atakuwa kiongozi wa chama au muungano wa vyama wenye idadi kubwa ya wabunge bungeni. Ulimwengu ulimshuhudia Annan na kamati yake iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mwenye kiti wa muungano wa nchi za Afrika Jakaya Kikwete, walipowaleta pamoja wapinzani hawa sugu kwenye sherehe za kutia sahihi mkataba huu. Sherehe hizi zilionyeshwa moja kwa moja kwenya televisheni ya kitaifa kutoka kiingilio cha Jumba la Harambee mjini Nairobi. Wawakilishi wa PNU na ODM walianza majadiliano ya kina kuhusu ugavi wa mamlaka tarehe 29 Februari 2008.[32] Wabunge wa Kenya, kwa pamoja, waliidhinisha mkataba wa ugawaji mamlaka tarehe 18 mwezi wa Machi 2008 ili kuiokoa Kenya iliyoaminika kama mojawapo ya nchi thabiti na iliyoendelea barani Afrika. Mkataba huu uliunganisha PNU iliyoongozwa na Kibaki na ODM ya Odinga kisha kupelekea kuundwa kwa serikali ya muungano, vyama vyote viwili vikiwa na mamlaka sawa.[33]

Tarehe13 Aprili 2008, Rais Kibaki aliitangaza baraza la mawaziri 41 wa serikali hii ya muungano ikijumuisha waziri mkuu na makamu wake wawili. Baraza hili lilijumuisha pia manaibu wa mawaziri 50 na lilitawazwa katikaIkulu ya Nairobi tarehe17 Aprili 2008 huku Kofi Annan na viongozi wengine mashuhuri wakishuhudia.

Tarehe4 Novemba2008 ilitangazwa kuwasikukuu ya kitaifa kusherehekeaushindi waBarack Obama, ambayebaba yake alikuwa Mkenya, kama rais waMarekani.

Katika sehemu za mashambani, kama wilayaniKisii, visa vya kuchoma watu wakidaiwa kuwawachawi vinaongezeka.[34] Waathiriwa hasa ni wanawake wakongwe. Mnamo Mei 2008, watu 11 waliuwa na nyumba 30 kuchomwa.[35]

Siasa na Utawala

Tazama pia:Orodha ya vyama vya kisiasa nchini Kenya

Kwa sasa Kenya nijamhuri yakidemokrasia ya kiuwakilishi inayoongozwa na rais, ambaye ndiye mkuu wa taifa na kiongozi wa serikali, na yenyemfumo wa vyama vingi.Serikali ndiyo yenyemamlaka ya juu.

Utungaji washeria ni jukumu la serikali na labunge la taifa. Idara ya Mahakama ni huru, na imejitenga na serikali kuu na bunge. Hata hivyo, kulikuwa na kutoridhika kwingi, hasa katika enzi ya rais mstaafuDaniel Arap Moi, kuwa serikali iliingilia sana shughuli za mahakama.

Kenya imedumisha uthabiti wa kutosha licha ya mabadiliko katika mifumo yake ya kisiasa na michafuko katika nchi kadhaa jirani. Bunge la mseto wa vyama vingi la1997 lilianzishamageuzi yaliyobadilisha sheria za kikoloni zenyedhuluma zilizotumika kuuzuia uhuru wa kuongea na kutangamana. Jambo hilo liliimarisha uhuru waumma na kuchangia kiasi kuaminika kwauchaguzi wa Desemba 1997.

Kaunti na tarafa

Kaunti za Kenya.

Kenya inakaunti 47, kila moja ikiongozwa na Mkuu wa Kaunti anayechaguliwa na watu ambao wanaishi kwenye hiyo kaunti.

Serikali za mitaa huendelezwa kupitia mabaraza ya miji. Maeneo mengi ya mijini huwa nimji,manisipaa au baraza la mji. Serikali za mitaa katika maeneo yamashambani huitwaserikali zawilaya. Madiwani wa mitaa hii huchaguliwa katikauchaguzi wa madiwani unaofanywa wakati mmoja nauchaguzi mkuu.

Maeneo ya uwakilishi bungeni yamegawanywa kwa sababu ya upigajikura. Kuna maeneobunge 210 nchini Kenya.[36]

Demografia

Miji

 
 
Jiji na miji kubwa zaidi katika Kenya
Kulingana na sensa ya 2019[37]
CheoKauntiWakaziRankKauntiWakazi
1NairobiNairobi4 397 07311Ongata RongaiKajiado172 569
2MombasaMombasa1 208 33312GarissaGarissa163 399
3NakuruNakuru570 67413KitaleTrans-Nzoia162 174
4RuiruKiambu490 12014JujaKiambu156 041
5EldoretUasin Gishu475 71615MlolongoMachakos136 351
6KisumuKisumu397 95716MalindiKilifi119 859
7KikuyuKiambu323 88117ManderaMandera114 718
8ThikaKiambu251 40718KisiiKisii112 417
9NaivashaNakuru198 44419KakamegaKakamega107 227
10KaruriKiambu194 34220NgongKajiado102 323

Kenya ni nchi yenye makabila mengi tofautitofauti, hasa yaKibantu (67%) na yaKiniloti. Wakenya wengi huzungumzalugha mbili,Kiingereza naKiswahili, naasilimia kubwa pia huzungumzalugha mama ya kabila lao.

Makundi ya makabila ni kama ifuatavyo:Wakikuyu 22%,Waluyia 14%,Wajaluo 13%,Wakalenjin 12%,Wakamba 11%,Wakisii 6%,Wameru 6%, makabila mengine ya Kiafrika 15%, wasio Waafrika (Wahindi,Waingereza naWaarabu) 1%[1]Kila kundi au kabila lina lugha yake na Kiswahili hutumika kama chombo cha kuwasiliana miongoni mwa makabila tofauti.

Dini

Kanisa Katoliki hukoMombasa.

Upande wadini, idadi kubwa ya Wakenya niWakristo: kulingana nasensa ya mwaka2019,asilimia 85.5 yawakazi waKenya walikuwaWakristo (asilimia 53.9 niWaprotestanti, asilimia 20.6 niWakatoliki, asilimia 11.8 ni Wakristo wamadhehebu mengine mbalimbali, wakiwemo Waorthodoksi 621,200), asilimia 10.9 niWaislamu, asilimia 0.7 ni wafuasi wadini asilia za Kiafrika, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini (kunaWahindu takribani 60,000, ambao wameingiliana vyema na Wakenya wengine na huchangia pakubwa uchumi wa nchi), na asilimia 1.6 wanadai hawana uhusiano nadini yoyote ile.

Dini nchiniKenya mwaka 2019
Ukristo
 
85.5%
Uislamu
 
10.9%
Wasio na dini
 
1.7%
Dini za jadi
 
0.7%
Chanzo : KNBS (Sensa 2019)

Waislamu wengi huishi katika kaunti za Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa nchi huku wengine wakiishi katika pwani. Wengi wa wanaoishi sehemu ya magharibi mkoani Pwani ni Wakristo. Eneo la kaskazini la Mkoa wa Mashariki ni makazi ya asilimia 10 ya jumla ya Waislamu nchini; hii ndiyodini ya wakazi wengi wa hapa, na mbali na idadi ndogo yaWasomali wanaoishi Nairobi, idadi kubwa ya Wakenya wengine ni Wakristo.[38]

Sanaa na Utamaduni

Utamaduni

Askari Wamasai
Mmasai katika mapambo ya jadi

Kenya ni nchi yenye tamaduni anuwai. Tamaduni zinazotambulika ni pamoja na Waswahili walio katika eneo la pwani, jamii za wafugaji katika eneo la kaskazini na jamii nyingine mbalimbali katika maeneo ya kati na magharibi.

Wajaluo wa Kenya ni wazawa wajamii zawakulima nawafugaji walioishi magharibi mwa Kenya kabla ya ukoloni. Inafahamika kwamba asili ya Wajaluo na makabila mengine yaWaniloti ni kaskazini mwa Kenya, pengine maeneo ya Sudan Kusini ya sasa. Waniloti, kama wanavyoitwa, ni kikundi cha kianthropolojia kilichotoka maeneo ya kaskazini mashariki mwa Afrika. Pengine walihamia kusini kutokana navita vilivyosababishwa na ukuaji waKush naMisri. Waniloti nchini Kenya niWajaluo,Waturkana,Wakalenjin naWamasai. Hili linadhihirika kutokana na kuwepo kwalahaja zinazofanana kati ya makabila fulani nchini Sudan Kusini leo. Makabila haya ni pamoja naAkoli naLwo (si sawa na Luo) wanaoishi katika eneo laDarfur.

Kuna makabila mengine ya Waniloti yanayoishi nchiniUganda naTanzania. Hii hasa ni kwa sababu ya Wajaluo kuvutiwa naZiwa Victoria, ambako wanapatikana katika nchi hizi tatu (Uganda, Tanzania na Kenya). Nchini Uganda, wanajulikana kwa kuanzishahimaya yaWaganda na ya himaya yaWatoro. Wajaluo nchini Kenya walipigana vita na majirani wao, hasa Wakalenjin, ili kulidhibiti ziwa hilo.

Leo hii, utamaduni wa Wamaasai unajulikana sana kwa kuangaziwa vilivyo na utalii, hata hivyo Wamaasai ni asilimia ndogo ya idadi ya Wakenya kwa jumla. Wamaasai wanatambulika kwa kujipamba sehemu ya juu ya mwili na kwa vito.

Kenya ina utajiri mwingi wamuziki, vituo vyaruninga namaonyesho ya sanaa.

Fasihi

Makala kuu:Fasihi ya Kenya

Ngugi wa Thiong'o ni mmoja wawaandishi maarufu wa Kenya.Kitabu chakeen:Weep Not, Child ni ufafanuzi wamaisha yalivyokuwa Waingereza walipoitwaa Kenya. Hii nihadithi kuhusu athari za Mau Mau katika maisha ya Wakenya asili. Kinavyochanganya maudhui - ukoloni, elimu, na mapenzi - kunakifanya kuwa kimojawapo kati ya vitabu bora vya hadithi barani Afrika.

Kitabu cha hadithi chaM. G. VassanjiThe In-Between World of Vikram Lall kilishinda tuzo la Giller Prize mwaka 2003. Hii ni hadithi ya kubuni ya Mkenya mwenye asili ya Kihindi nafamilia yake wavyojizatiti na mabadiliko ya kisiasa wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni nchini Kenya.

Kuanzia mwaka wa 2003, jarida la fasihiKwani? limekuwa likichapisha fasihi ya kisasa ya Kenya.

Elimu

Mfumo wa elimu nchini Kenya unajumuisha elimu yachekechea,ya msingi, yasekondari na yavyuo. Elimu ya watoto wadogo aghalabu huchukua miaka mitatu, ya msingi miaka minane, sekondari minne na chuo kikuu miaka minne au sita kwa kutegemea kozi.

Shule za chekechea, ambazo ni za watoto wa umri wa miaka mitatu hadi mitano, ni sehemu muhimu ya mfumo huu wa elimu na ni kigezo muhimu kabla ya kusajiliwa katika darasa la kwanza (Gredi ya Kwanza).

Mwishoni mwa elimu ya msingi wanafunzi hufanya mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Msingi Kenya (KCPE), ambao huamua watakaojiunga na shule ya sekondari au vyuo vya ufundi. Umri wa shule ya msingi ni miaka 6/7 hadi 13/14.

Wale wanaojiunga na shule ya upili hufanya mtihani wa taifa mwishoni mwa kidato cha nne - Mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Shule ya Upili Kenya (KCSE), ambao huamua watakaojiunga na vyuo vikuu, vyuo vya taatuma nyinginezo au kuajiriwa. Baraza Kuu la Usajili (JAB) ndilo lenye jukumu la kuwachagua wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu vya umma. Mbali na shule za umma, kuna shule nyingi za binafsi nchini, hasa katika sehemu za miji. Vilevile, kuna shule kadhaa za kimataifa zinazofundisha mifumo mbalimbali ya elimu ya ng'ambo.

Historia ya elimu

Mfumo wa kwanza wa elimu nchini Kenya baada ya uhuru uliletwa na wakoloni Waingereza. Baada ya nchi kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963, Tume ya Ominde iliundwa ili kuleta mabadiliko ambayo yaakisi matarajio ya taifa huru la Kenya. Tume hii ilimulika masuala ya usawa na umoja, ambayo yalikuwa muhimu hasa wakati huo. Mabadiliko ya kilichofundishwa katika historia na jiografia yalifanywa ili kuakisi umoja wa kitaifa. Kati ya miaka 1964 na 1985, mfumo wa 7-4-2-3 ulifuatwa (miaka saba masomo ya msingi, miaka minne sekondari ya daraja la chini, miaka miwili sekondari ya daraja la juu, na miaka mitatu masomo ya chuo kikuu). Shule zote zilifuatamtaala mmoja.

Mwaka wa 1981, kamati iliyoteuliwa na rais kuratibu namna ya kuanzisha chuo kikuu cha pili nchini Kenya, na pia kuubadilisha mfumo wa elimu kwa jumla, ilianza kazi yake. Kamati hii ilipendekeza kuwa mfumo ule wa 7-4-2-3 ubadilishwe kuwa mfumo wa 8-4-4 (miaka minane shule ya msingi, miaka minne shule ya upili, miaka minne elimu ya chuo kikuu). Jedwali lililo katika Elimu ya Sasa Nchini Kenya linaonyesha muundo wa mfumo wa 8-4-4. Ingawa mfumo wa 7-4-2-3 kinadharia ulifikia kikomo mfumo wa 8-4-4 ulipoanzishwa mwaka wa 1985, kundi la mwisho la mfumo huo wa awali lilihitimu kutoka vyuo vikuu vya Kenya mwaka wa 1992.

Elimu nchini Kenya sasa

Mfumo wa sasa wa 8-4-4 ilizinduliwa Januari 1985. Ulitilia mkazo masomo ya kiufundi kwa matarajio kuwa, muundo huu mpya utawawezesha wanaoacha shule katika viwango mbalimbali aidha kujiajiri wenyewe au kupata ajira katika sekta ya juakali.

Mnamo Januari 2003, Serikali ya Kenya ilitangaza kuanzishwa kwa masomo ya shule za msingi bila malipo. Hili lilipelekea kuongezeka kwa wanafunzi waliojiunga na shule za msingi kwa asilimia 70. Hata hivyo, idadi ya waliojiunga na shule za upili na vyuo haikuongezeka sana kwa sababu malipo bado yalihitajika ili kuhudhuria masomo.

Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya msingi nchini Kenya (KCPE) hufanywa katika darasa la nane. Matokeo ya mtihani huu huhitajika ili kusajiliwa katika shule ya upili. Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya shule ya upili nchini Kenya (K.C.S.E.) hufanywa katika kidato cha nne. Wanafunzi hufanya mtihani katika masomo nane.

Ukosoaji

Mfumo wa elimu wa Kenya 8-4-4 umepitia mengi magumu katika kipindi kirefu ulichodumu. Punde tu baada ya kufuzu kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa mfumo huu mwaka wa 1989, wananchi wengi walijitokeza kuilaumu na kuihukumu serikali kwa kuuanzisha mfumo huu. Wakosoaji hao walidai kuwa waliohitimu hawajaandaliwa vyema na hawangeweza kushindana na wenzao kutoka sehemu nyingine zaulimwengu. Wengine walihoji kuwa waliofuzu kupitia mfumo huu walikuwa aidha wachanga sana au hawajaandaliwa vyema kwa nafasi za kazi zilizokuweko. Serikali haikusikiliza hayo yote pengine kwa sababu uwezekano wa kuubadilisha na kuuunda upya kungeigharimu pesa nyingi.

Hata hivyo, kwa miaka mingi waliofuzu kupitia mfumo huu wamewaaibisha walioupinga kwa kufualu katika vyuo vya nchini na ng’ambo. Pia wasomi na wafanyakazi wa afya kuhamianchi zilizoendelea ni dhihirisho tosha la hali hii.

Mkazo uliotiliwa masomo ya ufundi umefifia na mabadiliko ya hivi juzi katika mtaala yanasisitizateknolojia yaupashanaji habari,sayansi,hesabu na lugha. Kwa vyovyote vile, kazi ya kiakademia na kusisitizwa kwa kupita mitihani iliyoandikwa hakujaacha nafasi kwauseremala,uashi,upishi na mafunzo mengine yaufundi.

Michezo

Makala kuu:Michezo ya Kenya
Timu ya kriketi ya Kenya
Timu ya rugby ya Kenya

Kenya hushiriki katikamichezo mbalimbali ikiwemokriketi,mbio za magari,soka,raga nangumi.

Lakini nchi hii inajulikana hasa kwa kutawala katikambio za masafa ya kadiri nambio za masafa marefu. Kenya, kwa muda mrefu, imetoamabingwa waOlimpiki namichezo ya Jumuia ya Madola katika nyanja mbalimbali, hasa katika mbio za mita 800, mita 1,500, mita 3,000 kuruka viunzi na maji, mita 5,000, mita 10,000 na mbio za masafa marefu.Wanariadha wa Kenya (hasa wa kabila la Wakalenjin) wanaendelea kutawala mbio za masafa ulimwenguni, ingawa ushindani kutoka nchi yaMoroko na Ethiopia umepunguza umaarufu huu.

Wanariadha wa Kenya wanaosifika sana ni pamoja na mshindi mara nne wa mbio za masafa marefu zaBoston kwawanawake na mshindi mara mbili wa mbio za duniaCatherine Ndereba, aliyeshikilia rekodi ya awali ya mbio za duniaPaul Tergat, naJohn Ngugi.

Wakati wa michezo ya Olimpiki yaBeijing Kenya ilishindamedali 6 zadhahabu, 4 zafedha, 4 zashaba na kulifanya taifa lililofaulu sana barani Afrika katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Wanariadha wapya walitambulikana, kamaPamela Jelimo, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 kwa wanawake aliyejitahidi na kushinda tuzo la Golden League, naSamuel Wajiru aliyeshinda mbio za masafa marefu kwa wanaume.

Bingwa mstaafu wa mbio za Olimpiki na za Jumuia ya Madola,Kipchoge Keino, alisaidia kuanza ubingwa wa mbio za masafa marefumiaka ya 1970 akafuatwa na bingwa wa michezo ya Jumuia ya Madola,Henry Rono, aliyeshikilia rekodi kadhaa za dunia.

Hivi majuzi, kumekuwa na mzozo wa wanariadha wa Kenya waliosaliti nchi yao na kuwakilisha nchi nyingine, hasaBahrain naQatar.Wizara ya michezo ya Kenya imejaribu kuzuia usaliti huu, lakini umeendelea tu,Bernard Lagat akiwa wa mwisho, akichagua kuiwakilishaMarekani.Usaliti huu, kwingi unatokana na sababu za kiuchumi au kifedha ingawa pia wanariadha wazuri wasioweza kufaulu katika timu nzuri ya taifa huona ni rahisi kufaulu kwa kukimbilia nchi nyingine.

Kenya pia imetawalavoliboli ya wanawake barani Afrika, huku vilabu natimu ya taifa vikishinda mashindano kadhaa barani Afrika katikamwongo uliopita. Timu ya wanawake pia imeshiriki katika michezo ya Olimpiki na Mashindano ya Ulimwengu ingawa haijafaulu vilivyo.

Mchezo wa kriketi ni maarufu na pia ni mchezo wa timu ambao umefaulu sana. Kenya imeshiriki katikaKombe la Dunia la Kriketi tangu mwaka1996. Timu hii ilishinda baadhi ya timu maarufu ulimwenguni na kufikiasemifainali katika mchuano wa mwaka2003 na wachezaji kama vileSteve Tikolo naMaurice Odumbe. Walishinda ligi ya kriketi ya dunia daraja la 1 iliyofanyika Nairobi kwa mara ya kwanza, kisha wakashiriki katika mchuano wa ulimwengu wa T20.Nahodha wa sasa wa timu niCollins Obuya.

Kenya imejiundia jina katika muungano wa raga na wachezaji kama vileCollins Injera naLucas Onyango. Mchezo huo ni maarufu nchini hasa kwa sababu ya mchuano wa kila mwaka wa Safari Sevens. Timu ya Kenya ya raga ya wachezajisaba kila upande ilikuwa nambari ya 9 katika michezo ya dunia ya wachezaji saba IRB katika msimu wa mwaka 2006.

Kenya ilikuwa bingwa wa soka katika eneo hili lakini ubingwa huu umefifia kutokana na kutoelewana kwa maafisa wa Kamati ya Soka Nchini.[39] Mizozo hii ilipelekea Kenya kupigwa marufuku na FIFA, lakini marufuku hii iliondolewa mnamo Machi 2007.

Kwa upande wa mbio za magari, Kenya ndio waandalizi wa mbio za magari maarufu zaSafari Rally zinazotambulika kuwa ngumu zaidi ulimwenguni,[40] na ambazo ni sehemu ya Bingwa wa Mbio za Magari kwa miaka mingi hadi kuondolewa kwake baada ya mbio za 2002 kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Baadhi yamadereva maarufu wa mbio za magari ulimwenguni walioshiriki na kushinda mbio hizi niBjorn Waldegard,Hannu Mokkola,Tommi Makinen,Shekhar Mehta,Carlos Sainz naColin McRae. Ingawa mbio hizi bado huendelea kila mwaka kama sehemu ya kutafuta Bingwa wa Mbio za Magari Afrika, waandalizi wanatarajia kuruhusiwa kujiunga tena na Ubingwa wa Magari Ulimwenguni katika miaka michache ijayo.

Uchumi

Makala kuu:Uchumi wa Kenya
Noti ya shilingi 20 ya mwaka 1994, ikimuonyesha Rais Daniel Arap Moi.

Baada ya uhuru, Kenya iliendeleza ukuaji wa kiuchumi haraka kupitia kwa uwekezaji wa umma, kuhimiza uzalishaji wa kilimo, na kushawishi uwekezaji wa watu binafsi na wageni katika viwanda. Pato la taifa lilikua kwa asilimia 6.6 kuanzia 1963 hadi 1973. Uzalishaji wa kilimo ulikua kwa asilimia 4.7 kila mwaka kwa kipindi hicho ukiwa umechochewa na ugawaji upya wa mashamba, kuanzishwa kwa kilimo cha mimea iliyoimarishwa, na kuanzisha mashamba mapya.

Hata hivyo, kati ya 1974 na 1993 ukuaji wa uchumi wa Kenya ulipungua. Kupungua kwa kilimo kulisababishwa na sera za kilimo zisizofaa, mikopo isiyotosha na vikwazo visiyofaa vya biashara ya kimataifa.

Mnamo mwaka wa 1993, Serikali ya Kenya ilianzisha mpango mkuu wa kuimarisha uchumi na kuufanya huru. Waziri mpya wa fedha na gavana mpya wa Benki Kuu ya Kenya walianza mikakati iliyofuatana kuimarisha uchumi kwa usaidizi waBenki ya Dunia naShirika la Fedha la Kimataifa). Kama sehemu ya mpango huu, serikali iliondoa usimamizi wa bei za bidhaa, leseni za uagizaji na uthibiti wa ubadilishaji fedha, kubinafsisha kampuni nyingi zilizomilikiwa na umma, kupunguza idadi ya wafanyi kazi wa serikali na kuanzisha sera madhubuti za kulinda fedha. Kuanzia mwaka wa 1994 hadi 1996 ukuaji halisi wa uchumi wa Kenya ulikadiriwa juu kidogo ya asilimia 4 kwa mwaka.

Hata hivyo, kati ya 1997 na 2000, uchumi uliingia kipindi cha kupungua au kutoimarika, kwa sababu ya hali mbaya ya anga na kupungua kwa shughuli za kiuchumi. Mwaka wa 2001 pato la taifa liliimarika kiasi kwani mvua ilirejea kunyesha karibu na viwango vya awali. Ukuaji wa kiuchumi uliendelea kuimarika kiasi mwaka wa 2002 na kufikia asilimia 1.4 mwaka wa 2003, asilimia 4.3 mwaka wa 2004, kisha asilimia 5.8 mwaka wa 2005.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, ambao ndio mkubwa zaidi na wenye shughuli nyingi zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.

Mnamo Julai 1997, Serikali ya Kenya ilikataa kutimiza makubaliano ya awali na IMF kuhusu mabadiliko ya utawala wake. Jambo hili lilisababisha kukatizwa kwa misaada kwa miaka 3, nayo Benki ya Dunia ikaubana mkopo wa dola milioni 90 za mpango wa kuufufua uchumi. Ingawa mabadiliko mengi ya kiuchumi yaliyofanywa kati ya 1993-94 yalibakia, wataalamu wa maswala ya kiuchumi wasiopendelea mabadiliko waliamini kuwa Kenya iliitaji mabadiliko zaidi, hasa ya kiutawala ili kuongeza ukuaji wa pato la taifa (GDP).

Serikali ya Kenya ilichukua hatua yakini za mabadiliko, pamoja na kuunda Tume ya Kupambana na Ufisadi (KACA), kuanzisha hatua za kuimarisha uwazi wa katika mikakati ya serikali kupata bidhaa na kupunguza fedha inayotumiwa na serikali kulipia mishahara. Mnamo Julai 2000, shirika la IMF lilitia saini dola milioni 150 za Poverty Reduction and Growth Facility (PRGF), nayo Benki ya Dunia ilifuatia na mkopo wa dola milioni 157 kuimarisha uchumi na kuibadilisha sekta ya umma. Mwezi wa Desemba 2000, iliamuliwa kuwa tume ya kupambana na ufisadi haikuwa ya kikatiba na sehemu za juhudi za mabadiliko kukatizwa mwaka 2001. Shirika la IMF na Benki ya Dunia zilikatiza mipango yao. Juhudi zilizofanywa kuanzisha upya mipango hii katikati ya mwaka wa 2002 hazikufaulu.

Chini ya uongozi wa Rais Kibaki, aliyechukua hatamu za uongozi tarehe 30 mwezi wa Desemba 2002, serikali ya Kenya ilianzisha mipango mipya na kabambe ya uimarishaji uchumi na imerejelea ushirikiano wake na Benki ya Dunia na IMF. Serikali mpya ya National Rainbow Coalition (NARC) iliidhinisha Sheria dhidi ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi pamoja na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma mnamo Mei 2003 iliyolenga kupiga vita ufisadi katika ofisi za umma. Mabadiliko mengine, hasa katika idara ya sheria, kuagiza bidhaa za umma na kadhalika yamepelekea kurejelewa kwa misaada na matumaini ya kuimarisha uchumi. Kufuatia kupitishwa kwa sheria muhimu za kupambana na ufisadi na serikali mpya, wafadhili walirejelea ufadhili mwezi wa Novemba 2003 na IMF ikaidhinisha msaada wa miaka mitatu wa dola milion 250 ili kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi. Wafadhili wakatoa dola bilioni 4.2 kama msaada wa miaka minnne. Kurejelewa kwa ufadhili na kujihusizisha upya kwao kumevutia imani ya wawekezaji.

Mswada waubinafsishaji umeidhinishwa ingawa kuanzishwa kwa tume ya ubinafsishaji hakujakamilika, mabadiliko katika utendakazi wa umma yametekelezwa na mwaka wa 2007 Kenya ilishinda tuzo la Umoja wa Kimataifa la Utendakazi wa Umma.[41][42] Hata hivyo, kazi nyingi zinahitajika kufanywa ili kuiwezesha nchi hii kuyafikia mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi, hasa yale ya Mashariki ya Mbali. Changamoto kuu ni pamoja na kuchukua hatua thabiti dhidi ya ufisadi, kupitisha sheria zinazoshughulikia ugaidi na biashara haramu, kutatua upungufu wa ufadhili wa bajeti kisha kurekebisha na kuunda miundo msingi. Inaaminika haya yatasaidia kudumisha sera za kimsingi za kiuchumi, na kuhakikisha ukuaji wa kasi wa kiuchumi uliofikia asilimia 7.2 mwaka wa 2007.

Mwaka wa 2007, serikali ya Kenya ilizinduaRuwaza 2030, ambao ni mpango wa kiuchumi wenye matumaini makuu na ambao ikiwa utatekelezwa kikamilifu, una uwezo wa kuifanya nchi hii kuwa katika kiwango sawa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi ya Asia.

Nairobi inaendelea kuwa kituo muhimu na cha kimsingi kwa mawasiliano na biashara cha Afrika Mashariki. Kinajivuna kuwa na miundo msingi ya uchukuzi na mawasiliano bora zaidi katika eneo hili, na wafanyi kazi wenye ujuzi. Makampuni mengi ya kigeni hudumisha matawi yao katika eneo hili ama ofisi za kuyawakilisha mjini Nairobi. Mnamo Machi 1996, Marais wa Kenya, Tanzania na Uganda waliifufua Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Shabaha za EAC ni pamoja na kusawazisha kodi na ada zinazotozwa bidhaa, utembeaji huru wa watu na kuimarisha miundo msingi katika eneo hili. Nchi hizi tatu za Afrika Mashariki zilitia saini mkataba wa Customs Union Agreement mwezi wa Machi 2004.

Mji wa Nairobi
Muhtasari wa uchumi wa nchi
Pato la taifaDola bilioni 41.84 (2012) kwa bei ya sasa. Dola bilioni 76.07 (Uwezo wa kununua bidhaa usio sawa, 2012) Kuna pia uchumi mkubwa usio rasmi ambao haujawahi kujumuishwa kama sehemu ya pato la taifa.
Ukuaji wa kiuchumi kwa mwaka5.1% (2012)
Pato la kila mtu kwa mwakaPato la kila mtu kwa mwaka (PPP)= $1,800
Malighafi ya kiasiliWanyama wa pori, Ardhi (5% inayolimika)
Bidhaa za kilimoChai, kahawa, mahindi, ngano, miwa, mboga na matunda, pareto, bidhaa za maziwa, nyama na bidhaa za wanyama
ViwandaBidhaa za petroli, usagaji wa nafaka na miwa, saruji, pombe, vinywaji, nguo, uunganishaji magari, makaratasi, utengenezaji wa bidhaa za kimsingi, utalii
Biashara ya mwaka 2012
BiasharanjeDola bilioni 5.942chai, kahawa, bidhaa za mboga na matunda, bidhaa za petroli, saruji, samaki
Masoko muhimu (2012)[1]Uganda, Tanzania, Uholanzi, Uingereza, Marekani, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
MaduhuliDola bilioni 14.39mashine, magari, bidhaa za petroli, vyuma, resini na bidhaa za plastiki
Mataifa muhimu yaletayo bidhaa Kenya  China, Uhindi, Muungano wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Ujapani

Utafutaji wa mafuta

Mwanzoni mwa mwaka wa2006 Rais waUchina,Hu Jintao, alitia saini kandarasi ya utafutaji wa mafuta na Kenya. Haya ndiyo makubaliano ya hivi punde kati ya mfululizo wa mapatano yaliyopagwa kuelekeza maliasili ya Afrika huko Uchina ambako uchumi wake waendelea kukua kwa haraka.

Kandarasi hii iliwezesha kampuni inayoongozwa na taifa la Uchina “offshore oil and gas company” CNOOC Ltd kutafuta mafuta Kenya, ambayo ilianza kuchimba visima vya kwanza mpakani mwa Sudan na Somalia na katika maji ya upwa wake.[43]

Tazama pia

Marejeo

  1. 123"Kenya".The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2026).Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo2024-03-30. (Archived 2023 edition)
  2. Knbs."Kenya population 2024" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2025-04-02.
  3. "2019 Kenya Population and Housing Census Volume IV: Distribution of Population by Socio-Economic Characteristics".Kenya National Bureau of Statistics.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Juni 2020. Iliwekwa mnamo24 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1234"World Economic Outlook Database, April 2025 Edition. (Kenya)".IMF.org.International Monetary Fund. Aprili 2025. Iliwekwa mnamo2025-04-22.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Human Development Report 2023/24"(PDF) (kwa Kiingereza).Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa. 13 Machi 2024. uk. 289. Iliwekwa mnamo13 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "East Africa: Kenya: History: Kenya Colony".Encyclopedia Britannica. Juz. la 17 (tol. la 15). 2002. ku. 801, 1b.ISBN 0-85229-787-4.
  7. Rough Guide Map Kenya (Ramani) (tol. la 9). 1:900,000. Rough Guide Map. Usanifu ramani wa World Mapping Project. Rough Guide. 2006.ISBN 1-84353-359-6.
  8. "Free topographic maps, elevation, terrain".Topographic maps (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2024-04-03.
  9. 123Climates to Travel."Climate in Kenya" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2024-04-03.
  10. ,ABC News Online, 2005/03/10
  11. 123Wonders wa Afrika World -PBS
  12. Hybrid Urbanism By Nezar Al-Sayyad
  13. Dispersal Afrika katika Deccan By Shanti Sadiq Ali
  14. Kiswahili Coast.Ilihifadhiwa 30 Desemba 2007 kwenyeWayback Machine. Nationalgeographic.com.
  15. Sultani wa Malinda, PBS
  16. "Ismaili muslim". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-01-03. Iliwekwa mnamo2021-01-16.
  17. Sikh
  18. Reuter (8 Julai 1920). "News".British East Africa Annexed--Kenya Colony. uk. 13.
  19. Foottit, Claire (2006) [2004].Kenya. The Brade Travel Guide. Bradt Travel Guides Ltd.ISBN 1-84162-066-1.
  20. "Kenya".Oxford English Dictionary. Oxford University Press. 2nd ed. 1989.
  21. The Spelling ya Kenya. BJ Ratcliffe. Journal ya Royal African Society, Vol. 42, Namba 166 (Januari 1943), uk. 42-44
  22. Foottit, Claire (2006) [2004].Kenya. The Brade Travel Guide. Bradt Travel Guides Ltd.ISBN 1-84162-066-1.
  23. Castro, Alfonso Peter (1995).Facing Kirinyaga. London: Intermediat Technology Publications Ltd.ISBN 1-85339-253-7.
  24. "Tunataka nchi yetu"Ilihifadhiwa 23 Julai 2013 kwenyeWayback Machine.. Wakati. 5 Novemba 1965.
  25. Kenya, AfricaGenWeb
  26. Post-Uhuru Low intensiteten Conflict Nchini Kenya
  27. E. H., Campbell (2006)."Urban Refugees in Nairobi: Problems of Protection, Mechanisms of Survival, and Possibilities for Integration".Journal of Refugee Studies.19 (3): 396.doi:10.1093/jrs.
  28. Wapiga kura wengi kukaa nyumbani kama Kenya Drops Secret Ballot katika Uchaguzi Parliamentaryhttp://www.highbeam.com/doc/1P2-1241691.htmlIlihifadhiwa 15 Februari 2011 kwenyeWayback Machine.: The Washington Post Kifungu tarehe: 25 Februari 1988 Author: Blaine Harden
  29. religiousfreedom.lib.virginia.edu / rihand / Kenya.html
  30. ghasia za uchaguzi Kenya unatishia mafanikio yake ya kiuchumihttp://www.chinadaily.com.cn/language_tips/auvideo/2008-01/07/content_6375707.htm
  31. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-07-15. Iliwekwa mnamo2009-12-07.
  32. 'Hope is back' kwa Kenya - CNN.comIlihifadhiwa 5 Machi 2008 kwenyeWayback Machine. saa edition.cnn.com
  33. wabunge Kenya kupitisha sheria ya kugawana madaraka-english.aljazeera.net/NR/exeres/111A3F40-0FD9-4DCB-ACB0-822D1E3A09EA.htm Al Jazeera Kiingereza 18 Machi
  34. Horror ya Kenya's 'Witch' lynchings
  35. Mob nzito kifo 11 Kenya 'witches'
  36. Kenya Roads BoardConstituency ufadhili chini ya RMLFIlihifadhiwa 13 Januari 2008 kwenyeWayback Machine.
  37. "2019 Kenya Population and Housing Census Volume III: Distribution of Population by Age and Sex".Kenya National Bureau of Statistics.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo8 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  38. http://www.state.gov/g/drl/rls/irf/2008/108374.htm US Department of State
  39. New Vision, 3 Juni 2004:Wrangles ardhi Kenya utan fastställd FIFA marufukuIlihifadhiwa 10 Januari 2008 kwenyeWayback Machine.
  40. The Auto Channel, 21 Julai 2001:FIA Rally: Delecour inachukua pointi kumaliza tarehe Safari Rally kwanza
  41. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2008-02-15. Iliwekwa mnamo2009-12-07.
  42. "Nakala iliyohifadhiwa"(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo(PDF) mnamo 2009-03-24. Iliwekwa mnamo2009-12-07.
  43. Barber, Lionel (10 Agosti 2006)."China's scramble for Africa finds a welcome in Kenya". Financial Times. Iliwekwa mnamo2008-06-27.

Viungo vya nje

Kenya portal
Serikali
Jumla
Vyombo vya habari
Utalii
Historia
Nyingine
Mada kuhusuKenya
Historia
Siasa
Jiografia
Uchumi namiundombinu
Demografia na jamii
Utamaduni


Nchi zaAfrikaBara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
Nchi wanachama waUmoja wa Afrika (AU)
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kenya&oldid=1479505"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp