Inafafanuliwa kamautendaji unatumianguvu yaakili au yamwili ili kufikia lengo fulani, ambalo mara nyingi nifaida yakiuchumi ili kuweza na kuwezesha kuendelea kuishi.
Kwa msingi huo, niwajibu wa kila mtu aliyefikiaukomavu fulani.
Ni pia mchango muhimu katikajamii na inayostahili kuheshimiwa na kutunzwa na wote kuanziaserikali hadi watu binafsi.
Kwa kuwa ni wajibu, kazi ni vilevilehaki ya msingi ya binadamu. Bila kuwa nayo, mtu anaelekea kunyong'onyea na kujiona hama maana, hasa kamautovu wa kazi unadumu muda mrefu na kumzuia asiweze kupangamaisha yake, kwa mfano upande wandoa nafamilia, kwa sababu ya kutojitegemea.
Biblia inazungumzia maisha halisi ya watu, hivyo haikuweza kuisahau kazi. Tokakitabu cha Mwanzo (1:1-2:4a) inaonyeshaheshima ya kufanya kazi kwa kumchoraMungu akitenda kazi kama binadamu kwasikusita, akipumzika ile yasaba.
Ndiye aliyewaagizaAdamu naEva wafanye kazi katikadunia ili kuistawisha (Mwa 2:15).
Baada yadhambi ya asili waliyoifanya wajibu huo umebaki, ila kamaadhabu sasa unachosha (Mwa 3:17-19).
Mtume Paulo alipinga kwa nguvuuzembe wa waliodai kazi haihitajiki tena kwa sababu eti,ufalme wa Mungu umefika. Aliandika, "Asiyetaka kufanya kazi, asile chakula" (2Thes 3:10).[1] Mwenyewe, pamoja na kuhubiriInjili alikuwa akiendelea na kazi yake yakushonamahema ili kupata mahitaji yake bila kulemea wengine.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.