Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kasoko ya Chicxulub

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha kutoka kwa chomboanga chaNASA zinaonyesha sehemu ya mzingo wa kasoko.[1]


Kasoko ya Chicxulub (tamkachik-shulub) nikasoko kubwa ya dharuba kwenyepwani yarasi ya Yucatan katikaMeksiko, iliyosababishwa na pigo laasteroidi miakamilioni 66 iliyopita. Inaaminiwa ya kwamba tukio hilo lilisababisha kuangamia kwadinosauri pamoja naspishi nyingine nyingiDuniani.

Kasoko hii inakipenyo cha zaidi yakm 180, hivyo ni kasoko kubwa yatatu duniani iliyosababishwa na dharuba yaasteroidi (en:impact crater)[2] Asteroidi iliyogonga huko ilikuwa na kipenyo cha angalaukm 10. Pigo hilo lilisababishatsunami, kuwaka kwamoto katika sehemu nyingi za Dunia,matetemeko ya ardhi na kulipuka kwavolkeno nyingi. Kutokana navumbi namajivu yaliyorushwaanganinuru yajua ilizuiliwa na hivyo kilitokea kipindi kirefu chagiza nabaridi kali kote duniani.[3]

Kasoko haionekani tena kwamacho au kutokandege maanammomonyoko kwenye uso wa ardhi umeshasawazishamilima na kufukia shimo. Lakinivipimo vinaonyesha mabadiliko katikamiamba ya eneo hilo na mabadiliko katikauga wagraviti ya eneo hili yanayotokana nadensiti kubwa ya miamba pale ambako pigo lilikandamiza mwamba.Umri wa mwamba ulipimwa na kukadiriwa kuwa takriban miaka milioni 65 - 66. Umri huo unalingana na kupotea ghafla kwa spishi nyingi kote duniani jinsi inavyoonekana katika mabaki yakisukuku.[4][5]

Marejeo

  1. "PIA03379: Shaded Relief with Height as Color, Yucatan Peninsula, Mexico".Shuttle Radar Topography Mission.NASA. Iliwekwa mnamoOktoba 28, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Earth Impact Data Base:Ilihifadhiwa 12 Februari 2010 kwenyeWayback Machine.
  3. Climate model simulations of the effects of the asteroid impact at the end of the Cretaceous, Brugger, J., G. Feulner, and S. Petri (2017), Baby, it's cold outside: Climate model simulations of the effects of the asteroid impact at the end of the Cretaceous, Geophys. Res. Lett., 44, 419–427, doi:10.1002/2016GL072241.
  4. Schulte, Peter; na wenz. (5 Machi 2010)."The Chicxulub Asteroid Impact and Mass Extinction at the Cretaceous-Paleogene Boundary".Science.327 (5970). AAAS: 1214–1218.doi:10.1126/science.1177265.ISSN 1095-9203.PMID 20203042. Iliwekwa mnamo5 Machi 2010.{{cite journal}}:Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help);Explicit use of et al. in:|first= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kasoko_ya_Chicxulub&oldid=1353517"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp