Karafuu (kutokaKiarabu قَرَنْفُلqaranful[1]) nimatumba (macho yamaua) makavu yamikarafuu ambayo nimiti yafamilia yaMyrtaceae.
Karafuu hutumiwa kamakiungo chachakula na chanzo chamafuta yenyeharufu inayopendwa nawatu wengi.
Asili ya mti na pia matumizi ya matumba nivisiwa vyaIndonesia. Katikakarne ya 19 mikarafuu ilipelekwaUnguja naPemba hasa namtawala waOmani na kuanzishauzalishaji mkubwa saa wa karafuu kwenye visiwa hivi.
Karafuu hutumiwa katikaupishi wa nchi nyingi zaAsia,Afrika,Ulaya na hataAmerika. Hutumiwa katika kupikanyama, curry namichuzi mbalimbali pamoja na kupikamatunda pamoja navinywaji. Ni kiungo cha lazima kwenyepilau.
Hutafunwa piamdomoni kuboresha harufu yapumzi.
Kutafuna karafuu nidawa ya kupunguzamaumivu yameno.
Nchini Indonesiasigara huungwa na mafuta ya karafuu.
Karafuu zilifanyiwabiashara tangu kale. Kunaushuhuda wa karafuu katika chombo kilichopatikana nchiniSyria kilichogunduliwa kuachwa huko mnamo mwaka1721 KK[2].
Kunataarifa ya kwamba mtawala nchiniChina alitaka watu wanaotaka kuongea naye watafune karafuu ili wawe na pumzi ya kupendeza.[3]
Katikakarne ya 17 karafuu ilikuwa kati ya vivutio vyakiuchumi vilivyoletaUholanzi kuanzishamakoloni yake kwenye visiwa vya Indonesia.
Katikakarne ya 18MfaransaPierre Poivre alifaulu kuibamiche ya mikarafuu na kuipelekaMorisi ambakoWafaransa walianzishakilimo hicho.
Soko la karafuu lilikuaduniani na hii ilikuwachangamoto yaSultani wa Omani kupeleka miti hiyoUnguja na Pemba iliyoendelea kuwa nchi ya kuzalisha karafuu nyingi zaidi duniani na kuundautajiri wa Zanzibar ilhali kilimo hicho kilichochangia pia katikabiashara ya watumwa waliotumiwa kuzalishazao hili katika karne ya 19.[4]
Mapato ya karafuu yalimsababishaSaid bin Sultani kuhamishamakao makuu yake Unguja na baada yakifo chakeUsultani wa Zanzibar ulianzishwa kama nchi ya pekee na Omani.