Baada yafarakano hilo, yalifanyika mabadiliko mbalimbali upande waimani,ibada nasheria kuelekeaUprotestanti. Hata hivyo mwelekeo wa Kikatoliki uliendelea kuwepo, na bado una nguvu, hasa katika baadhi yadayosisi. Hasa miaka hii ya mwisho mvutano kati ya pande hizo mbili umeongezeka hata kusababisha umoja kulegea.
Katika karne zilizofuata, kutokana na uenezi wa himaya ya Uingereza duniani, Anglikana ilienea sehemu nchi, na leo ina wafuasi wengi hasaAfrika (Nigeria,Uganda n.k.). Kwa jumla wanazidimilioni 85 katika nchi 165.
Majimbo yake 38 yanajitegemea, lakini yanaundaushirika mmoja. Maaskofu wake wote wanakutanaLambeth kila baada ya miaka 10 chini yaAskofu mkuu waCanterbury.
Alikuwa Mkatoliki aliyependaKanisa lake. Lakini alikuwa na matatizo mawili juu yaPapa waRoma.
Kwanza kabisa Uingereza ulikuwa nawajibu wa kumlipa Papa kilamwakakodi ya pekee, tofauti na mataifa mengine yaUlaya.
Pili, huyo mfalme alikuwa na tatizo la binafsi: alishindwa kuzaliana namke wakemtotowa kiume atakayerithiufalme. Basi, akamwomba Papa apatekumwoa mwingine, lakini Papa alikataa kutokana nasheria za Kanisa.
Henri, aliyekuwa mtu wahasira, aliitishaBunge la Uingereza akawalazimishawabunge kutangaza kwamba mfalme ndiye mkuu wa kanisa nchini. Halafubunge lilikubalitalaka yake.
Azimio lingine lilikuwa kutolipia tena kodi kule Roma, hivyo ikaingia katikamfuko wa Mfalme mwenyewe. Lakini Henri hakupenda mabadiliko katika mafundisho yaimani nadesturi zaibada.
Baada yakifo chake viongozi wa taifa waliamua kutengeneza kanisa kwa jumla. Hasanyumba zawatawa zilifungwa namali zao zikachukuliwa na mfalme.
Askofu Mkuu Cranmer akachukua mafundisho mengi ya Luther naCalvin, lakini katika desturi za nje alibadilisha taratibu chache tu.
Hivyo Kanisa la Uingereza likajitokeza kuwa na hali mbili. Wale wanaokaza sana urithi wa kale pamoja naliturujia (mavazi ya wachungaji, kupiga magoti, kufanyaalama yamsalaba kwamkono wakati wasala, kutunza kumbukumbu yawatakatifu) wanaitwa "High Church (Kanisa la juu)". Waanglikana wengine, waliovutwa zaidi namatengenezo ya Kiprotestanti na kutojali sana urithi wa kale wanaitwa "Low Church (Kanisa la chini)".
Kwa mambo ya nje wale wa "juu" wanafanana na Wakatoliki, na wale wa "chini" wanafanana zaidi na Wareformati. Lakini Waanglikana hujisikia kuwa naumoja; kwa kweli walifaulu kuliko madhehebu mengine kuunganisha pande zote mbili na kuepuka hatari ya kufarakana kama ilivyotokea mahali pengine.
Waanglikana wako katika nchi zote zilizokuwa chini yaukoloni wa Kiingereza, kwani hukowamisionari wao waliweza kufanya kazi kwa urahisi.
"Majimbo" ya Waanglikana (Jimbo laTanzania, Jimbo laKenya, Jimbo laUganda n.k., kila jimbo likiwa na madayosisi mbalimbali) hujitegemea, pamoja na kumkubali Askofu waCanterbury (Uingereza) kuwa kiongozi wa kiroho kamamwenyekiti wa maaskofu wa Kianglikana lakini hanautawala.
Siku hizi Waanglikana waMarekani wamekuwa wa kwanza kumbarikiaskofu wa kike (niMnegro) na askofushoga, lakini katika suala la kupokeawanawake katikaukasisi nauaskofu na vilevile katika suala la ushoga majimbo yao yametofautiana kiasi cha kuelekeafarakano.
Kwa sababu hizo, mnamo Januari2016, Jimbo la Marekani lilisimamishwa kwa miaka 3.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuWaanglikana kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.