Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kanaani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wakanaani walivyochorwa naWamisri katika karne ya 13 KK.

Kanaani ni jina la zamani la eneo laMashariki ya Kati ambalo siku hizi limegawanyika katika nchi zaIsraeli naPalestina,Lebanoni na sehemu zaMagharibi zaJordan naSirya.

KatikaBiblia jina hilo (kwaKiebrania כנען, knaʿn) linatumika zaidi kumaanisha sehemu ile tu ambayo ilitekwa naWaisraeli na kuitwaIsraeli. Sehemu hiyohiyo baadaye tena ilikuja kuitwa piaPalestina, yaani nchi yaWafilisti.

Baada ya mataifa hayo mawili kuteka sehemu kubwa upande wa Kusini kuanziakarne ya 13 KK, ile ya Kaskazini zaidi iliyobaki chini ya wakazi asili ilikuja kuitwa piaFoinike.

Katika eneo hilo kati yaMesopotamia naMisri kuanziamilenia ya 4 KK ulistawiustaarabu muhimu waKisemiti ambao, kati ya michango mingine, ni asili yaalfabeti.

Habari nyingi kuhusu ustaarabu huu zimejulikana hasa kwa njia yaakiolojia.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kanaani&oldid=1231887"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp