Kalimantan (inajulikana pia kwa jina laBorneo ya Indonesia) ni sehemu kubwa yakisiwa chaBorneo iliyopoIndonesia.[1] Sehemu hii niasilimia 73 za eneo lote la kisiwa hicho. Sehemu nyingine zisizo za Indonesia niBrunei naMalaysia yaMashariki.
Jina laKalimantan (piaKlemantan) linatokana nalugha ya {{Kisanskrit]]:Kalamanthana ikimaanisha kisiwa chenyehali ya hewajoto sana. Linafanywa na maneno mawili:kal(a) (wakati. majira) namanthan(a) (moto sana, ya kuchoma).[2]
Sehemu hii ya Indonesia ina asilimia 73 (km² 544,150[3]) za kisiwa chote cha Borneo na 69.5% (watu 13,772,543 wakati wasensa ya 2010) za wakazi wa kisiwa hiki. Sehemu zisizo za Kiindonesia ni Brunei (wakazi 400,000) naMalaysia ya Mashariki (wakazi 5,625,000) inayokumlisha majimbo yaSabah,Sarawak na eneo laLabuan.