Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kaizari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Julius Caesar alikuwa asili ya cheo cha Kaizari.
Kaizari Augusto waDola la Roma.
Mtawala waUfaransaNapoleon Bonaparte aliyejiwekea taji la Kaizari 1804.

Kaizari nicheo chamfalme mkuu.Neno laKiswahili limetokana nalugha yaKijerumani "Kaiser", lakini asili yake niKilatini "Caesar".

Asili ya Kiroma

[hariri |hariri chanzo]

Asili ya cheo niJulius Caesar aliyekuwa kiongozi waDola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka44 KK.

Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwaheshima yake hadi jina likawa cheo.

Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola laRoma ya Mashariki (Bizanti) hadi mwaka1453.

Ulaya

[hariri |hariri chanzo]

KatikaUlaya yenyewemfalme waWafarankiKarolo Mkuu alipokea cheo cha "Caesar" au Kaizari. Baadaye wafalmeWajerumani waliomfuata Karolo Mkuu katika sehemu yamashariki yaufalme wake waliendelea kutumia cheo hiki cha Caesar au Kaizari.

Neno la Kaizari liliingia katika lugha ya Kiswahili wakati waukoloni wa Kijerumani hukoTanzania, kwa kuwaAustria naUjerumani zilitawaliwa hadi mwisho waVita Kuu ya Kwanza ya Dunia1918 na wafalme wenye cheo cha "Kaizari".

Vilevile mfalme waUrusi alikuwa na cheo kilekile kilichoitwa "Tsar" kwaKirusi, ilhali neno hili limeundwa pia kutoka "Caesar".

Lugha zaKiingereza naKifaransa zilitumia cheo tofauti cha macaesar wa Kiroma, ndicho "Imperator" (= mwenye amri, mwenye mamlaka, jemadari) kilichokuwa "Emperor" kwa Kiingereza au "Empereur" kwa Kifaransa.

Nje ya Ulaya

[hariri |hariri chanzo]

Kaizari ni cheo cha mfalme aliye juu ya wafalme wengine. Kutokana na uzoefu huu hataShah waUajemi,Tenno waJapani,Huangdi waChina naNegus Negesti waEthiopia hutajwa kwa cheo cha "Kaizari".

MalkiaViktoria wa Uingereza alitumia cheo cha Kaizari ("empress") kama mtawala waUhindi tangu mwaka1877.

Wakati waukoloni mtawala mkuu waAfrika ya Mashariki ya Kijerumani alikuwaKaizari Wilhelm II wa Ujerumani; kwenyesarafu yarupia alionyeshwa pamoja cheo kwa lugha yaKilatini "imperator".

RaisJean-Bedel Bokassa alijitangaza kuwa Kaizari ("empereur") waAfrika ya Kati mwaka1977 akiiga mfano waNapoleon Bonaparte aliyejiwekeataji la Kaizari yaUfaransa mwaka1804. Bokassa alipinduliwa mwaka1979 na nchi kuwajamhuri tena.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kaizari&oldid=1390924"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp