Mfano wa uso wa kadi karadha: 1. Logo ya benki iliyotoa kadi 2.Chipu (kwenye "kadi janja") 3. Alama ya usalama (hologramu) 4. Namba ya kadi 5. Logo ya kadi 6. Tarehe ya kumalizika kwa kadi 7. Jina la mwenye kadi 8. Chipu
Mtoaji wa kadi (kawaida huwa nibenki) anatoamikopo kwa mmiliki wa kadi ambaye hulipa benki baadaye.Malipo yake hujumuishariba.
Mkabidhi kadi (benki) huundaakaunti mzunguko na kumpa mmliki kadimikopo ainati ambayo mwenye kadi anaweza kukopafedha za kulipiaununuzi au fedha anazozihitaji.
Kwa maneno mengine, kadi ya mkopo hujumlisha kufanya malipo pamoja na mikopo zaidi.
Miundo tata ya anda katikaviwanda vya kadi ya mkopo yaweza kumzuiamteja uwezo wa kulinganishamaduka, hii ni njia ya kuhakikisha kuwa viwanda hivi havina mashindano yabei hivyo kupatafaida iliyo juu.
Kutokana na wasiwasi wa shughuli kama hizo,sheria nyingi zimetumika kudhibiti malipo ya kadi za mkopo.
Kadi ya mkopo ni tofauti na kadi ya kulipa (charge card) ambayo huhitaji kulipa matumizi yote kwa ukamilifu baada yamwezi, kinyume na kadi ya mkopo unaomwezesha mtumizi kuendelezadeni kulingana na riba anayotozwa juu yake.
Kadi ya mkopo pia ni tofauti na kadi ya fedha (cash card) ambayo inaweza kutumiwa na mwenye kadi kamasarafu.
Kadi ya mkopo pia ni tofauti na kadi ya malipo kwa kuwa kadi ya mkopo inahusisha mhusika wa tatu (benki) anayelipa muuzaji na baadaye anarejeshewa fedha hizo na mnunuzi, ilhali kadi ya malipo mnunuzi huchelewesha tu malipo hadi siku nyingine.
Dhana ya kutumia kadi kufanyia malipo ilielezewamwaka1887 naEdward Bellamy katika novela yakeLooking Backwards. Bellamy alitumiamsamiati ‘kadi ya mkopo’ marakumi na moja kwa novela hii ilhali alikuwa akirejelea kadi iliyotumika na wananchi kutumiapesa walizopewa naserikali pasipo kukopa, hivyo kufanya sawa na kadi ya debit.
Hatari kuu katika utumizi wa kadi ya mikopo niwizi wa kadi yenyewe aumaandishi yaliyomo kama vilejina,nambari ya akaunti ya benki naanwani yako.Wanaotumia kadi hizi huombwa kuwa makini zisije zikaibwa wakajikuta wameporwa pesa zao au kadi zao zikafanya manunuzi na mikopo bila ya wao kujua. Wizi huu hujulikana kamaidentity theft. Kuukwepa wafaa kujulishakampuni iliyokupa kadi mara moja baada ya kuibiwa kadi. Wafaa pia uweke kadi yako mahala pema ambapo haitaporwa[1].
Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKadi karadha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.