Tangu kufufuliwa kwake, Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanzisha hatua mbalimbali muhimu za ujumuishaji, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha mwaka 2005, Soko la Pamoja mwaka 2010, na juhudi zinazoendelea kuelekea Muungano wa Fedha na hatimaye Shirikisho la Kisiasa. EAC pia imekuwa ikifanya kazi ya kuoanisha sera katika sekta kama usafiri, afya, elimu, na nishati. Ikiwa na jumla ya watu wanaozidi milioni 300 na msisitizo wa pamoja juu ya maendeleo ya kikanda, EAC ina nafasi inayoongezeka katika masuala ya bara na inachukuliwa kama mfano wa ushirikiano wa kikanda barani Afrika.[1][2][3][4]
Kwa sasa eneo la Mtangamano nikm2 4,810,363, likiwa na wakazi 312,362,653 (kadirio la mwaka2022), hivi kwamba ingekuwa nchi moja tu ingekuwa yanneduniani.
Demografia
Idadi ya Watu
Jumuiya ya Afrika Mashariki ina idadi ya watu takriban milioni 333.93 ambapo aslimia 31 wanaishi katikaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ,Sudan Kusini ndiyo iliyo na watu wachache sana ikiwa na watu takriban milioni 11.48 .Asilimia ya wakazi wanaoishi mijini ni 20 tu, lakini wanaongekeza kwa 4.71% kila mwaka
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Idadi ya watu
Kongo JK 105.83 (31.7%)
Tanzania 66.62 (19.9%)
Kenya 55.53 (16.6%)
Uganda 48.86 (14.6%)
Somalia 18.36 (5.49%)
Rwanda 13.95 (4.17%)
13.69 (4.09%)
Sudan Kusini 11.48 (3.43%)
[{"value":105.83,"color":"#36A","label":"Kongo JK $v"},{"value":66.62,"color":"#1A9","label":"Tanzania $v"},{"value":55.53,"color":"#6A5","label":"Kenya $v"},{"value":48.86,"color":"#CC5","label":"Uganda $v"},{"value":18.36,"color":"#928","label":"Somalia $v"},{"value":13.95,"color":"#E33","label":"Rwanda $v"},{"value":13.69,"color":"#E72"},{"value":11.48,"color":"#E79","label":"Sudan Kusini $v"}]
{"legend":true,"caption":"Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Idadi ya watu","size":200}
Ukristo ndiyo dini kubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa na wafuasi milioni 261.86 na asilimia 79% ya watu wa EAC,Kongo,JK ndio iliyo na wafuasi wengi takriban milioni 100 au asilimia 95.4 .Uislamu ina wafuasi takriban milioni 56.69 ambayo ni asilimia 16.98 ya watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiongozwa naSomalia ambapo 99 ni waislamu.Dini za jadi ni asilimia 2.4% haswaaSudan Kusini ambapo asilimia 35 ni wafuasi wadini za jadi,Wasio na dini ni asilimia 1.75%
Mgawanyo wa Dini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ukristo 261.86 (78.4%)
Uislamu 56.69 (17.0%)
Dini za Jadi 8 (2.40%)
Wasio na Dini 5.83 (1.75%)
Zingine 1.53 (0.46%)
[{"value":261.86,"color":"#36A","label":"Ukristo $v"},{"value":56.69,"color":"#1A9","label":"Uislamu $v"},{"value":8,"color":"#6A5","label":"Dini za Jadi $v"},{"value":5.83,"color":"#CC5","label":"Wasio na Dini $v"},{"value":1.53,"color":"#E33","label":"Zingine $v"}]
{"legend":true,"caption":"Mgawanyo wa Dini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki","size":200}
Kiswahili,Kiingereza naKifaransa ndizo Lugha rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kiswahili hutumika kama Lingua Franca katika nchi hizi hukuKiingereza naKifaransa zikitumika kama lugha za kufundishia shuleni. Lugha za Jumuiya ya Afrika mashariki zimegawanyika katika kundi tatu ambazo ni Lugha zaKibantu ambayo ndiyo kundi kubwa ya Lugha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Lugha za Kinilotiki na Lugha za Kikushi.
Mijini na Vijijini
Asilimia ya watu walioishi mijini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni 35% na walioishi Vijijini asilimia 64%.Somalia naJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndizo nchi zilizokuwa na asilimia kubwa ya wakazi wa mijini zikiwa na asilimia 46% na 45% mtawaliwa.Burundi naSudan Kusini ndizo nchi zilizokuwa na wakazi wa mjini wachache sana zikiwa na asilimia 13% na 17% ya wakazi wanaoishi mijini huku asilimia 86% na 82% mtawaliwa wakiishi vijijini.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yenye makao yake makuu Arusha, Tanzania,kazi yake kuu ni kuendeleza muungano wakiuchumi,kisiasa, nakijamii katika ukanda huu. Mwenyekiti wa sasa wa EAC niWilliam Ruto,Rais wa Kenya, anayeongoza Mkutano wa Wakuu wa Nchi, ambao ndio chombo cha juu zaidi cha maamuzi katika jumuiya hii.
Kwa miaka iliyopita, EAC imepiga hatua muhimu ikiwemo kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, na mikataba ya kuunda Umoja wa Fedha. Pia imeongeza uanachama wake, ikiwemo kuipokeaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ,Somalia naSudan Kusini. Miradi mikubwa ya miundombinu ya kikanda, programu za kurahisisha biashara, na ushirikiano katika sekta za afya na usalama ni miongoni mwa mafanikio yanayoonyesha ushawishi unaokua wa jumuiya hii katika kuendesha mipango ya maendeleo yaAfrika Mashariki.
Historia
Jumuiya ya kwanza
Nchi tatu za Afrika ya Mashariki zilizokuwa chini yautawala waUingereza zilianzauhuru wao kwa kuendelezaushirikiano wa karibu uliorithiwa kutokana nautawala wa pamoja wakati waukoloni.
Lakini mielekeo ya nchi zote tatu zilitofautiana mno: Kenya iliendelea kwa njia yaupebari lakini Tanzania ilijaribu kujengaUjamaa (usoshalisti) kuanzia mwaka 1967. Uganda uliingia katika kipindi chaudikteta kali yaIdi Amini aliyeharibuuhusiano na majirani alipoanza kudai sehemu za maeneo yao.
Sababu nyingine ni madai ya Kenya ya kuwa na viti zaidi kuliko Uganda na Tanzania katikakamati za maamuzi,[5] huku kukiwa na kutokuelewana kulikosababishwa na udikteta waIdi Amin nchini Uganda, Usoshalisti huko Tanzania, nasoko huria nchini Kenya,[2] hivyo wanachama hawa watatu wakapoteza ushirikiano wa miaka zaidi ya sitini namanufaa yaukubwa wa jumuiya hii kiuchumi. Kila mmoja wa wanachama hawa ilimbidi kuanza kutoahuduma na kujenga viwanda ambavyo hapo awali vilikuwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hivyo mwaka1977 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikoma kufanya kazi yoyote na1983 ilifutwa rasmi.Mali iliyobaki iligawanywa kati ya nchi zote tatu.
Kufufuka kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki tangu 1993
Tangumiaka ya 1990 majaribio ya kujenga umoja mpya yalionekana tena.
Kuna majadiliano ya kuanzishashilingi mpya ya pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kwanza ilitarajiwa kuanzishwa mwaka2012, halafu mwaka2015, sasa mwaka2024. Mwaka2013 ulisainiwamkataba wa kuamua kuanzisha hiyopesa ndani ya miaka 10.[7]
Uchumi
Pato la taifa
Jumuiya ya Afrika Mashariki inauchumiunaoendelea ikiwa naPato la taifa jumla dola bilioni 399 zaMarekani kwa Kawaida na trilion 1.197 kwaUsawa wa nguvu ya ununuzi (PPP) hata hivyo ni uchumiwa pili kwa ukubwa baraniAfrika baada yaAfrika Kusini.Kenya ndiyo iliyo na uchumi mkubwa zaidi katika jumuiya hii, ikichangia asilimia 37% ya jumla,Tanzania,Kongo, JK zilichangia asilimia 24% na 22% mtawaliwa.Sudan kusini naBurundi ndizo zilizokuwa na uchumi mdogo zaidi. Jumuiya ya Afrika Mashariki ni ya kipato cha chini ikiwa na pato la taifa kwa kila mtu dola 1,197 .Sudan Kusini ndiyo nchi maskini zaidi ikiwa na pato la taifa kwa kila mtu dola 252 zaMarekani,Kenya ndiyo nchi iliyo na pato la taifa kwa kila mtu dola kubwa zaidi ya dola 2,468 za Marekani.
Pato la taifa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (2025)
Mnamo 2023, jumla yabiashara ya kimataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilifikia dola bilioni 130.4. Mchango mkubwa zaidi ulitokaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (JKK), ambayo ilichangia asilimia 25.8 ya jumla hiyo, ikifuatiwa naKenya (24.7%) naTanzania (24.6%). Kwa upande mwingine, nchi zilizo na mchango mdogo zaidi zilikuwaSudan Kusini (1.8%) naBurundi (0.7%). Kwa Mahuruji (mauzo ya nje)Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliongoza zaidi ikichangia asilimia 40% ya mauzo ya nje ya Jumuiya hii, HukuKenya ikiongoza kwaMaduhuli ikichangia asilimia 30% ya Maduhuli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kati ya nchi zote, Kongo,JK ilikuwa na mizani chanya ya biashara (balance of trade) ya dola bilioni 7.8, ikiwa ya juu zaidi katika kanda, hukuKenya (-16.24),Tanzania (-9.90), na Somalia (-4.22) zikiripoti nakisi kubwa zaidi yabiashara, ishara ya uagizaji mkubwa wa bidhaa kuliko mauzo ya nje.
Kutokakushoto: RaisYoweri Museveni waUganda, RaisMwai Kibaki waKenya na RaisJakaya Kikwete waTanzania wakati wa mkutano waoArusha, mnamo Novemba2006.Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka wa 2006. Rwanda ilijiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki tarehe 1 Julai 2007
Kenya, Tanzania na Uganda zinahistoria yaushirikiano tangu mwanzoni mwakarne ya 20, wakati waukoloni, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Forodha baina ya Kenya na Uganda mwaka 1917,Tanganyika ilijiunga mnamo mwaka1927, katikaUbalozi wa Afrika Mashariki (1948-1961), 'East African Common Services Organisation' (1961-1967) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (1967-1977).[10]
Jumuia ambayo ilianzishwa baada yauhuru ilidumu miaka 10 tu, lakini ilifufuliwa kwa mkataba wa tarehe30 Novemba1999, ulioanza kufanya kazi tarehe7 Julai2000, miaka 23 baada yakifo cha ile ya kwanza.
Mara baada ya kupatauhuru mwaka2011, Sudan Kusini iliomba kujiunga na Jumuia, lakini haikukubalika hadi Machi 2016 kutokana na hali yavita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hatua kubwa ya awali katika kuanzishaShirikisho la Afrika Mashariki nimuungano wa forodha katikamataifa husika uliotiwasaini mnamo Machi 2004 na ulioanza kutumika tarehe1 Januari mwaka2005. Chini ya masharti ya mkataba, Kenya, ambayo ndiyo nchi inayopata mauzo bora zaidi nje ya nchi katika kanda ya Afrika Mashariki, iliendelea kulipaushuru kwabidhaa zake zinazoingia nchi nyingine wanachama hadi mwaka2010, kwakiwango kilichopungua na wakati.Mfumo sawa waushuru utatumika kwa bidhaa kutoka nchi ambazo si wanachama.
Changamoto
Kwa ujumla, mataifa wanachama kwa kiasi kikubwa wanaona neema yaShirikisho la Afrika Mashariki, lakini utafiti usio rasmi unaonyesha kwamba Watanzania wengi (asilimia themanini ya wakazi wake) wanamtazamo hasi.[13]
Pia ni kwamba Tanzania inaardhi kubwa, na baadhi ya Watanzania wanahofu yaunyakuzi wa ardhi na wakazi wa sasa wa mataifa mengine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.[14][15][16]
Uhaba wa ardhi ni suala nyeti katika eneo la Afrika Mashariki, hasa nchini Kenya, ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe upande waMlima Elgon mwaka2007 yaliwaacha zaidi ya watu 150 wamefariki na kulazimisha takriban watu wengine 60,000 kugura makazi yao.[17]
Bunge la Afrika Mashariki ndichokitengo cha kutengeneza sheria katika eneo la Afrika Mashariki. Ina wajumbe 27 ambao wote wamechaguliwa na mabunge ya nchi wanachama. Linahusika na masuala yote ambayo yanahusu Jumuiya hii kama vile kujadilibajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na masuala yote ya Jumuiya na kutoa mapendekezo kwa Baraza juu ya mambo wanayoyadhani muhimu kwa utekelezaji wa mkataba, kushirikiana pamoja na Bunge husika na kuanzishakamati kwa makusudi kama vile wanavyodhani ni muhimu. Tanguuzinduzi wake mwaka 2001,bodi hii imekuwa na vikao kadhaa mjini Arusha,Kampala na Nairobi.
Viungo
Pasipoti ya Afrika Mashariki
Pasipoti ya Afrika Mashariki ilizinduliwa rasmi tarehe1 Aprili1999 ili kurahisishausafiri na kuvuka mipaka ya nchi husika.[18][19] Nihalali kwa kusafiri ndani ya eneo la Afrika Mashariki (Kenya,Uganda na Tanzania) na kutoahaki ya kuingia na kukaa kwa miezi sita katika nchi yoyote na kisha unaweza ukaitumia tena.[18] Pasipoti hii inapatikana katika Makao Makuu yaIdara ya Uhamiaji katika miji ya Nairobi, Kampala na Dar es Salaam. Niraia tu wa Afrika Mashariki wanaoweza kuomba pasipoti hii.[18][19]Gharama ya pasipoti hii ni dola 10 zaMarekani au pesa sawa ukibadilisha kwa sarafu za nchi za Afrika mashariki.[19] Baada ya kujaza fomu za kupata pasipoti hii itachukua muda wawiki mbili au tatu kuipata tayari kwa matumizi. Ingawa pasipoti hii ni halali tu ndani ya Afrika Mashariki, majadiliano yalifanywa ili kuwa na hati sawa za kusafiri kwa watu wote wa Afrika Mashariki.[18]
Lilikuwatarajio la wengi kuwa kabla ya 2006 kungekuwa na viza moja kwa watalii wote wanaozuru Afrika Mashariki, iwapo mpango huo ungeidhinishwa na mamlaka yasekta husika chini ya jumuiya hiyo. Iwapo ingekubalika basi viza hiy ingetumika kote katika ardhi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Chini ya pendekezo hili viza yoyote mpya ya Afrika Mashariki ingeweza kupokewa kutokaubalozi wowote katika eneo la Afrika Mashariki.
Mtandao
Matumizi yawavuti katika eneo la Afrika Mashariki bado yako chini mno yakilinganishwa na mataifa yaliyostawi kiuchumi.
Eneo la Afrika Mashariki ni kituo kizuri kiuchumi huku likikadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni 150. Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya wakazi wa Afrika Mashariki - milioni 15 - huutumiaMtandao.
Hivi karibuni kumekuwa na majukwaa mengi yanayoibuka katika eneo hili kwa lengo la kuileta pamoja Afrika Mashariki.
Kasi ya mawasiliano kupitia kwa mtandao pia iko chini mno katika eneo la Afrika Mashariki, ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi. Hii labda ni mojawapo ya vikwazo vya maendeleo ya mawasiliano ya mtandao Afrika Mashariki.
Jiografia
Mtangamano ungekuwa nchi moja tu, ungekuwa ya 7duniani kwa eneo (kilometa mraba 4,812,618).
↑"EAC Update E-newsletter".www.eac.int. Directorate of Corporate Communications and Public Affairs. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2012-04-26. Iliwekwa mnamo10 Desemba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)