Kuna nchi zilizobadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku zaJumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia.
Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali
Katika lugha yaKiswahili jina la siku lina namba "5" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira yaUyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu yaIjumaa siku ya sala ya pamoja:Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa,Jumapili kama siku ya pili,Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababuKiarabu ambacho ni lugha yaKorani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita أربعاءarba'a (ya nne).
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya nne", kwa mfanoKiindonesia (Rabu - ya nne) auKiajemi (Farsi) (چهارشنبه -tchahor shanbe - siku ya nne).
Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Mercredi" (siku yaMercurius) au Kiingereza "Wednesday" (siku yaWodan).
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuJumatano kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.