Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Jumamosi kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu maarufu yaPietà yaMichelangelo iliyochongwa katikamarumaru kumuonyeshaBikira Maria akipakatamaiti ya mwanaeYesu mara baada yakifo chakemsalabani.
Picha takatifu ya Jumamosi Kuu na Takatifu, ikimuonyeshaYesuKushukia kuzimu.

Jumamosi kuu nisiku yaJuma kuu inayoadhimisha hasapumziko lamwili waYesu Kristokaburini naroho yake kushukiakuzimu kabla yakufufuka kwautukufuusiku wa kuamkiaJumapili yaPasaka.

Tarehe yake inabadilikabadilika kilamwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katikamadhehebu yaUkristo, hasa yanayofuatamapokeo yamashariki na yale yanayofuata mapokeo yamagharibi.

Siku hiyoMisa nasakramenti mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwawafuasi waYesu wanatuliakimya wakitafakari matukio yaIjumaa kuu na kujiandaa washangilieufufuko wake kuanziakesha la Pasaka hadiJumapili yaPentekoste siku50 baadaye.

Majina katika lugha mbalimbali

[hariri |hariri chanzo]

Jumamosi kuu inaitwa kwa namna tofauti katikalugha mbalimbali. Baadhi ya mifano ni kama ifuatavyo:

LughaJinaTafsiri
KichekiBílá sobotaJumamosi nyeupe
KifaransaSamedi saintJumamosi takatifu
KihispaniaSábado SantoJumamosi takatifu
KiholanziStille ZaterdagJumamosi ya kimya
KihungariaNagyszombatJumamosi kuu
KiingerezaHoly SaturdayJumamosi takatifu
KiitaliaSabato SantoJumamosi takatifu
Kijapani聖土曜日 (Sei Doyoobi)Jumamosi takatifu
KijerumaniKarsamstagJumamosi ya ombolezo
KipolandiWielka SobotaJumamosi kuu
KislovakiaBiela sobotaJumamosi nyeupe

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuJumamosi kuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Jumamosi_kuu&oldid=1326920"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp