Kipenyo cha Jua ni takribankilomita 1,392,684 ambayo ni mara 109 ya kipenyo cha Dunia yetu.Masi yake ni mara 330,000 ya masi ya Dunia. Kwa ujazo Jua ni kubwa mara milioni moja kuliko Dunia.
Kikemia masi ya Jua ni hasahidrojeni (73%) naheli (25%). Kiasi kinachobaki nielementi nzito zaidi, kama vileoksijeni,kaboni,chuma nanyingine. Ingawa elementi nzito niasilimia ndogo tu za masi ya Jua, kutokana na ukubwa wa Jua, elementi nzito zinalingana mara 5,000 na masi ya Dunia
Muundo wa Jua
Muundo wa Jua
Muundo wa Jua hufanywa na kanda tatu:
Kiini ambako atomi za hidrojeni zinayeyungana kutengeneza heli kutokana na hali ya shinikizo na joto kubwa mno;
Ukanda wa myuko (convection zone) ambako joto la kiini linaendesha mizunguko ya utegili inayopeleka nishati kutokana kiini kwenda angahewa ya Jua
Ukanda wa angahewa ya Jua. Sehemu yake kubwa inaitwa tabakanuru (photosphere). Tabakanuru ni asili ya nuru na joto tunazopokea duniani. Sehemu ya nje ya angahewa ni "korona" inayoonekana tu wakati wa kupatwa kwa Jua.
Historia ya Jua
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Jua lilitokea takriban miakabilioni 4.57 iliyopita katikawingu kubwa lamolekuli za hidrojeni.
Kama nyota zote Jua linapitia ngazi mbalimbali katikamaisha yake.Wataalamu wengi hukadiria kwamba baada ya miaka bilioni 5 ijayoakiba ya hidrojeni katika kitovu cha Jua itapungua. Halafu Jua litapanuka sana na kuwajitu jekundu[1]. Katika hali hii inaweza kuenea hadi njia yaobiti yaZuhura na hakuna nafasi tena kwauhai kwenye Dunia kutokana na joto kali.
Wataalamu wanatofautiana katika makadirio yao kama upanuzi huu utasababisha pia kupotea kabisa kwa sayari zaUtaridi,Mirihi naDunia zikimezwa na kuingia ndani ya Jua.[2]
Baada ya miaka bilioni kadhaa ya kuwaka kama jitu jekundu, masi yake itakuwa imepungua itajikaza na kuendelea kwamuda usio mrefu kama nyota ndogo na hafifu. Kuna uwezekano mkubwa wa kwamba Jua litaendelea baadaye kamanyota kibete nyeupe (White Dwarf) itakayoendelea kuzimika polepole[3].
Mnururisho na upepo wa Jua
Jua linatoamwanga,joto namnururisho mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la chembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kamaupepo wa Jua. Masi ya upepo wa Jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde.[4]Asili yanishati hii ni mchakato wamyeyungano wa kinyuklia ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heliamu. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heliamu inaachisha nishati inayotoka kwenye Jua kwa njia ya mnururisho.
Dunia yetu ina mistari ya kubuni inayowezesha kutambua maeneo mbalimbali kwa urahisi,mistari hiyo ni pamoja na mstari waIkweta,tropiki ya kansa natropiki ya KaprikoniMstari waIkweta unaigawa dunia katika sehemu nbili zakaskazini nakusini,mstari huu una nyuzi 0 na unapita eneo la Afrika mashariki katika nchi zaKenya naUganda.Mstari wa Tropiki ya kansa upo upande wa kaskazini mwa Ikweta.Mstari wa tropiki ya Kaprikoni Upo Kusini mwa Ikweta.Kipindi ambacho jua la Utosi lipo Tropiki ya kansa ,eneo La Kizio cha Kaskazini Huwa najoto,kwa kuwa hewa ikipata joto hutanuka hivyo huwa na mgandamizo mdogo wa hewa.Pepo huvuma kuelekea huko.
Upepo
Pepo hizi huvuma kutoka kusini-mashariki kuanzia mwezidesemba wakati jua la utosi linapokuwa tropiki ya kaprikoni kipindi hiki kizio cha kusini huwa na joto na Pepo huvuma kutoka kusini-mashariki.Pia hali hiyo husababisha mabadiliko ya upatikanaji wa mvua na hali ya joto katika eneo la Afrika Mashariki.Maeneo ya Ikweta yana tabia ya Kiikweta ya kuwa namvua nyingi najoto jingi.Kusini na Kaskazini mwa eneo lenye tabia ya Kiikweta kuna tabia ya kitropiki yenye majira mawili makuu ya mwaka.Majira hayo ya mwaka nimasika nakiangazi.Lakini katika maeneo ya pwani majira ya mwaka hugawanyika katika sehemu nne ambazo nivuli,kipupwe,masika nakiangazi.
Mwinuko
Afrika Mashariki ina mwinuko wa meta 0 kutoka usawa wa bahari hadi kufika meta 4600.Maeneo ya pwani mwinuko wake ni kuanzia meta 0 hadi meta 500 kutoka usawa wa bahari.Wastani wa jotoridi ni nyuzi za sentigredi 26.Joto hupungua kadiri unavyoelekea bara.Meta 1500 Kutoka usawa wa bahari ni nyuzi za sentigredi 22 ambapo ni wastani wa joto linalopatikana katika maeneo yaTabora.Maeneo ya mlima mrefu kamakilimanjaro wenye urefu wa meta 5895 huwa na jotoridi la chini ya nyuzi za sentigredi 0
Maziwa na bahari
Maeneo yaliyo kandokando yamaziwa nabahari huwa na unyevunyevu na mvua nyingi.Mara nyingi maeneo yanayozunguka bahari na maziwa mfanoZiwa Viktoria naBahari ya Hindi yana tabia ya nchi ya aina moja.Maeneo hayo kwa kawaida hupata mvua nyingi.
Uoto wa misitu
Maeneo yenyemisitu hupata mvua nyingi kwanimawingu huweza kufanyika kwa urahisi.Misitu hiyo pia huifadhi unyevu usipotee ardhini kwa urahisi kwa njia ya mvukizo.
Pepo
Pepo za msimu zaKaskazini-mashariki Huleta Mvua kidogo katika eneo kubwa lakenya na kaskazini mwaTanzania. Pepo huvuma sambamba na pwani.Pepo hizi pia huvuma kutoka sehemu kubwa ya nchi kavu katika nchi yaEthiopia naSudani kabla ya kufika eneo laAfrika Mashariki.
Angalia mengine kuhusuSun kwenye miradi mingine yaWikimedia:
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuJua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.