Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Joseph Kony

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Joseph Kony (alizaliwa mwaka1961 hivi) ni kiongozi wa kundi la wanamgambo waLord's Resistance Army (LRA), ambalo limejihusisha na kampeni za ghasia likiwa na azma ya kuanzisha serikali inyoongozwa na viongozi wadini nchiniUganda, kundi hili liandai limejengeka kwenye misingi yaBiblia ya Kikristo naamri kumi. Kundi la LRA ambalo lilijulikana kwa vitendo vyake dhidi ya wenyeji wa Uganda Kaskazini, limeteka nyara takribani watoto 30,000 na kusababisha watu milioni 1.6 kukimbia makazi yao tangu uasi wao ulipoanza mwaka 1986.[1][2][3]

Wasifu

Joseph Kony alizaliwa mwaka 1961 katika kijiji chaOdek, kinachopatikana mashariki mwaGulu kaskazini mwaUganda, wazazi wake walikuwa wakulima. Aliwapenda wadogo zake lakini walipomkosea aliwaadhibu.[4] Katika ujana wake, Joseph Kony alifunzwa kuwa mganga wa kijiji na kaka yake, Benon Okello, na huyo alipoaga alichukua kikamilifu wajibu wa kuwa mganga wa kijiji.[5] Alipokosewa alipendela kupigana badala ya maelewano kwa njia ya mazungumzo. Akiwa shuleni alitaniwa kwa ukubwa wake na walimu walimpa wakati mgumu kwa sababu hakuonekana muerevu sana. Baba yake alikuwa mteandakazi wa mungu katikaKanisa Katoliki na mama yake alikuwa Mwanglikana, Kony alikuwa alatare kwa miaka kadhaa. Aliacha kwenda kanisani akiwa na umri wa karibu miaka 15.[4] Aliacha masomo yake shule ya upili na alipata umaarufu mwezi wa Januari mwaka 1986, akiwa na miaka ishirini na kitu hivi. Kundi lake lilikuwa moja ya makundi makubwa yaliyoibukahuko Acholi wakati wa vuguvugu maarufu laRoho Mtakatifu lililoongozwa naAlice Auma (aka Lakwena). Hata hivyo kulikuwa na mgogoro miongoni mwa Wacholi walionung'unikia kupoteza uashawishi wao baada ya RaisTito Okello aliyekuwa Muacholikupinduliwa naYoweri Museveni na jeshi lake la NationalResistance Army (NRA) wakati waVita vya msituni vya Uganda vilivyoisha mwaka 1986.

Mwanzoni, kundi la Kony's liliitwa United Holy Salvation Army (UHSA) na halikuchukiliwa kama tisho na NRA. Kufikia mwaka 1988, baada ya mkataba kati ya NRA naUganda People's Democratic Army kuongeza makundi yake mengine ya wapiganaji pamoja na kusajili watoto kwa nguvu kulilifanya kundi la United Holy Salvation Army kuwa jeshi lililoogofya. Askarijeshi wake wengi walikuwa watoto. Inakadiriwa kuwa amechukuwa watoto zaidi ya 104.000 wavulana na wasichana tangu LRA ilipoanza kupigana mwaka 1986. MMara nyingi aliua jamaa na majirani wa watoto hawa alipokuwa akiwateka na kuwalazimisha wapigane katika jeshi lake. Kamanda wa kundi lilosalia la UPDA alikuwaOdong Latek, ambaye alifanikiwa katika kumshawishi Kony atumie mbinu za kisasa za kijeshi kinyume na majaribio ya awali ambayo yalihusu mashambulizi ya mslaba na kutumia maji matakatifu. Mbinu hii mpya ilifanikiwa na UHSA mapigano madgomadogo lakini waliweza kuwashinda NRA. Baada ya ushindi huu NRA ililipiza kizazi kwa kudhoofisha kundi la Kony kisiasa na kampeni iliyoitwa Oparation North.

Kufikia mwaka 1992 alilipa hilo kundi jiypa la Muungano wa Jeshi la Kikristo la Demokrasia na ni katika wakati huu ndiyo waliowateka nyara wasichana 44 kutoka shule za upili za Sacred Heart Secondary na St. Mary's Girls School Operation North iliharibu kabisa kile kingekuwa wanamugambo wa Lord's Resistance Army,hata hivyo, ingawa idadi yao ilipungua kutoka maelfu hadi mamia waliendelea kuwavamia raia na washirika wa NRA.

Mazungumzo ya Bigombe ya mwaka 1993 yalifunua mengi kumhusu Joseph Kony.Betty Bigombe alikumbuka kwamba mara ya kwanza alikutana na Kony na wafuasi wake walitumia mafuta kujikinga na risasi na pepo mbaya.[6] Katika barua ilyohusu mazungumzo ya baadaye Kony pia alieleza kwamba sharti angetafuuta ushauri kutoka kwaRoho Mtakatifu. Mazungumzo yalipoanza walisisitiza kwamba viongozi wa dini washirikishwe na walifungua mkutano kwa maombi yaliongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Dini wa LRA Bw. Jenaro Bongoni. Hatimaye katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1994 Kony aliingia huku wanaume waliovaa majoho wakiwa mbele yake wakimyumyiziamaji takatifu.[7]

Juhudi nyingi za kimataifa za kuleta amani na kukomesha utekaji nyara wa watoto na Kony na Wanamugambo wa kundi lake la Lord's Resistance Army zilifanyika kati ya 1996 na 2001. Juhudi zote zilishindwa kumaliza utekaji nyara wa watoto, ubakaji, askari-jeshi watoto mauji ya raia ikiwemo usambuliaji wa kambi za wakimbizi. Baada yashambulizi latarehe 11 Septemba Marekani ilitangaza rasmi wanamgambo wa Lord's Resistance Army kuwa kundi la kigaidi na Joseph Kony kuwa gaidi.[8]

Josph Kony alifikiriwa kuwa mtu mwenye pepo; amesawiriwa kama ama kma Masihi au shetani. Alizuru mara kadhaa milima ya Ato nchini Uganmda. Inadaiwa kuwa angekwea hadi kileleni cha milima na kulala huko kwenye jua kali kwa siku kadhaa. Angefunikwa na kundi la kumbikumbi wekundu ambao waliing'ata ngozi yake kwa undani. Mafuta kutoka mti uitwao Yao ilipakwa mwilini mwake. Kisha aliingia kwenye pango na kushinda huko pekee kwa majuma kadhaa. Alichowaamuru watoto wafanye kilikuwa kitu cha upuzi- aliwaambia kuwa iwapo wangechora mslaba kwenye vifua vyao na mafuta wangekingwa kutoka kutoka kwa risasi.[4] Kony anasisitiza kwamba wanamugambo waLord's Resistance Army wanapigania Amri Kumi."Ndiyo, tunapigania Amri Kumi," Je, ni vibbaya? siyo kukiuka haki za binadamu. Na amri haikutolewa na Joseph. Haikutolewa na LRA. la, amri hiyo ilitolewa na Mungu. "[9]

Mashtaka rasmi

Lord's Resistance Army
insurgency
Events

1987–1994
1994–2002
2002–2005
Juba talks
2008–

Related articles

Lord's Resistance Army
Holy Spirit Movement
Alice Auma
Joseph Kony
ICC investigation


Tarehe 6 Oktoba 2005 Mahaka ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa vibali vya kukamtwa kwa wanamugambo watano wa kundi la Lord's Resistance Amy kwa uhalifu dhidi ya haki za binadamu kufuatia kufunguliwa mashitaka. Siku iliyofuata waziri wa ulinzi waUganda Amama Mbabazi alidokeza kuwa Joseph Kony, naibu wake Vincent Otti na makamanda wa Raska Lukwiya, Okot Odiambo na Dominic Ongwen walikuwa miongoni mwa wale ambao vibali vyao vya kukamtwa vilitolewa. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, jeshi la Uganda lilimua Lukwiya tarehe 12 Agosti 2006.[10]

Juma moja baadaye, tarehe 13 Oktoba, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICCLuis Moreno Ocampo alitoa maelezo kuhusu mashitaka yaliyomkabili Kony. Kuna jumla ya mashtaka 33, 12 yakiwa ni uhalifu dhidi ya haki za binadamu, ambayo ni pamoja na mauaji, utumwa, utumwa wa ngono na ubakaji. Kuna mashitaka mengine 21 ya uhalifu wa kivita ambayo ni pamoja na mauaji, ukatili kwa raia, ushambulizi wa kimakusudi kwa raia, uporaji mali, ubakaji na kusajili watoto kwa nguvu katika vikosi vya waasi. Ocampo alisema kwamba "Kony aliwateka wasichana kuwatoa kama zawadi kwa makamanda wake."

Jeshi la Uganda limejaribu kumua Kony kwa shutuma za Upinzani .

Tarehe 31 Julai 2006, Kony alikutana na viongozi kadhaa kitamaduni, kisiasa, na viongozi wa dini kutoka Kaskazini mwaUganda mafichoni mwake katika msitu wa kondo kuzungumzia vita. Siku iliyofuata,1 Agosti, alivuka mpaka na kuingia Sudan kuzungumza na Makamu wa Rais wa Kusini mwa Sudan Riek Machar. Baadaye Kony aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa tayari kufika mbele ya mahakama ya ICC kujibu mashitaka kwa kuwa hajafanya lolote baya.

Tarehe 12 Novemba 2006 Kony alikutana naJan Egeland, Umoja naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura. Kony aliambia shirika la habari laReuters: "Hatuna watoto wowote. tunawapiganaji tu.[11]

Tarehe 28 Agosti mwaka 2008, wizara ya fedha ya Marekani ilimuorodhesha Kony miongoni mwa kundi la "magaidi wa kipekee duniani" kundi ambalo huwa na adhabu za kifedha na adhabu. Haijulikani iwapo Kony ana miliki au hamilki rasilimali yoyote amabyo inaathiriwa na maelezo yaliyotolewa.

25 Desemba 2008, kwa mujibu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, waasi waLord's Resistance Army (LRA) waliwaua watu 189 na kuteka nyara watoto 120 wakati wa sherehe iliyofadhiliwa na Kanisa Katoliki huko Faradje, katikaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Desemba 2008, jeshi la Kongo, pamoja na vikosi vya jeshi laUganda naSudan, vilivamia waasi wa LRA wakiwa na lengo la kuwanyang'anya silaha waasi wa LRA.

Tanbihi

  1. Flight of the child Soldiers
  2. BBC News - Mjube wa Umoja wa mataifa akutana na kiongozi wa waasi
  3. Buteera, Richard. The Reach Of Terrorists Financing And Combating It-The Links Between Terrorism And ordinary Crime. International Society of Prosecutors. Washington, DC. 12 Agosti 2003.[1]Ilihifadhiwa 27 Aprili 2007 kwenyeWayback Machine.
  4. 4.04.14.2 Jimmie Briggs "Innocents Lost: When Child Soldiers Go to war" 2005 s. 105-144
  5. Petro Eichstaedt,First Kill Your Family: Child Soldiers of Uganda and the Lord's Resistance Army, s. 206
  6. The Woman Behind Uganda's Peace Hopes- Betty Bigombe Put life on Hold to Interced in Northern War[2]
  7. BBC - Profile: Ugandan rebel Joseph Kony
  8. Philip T. Reeker (6 Desemba 2001). [https://web.archive.org/web/20020202195601/http://www.state.gov/r/pa/prs/ps/2001/6695.htm "Statement on the Designation of 39 Organizations on the USA PATRIOT Act's �Terrorist Exclusion List�"]. U.S. Department of State. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2002-02-02. Iliwekwa mnamo2009-12-12.{{cite web}}:replacement character in|title= at position 75 (help)
  9. "I wil use the Ten Commandments to liberate Uganda". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2007-11-17. Iliwekwa mnamo2009-12-12.
  10. "Ugandan army kills senior rebel'."BBC News. 13 Agosti 2006. 15 Februari 2007.[3]
  11. Kony told Reuters: "Hatuna watoto wowote tunawapiganaji pekee.[4]

Marejeo

Viungo vya nje

Legal texts
International
UN resolutions
General Assembly
Security Council
1422 ·1487 ·1593 ·1970
National
The seal of the International Criminal Court
Crimes
Organisation
States Parties
Court
Investigations
Official
Complaints
Individuals
Other
Persondata
NAME
ALTERNATIVE NAMES
SHORT DESCRIPTION
DATE OF BIRTH
PLACE OF BIRTH
DATE OF DEATH
PLACE OF DEATH
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Joseph_Kony&oldid=1378061"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp