Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Joseph Kabila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph Kabila.

Joseph Kabila Kabange (alizaliwa4 Juni1971) alikuwarais wanne waJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aliingiaurais baada yakifo chababa yake RaisLaurent-Desiree Kabila aliyeuawa nawanajeshitarehe16 Januari2001.Wanasiasa wengine walimteuamwana kuwa rais badala ya baba.

Katikauchaguzi wa kitaifa wa tarehe30 Julai2006 alipatakura nyingi kuliko wagombea wote kuwa rais lakini hakufikianusu ya kura zote. Katika uchaguzi wa pili kati yake naJean-Pierre Bemba alishinda akathibitishwa kuwa rais tarehe17 Novemba2006. Joseph Kabila ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyechaguliwa na wananchi wote katika uchaguzi huru.

Maisha yake

[hariri |hariri chanzo]

Joseph Kabila alizaliwa mjiniHewa Bora katikamkoa waKivu Kusini,mashariki mwa Kongo. Baba yake alikuwa mwanasiasa nakiongozi wa kikundi chawanamgambo waasi waliopingaserikali yaMobutu Sese Seko.

Pamoja nafamilia ya baba Joseph alihamiaDar es Salaam (Tanzania. Alisomashule ya msingi na yasekondari huko Dar es Salaam na shule ya sekondariSangu secondary (Mbeya). Anasemekana wakati ule alitumiajina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu zausalama.

Mwaka1996 alijiunga na wanamgambo wa baba yake katikavita vya Kongo ya Mashariki.

Baada yaushindi wa wapinzani dhidi ya Mobutu, baba alikuwa rais na Joseph alipelekwa masomoni kwenyechuo cha kijeshi hukoUchina. Wakati wa kurudi alipewacheo chajenerali jeshini na mwaka2000 alipandishwa cheo kuwamkuu wa jeshi.

Tangu kuwa rais mwaka 2001 Joseph Kabila alijitahidi kumaliza hali yavita vya wenyewe kwa wenyewe Kongo akakubali kufika kwawalinzi wa amani waUM.

MnamoDesemba2002 alikubali mapatano yaamani kati ya serikali na waasi yaliyokuwa msingi wa kuundwa kwaserikali ya umoja wa kitaifa na maandalizi ya uchaguzi wa mwaka2006.

KatikaJuni 2006 alimwoaOlive Lembe di Sita aliyekuwamchumba wake wa miaka mingi namama wabinti aliyezaliwa mwaka 2001.

Mnamo Oktoba2021, Joseph Kabila aliteteatasnifu yake ya kuhitimu katikaChuo Kikuu cha Johannesburg. Shahada yauzamili katikasayansi ya siasa na uhusiano wa kimataifa alitunukiwa mwishoni mwa masomo yake ambayo yalidumu kwa miaka mitano.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuJoseph Kabila kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Joseph_Kabila&oldid=1198866"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp