Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Joseph Haydn

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph Haydn mwaka 1791

Joseph Haydn (jina kamiliFranz Joseph Haydn) alikuwamtungaji wamuziki kutoka nchi yaAustria. Alizaliwa tarehe31 Machi au1 Aprili1732 katikakijiji kikubwa chaRohrau, jimbo laAustria Chini. Aliagadunia tarehe31 Mei1809 mjiniVienna.

Amekuwa maarufu kwa jina la heshima la "baba wasimfoni".Wajerumani na Waaustria hasa wanamkumbuka kama mtungaji wa muziki wawimbo uliokuwawimbo wa taifa katikaMilki ya Austria na baadaye kuwa wimbo wa taifa nchiniUjerumani hadi leo (wimbo wa Wajerumani).

Maisha

[hariri |hariri chanzo]

Mvulana wa kwaya na mwanamuziki wa kujitegemea

[hariri |hariri chanzo]
Kanisa kuu la Mt. Stefano hukoVienna.

Alipokuwamtoto wa miaka 8 alialikwa kwenda Vienna na kuwamwimbaji wakwaya yawavulana kwenyekanisa kuu lamji huo. Katika miaka yake kamamwanakwaya alipokea mafundisho yauimbaji,piano nafidla. Aliongozwa pia katika majaribio ya kwanza ya kutunga muziki.

Baada ya kubalehe na kubadilika kwasauti yake aliondoka katika kwaya hiyo mnamo1749 na kuanza kujitegemea kamamwanamuziki. Hakuwa naajira ya kudumu bali alipatakazi kama mwimbaji au mwanamuziki kwa nafasi mbalimbali.Makazi nachakula alijipatia kamamwalimu wa muziki katikanyumba yatajiri mmoja alipofundisha kila siku kwa masaa machache. Wakati huo alifaidika sana na maelekezo yaNicola Porpora, mwanamuzikimzee kutokaNapoli,Italia.

Mkurugenzi wa muziki kwenye ikulu ya Esterhazy

[hariri |hariri chanzo]

Kuanzia mwaka1761 Haydn alipata ajira kwenyeikulu yafamilia Esterhazy waliokuwa kati ya makabaila matajiri zaidi nchiniHungaria iliyokuwa sehemu ya milki ya Austria. Alianza kamamakamu wamkurugenzi wa muziki na tangu1766 kama mkurugenzi wa muziki wa akina Esterhazy. Hapo alihamia pamoja na familia yamwajiri wake baina ya ikulu tatu walipoishi kulingana namajira ya mwaka.

Aliwajibika kuongozaokestra, kuandaatafrija, kutunga muziki kwa nafasi maalum, kupiga muziki wakati wa chakula aujioni kwaburudani ya bwana wake.

Kutokana na maisha ya kuhamahama baina ya ikulu za familia hiyo aliishi muda mrefu mashambani. Aliandika mwenyewe kuhusu maisha haya yaliyokuwa mbali na wanamuziki wengine: "Nilitengwa na dunia, bila mtu aliyeweza kunishawishi au kunivuruga na kwa hiyo nilipaswa kuwa mimi mwenyewe".

Mtungamuziki

[hariri |hariri chanzo]

Katika kipindi cha karibu miaka 30 alipokuwa mkurugenzi wa muziki kwa Esterhazy, Haydn alitunga miziki mingi iliyochapishwa na kusambazwa. Kazi zake zilianza kuwa maarufu ilhali wengine walipiga muziki aliotunga yeye mahali pengine.

Aliombwa pia kutokang'ambo kutunga muziki kama vileSimfonia za Paris (17851786) na muziki kwaibada yaIjumaa Kuu "Maneno saba ya mwisho yamwokozi wetumsalabani" (1786) iliyoagizwa kutokaHispania.

Urafiki na Mozart

[hariri |hariri chanzo]

Tangu 1781 Haydn na Mozart walikuwa marafiki. Mozart aliyekuwakijana wake aliwahi kupenda muziki ya Haydn tangu miaka kadhaa. Hao watungaji wawili walipenda kupiga fidla pamoja na kushauriana juu ya kazi yao.

Ziara za Uingereza

[hariri |hariri chanzo]

Tangu1790mtemi Esterhazy aliaga dunia namrithi wake hakujali muziki, hivyo aliachisha wanamuziki wote.

Haydn alitumiauhuru wake mpya akifuatamwaliko wa mtoaji wa muziki MjerumaniJohann Peter Salomon kwendaUingereza na kuendesha simfonia zake kwa okestra kubwa. Maonyesho yake yalileta mafanikio makubwa: watu wengi walitaka kumsikia akawa tajiri.

Mara mbili Haydn alisafiri hadi Uingereza (17911792 na17941795) akafanikiwa kila mara. Alitumia miezi yake huko kwa kutunga idadi ya kazi zake zilizokuwa mashuhuri hasa baadaye kama vile "Simfonia na pigo la ngoma", "simfonia yajeshi" na "simfonia za London".

Kwa muda alitafakari kubaki Uingereza na kuombauraia wa kule lakini hatimaye alirudi Vienna.

Uzee

[hariri |hariri chanzo]

Aliporudi Vienna 1795 kulikuwa tena na mabadiliko katika nyumba ya Esterhazy, na mtemi mpya alimwomba arudi kama mkurugenzi wa muziki kwenye ikulu zake. Haydn alikubali lakini kwa miezi kadhaa ya kilamwaka pekee. Hapo kwenye ikulu ya Eisenstadt aliandika muziki kwamisa 6 lakini sehemu kubwa ya mwaka alikaa katika nyumba yake huko Vienna alipoendelea kutunga muziki.

Pamoja namshairiGottfried van Swieten aliyeandika maneno kwauimbaji alitungaoratori kubwa mbili (yaani muziki inayosimulia habari za kidini na nyingine kwa kutumia mitindo inayofanana naopera), ambazo ni "Uumbaji" (1798) na "Majira ya mwaka" (1801). Akatunga pia muziki zaidi yakwateti (kwa wapigaji wanne).

Hapo alianza kusikiaumri umekwenda, akapaswa kupambana na magonjwa akajitahidi sana kukamilisha kazi zake. Tangu1802 alishindwa kutunga muziki tena.

Mwaka1808 alitoka tena katika nyumba kwa maonyesho ya oratori "Uumbaji" yaliyoendeshwa naBeethoven naSalieri kwa heshima yake. Alishindwa kukaa hadi mwisho kwa sababu alikosanguvu.

Aliaga dunia mwisho wa Mei 1809 wakati jeshi laNapoleon Bonaparte liliposhambulia Vienna. Kati ya maneno yake ya mwisho ni jaribio la kutuliza wafyanyakazi wa nyumbani waliokuwa nahofu wakisikiangurumo wa mizinga ya jeshi laWafaransa.

Haydn alizikwa makaburini na ibada ya kumbukumbu yake ilifanywa baada yauvamizi kwisha, tarehe15 Juni 1809.

Matukio baada ya kifo

[hariri |hariri chanzo]

Mwaka1820 familia ya Esterhazy ilimkumbuka mtumishi wake wa zamani wakamwandalia kaburi katika kanisa laEisenstadt alipowahi kufanya kazi miaka mingi. Wakati wa kuhamishamaiti yake,jeneza lilifunguliwa, kumbekichwa chake hakikuwepo.

Iligunduliwa kwamba wakati wa kumzika mara ya kwanzagavana wagereza la Vienna, Johann Peter, pamoja nakatibu wa zamani wa nyumba ya Esterhazy, Rosenbaum waliwahonga maafisa wamanispaa ya Vienna ili wafungue kaburi kwasiri siku nane baada yamazishi na kumpatia kichwa. Maana hawa watu wawili walikuwa wafuasi waimani kuwaumbo lafuvu linaonyeshatabia zamtu, hivi walikusanya mafuvu wakataka kuwa na fuvu la huyu mtu mashuhuri pia.

Wakati wa mazishi ya pili fuvu halikupatikana tena, hivyo Haydn alizikwa mara ya pili bila kichwa.

Peter na Rosenbaum waliamua kuficha fuvu wakafaulu hata wakatipolisi ilipopekua nyumba zao. Baadaye walimkabidhi mtemi Esterhazy fuvu tofauti lisilokuwa la kweli.

Kabla ya kufa Rosenbaum aliacha fuvu kwa Peter katikawasia wake, kwa ombi la kukipatia fuvu hilo chuo cha muziki Vienna. Lakini Peter namjane wa Rosenbaum waliogopa kuonyesha kuwa fuvu lilikuwa badomikononi mwao. Hivyo fuvu la Haydn lilifichwa hadi Peter kabla yakifo chake alilikabidhi kwa shirika la marafiki wa muziki wa Vienna lilipotunzwa kuanzia mwaka1895.

Katikamiaka ya 1930 mtemi wa Esterhazy alipamba upya kaburi la Haydn katika kanisa la Eisenstadt akatafutakibali cha shirika la marafiki wa muziki wa Vienna ili fuvu la Haydn lipelekwe huko. Baada yamajadiliano marefu walikubali, lakini sasasiasa navita viliingia kati, yaaniuvamizi wa Austria naAdolf Hitler mwaka1938 naVita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mwishoni fuvu lilipelekwa Eisenstadt mwaka1954 na kuunganishwa na mabaki mengine yamwili wa Haydin katika ibada ya kumkumbuka. Isipokuwa katika jeneza lake lilikuwepo fuvu lauongo lililopelekwa huko mwaka 1820 na fuvu hilo halikutolewa. Hivyo jeneza la Haydn lina mafuvu mawili.

Imani na maisha ya kiroho

[hariri |hariri chanzo]

Maisha yake yote Haydin alikuwaMkatoliki safi na ni imani yadini iliyomuongoza sana katika utunzi. Hata alipojisikia kukosaubunifu alikuwa akikimbiliasala. Maandishi yake mengi yanaishia na maneno yaKilatini, "Laus Deo", yaani, "Sifa kwaMungu".

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
Kuhusu maisha yake
  • Dies, Albert Christoph (1963). "Biographical Accounts of Joseph Haydn". Katika Gotwals, Vernon, translator and editor (mhr.).Haydn: Two Contemporary Portraits. Milwaukee: University of Wisconsin Press.ISBN 0-299-02791-0.{{cite book}}:|editor-first= has generic name (help);Invalid|ref=harv (help)CS1 maint: multiple names: editors list (link) A translation from the original German: "Biographische Nachrichten von Joseph Haydn nach mündlichen Erzählungen desselben entworfen und herausgegeben" ("Biographical accounts of Joseph Haydn, written and edited from his own spoken narratives") (1810). Camesinaische Buchhandlung, Vienna. One of the first biographies of Haydn, written on the basis of 30 interviews carried out during the composer's old age.
  • Finscher, Ludwig (2000).Joseph Haydn und seine Zeit. Laaber: Laaber-Verlag.ISBN 3-921518-94-6.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) Highly detailed discussion of life and work; in German.
  • Geiringer, Karl; Geiringer, Irene (1982).Haydn: A Creative Life in Music (tol. la 3rd). University of California.ISBN 0-520-04316-2. The first edition was published in 1946 with Karl Geiringer as the sole author.
  • Griesinger, Georg August (1963). "Biographical Notes Concerning Joseph Haydn". Katika Gotwals, Vernon, translator and editor (mhr.).Haydn: Two Contemporary Portraits. Milwaukee: University of Wisconsin Press.ISBN 0-299-02791-0.{{cite book}}:|editor-first= has generic name (help);Invalid|ref=harv (help)CS1 maint: multiple names: editors list (link) A translation from the original German: "Biographische Notizen über Joseph Haydn" (1810). Leipzig. Like Dies's, a biography produced from interviews with the elderly Haydn.
  • Hadden, James Cuthbert (2010).Haydn (tol. la Reissue). London: Cambridge University Press.ISBN 1-108-01987-0.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
  • Hughes, Rosemary (1970).Haydn (tol. la Revised). New York:Farrar, Straus and Giroux.ISBN 0-460-02281-4.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) Originally published in 1950. Gives a sympathetic and witty account of Haydn's life, along with a survey of the music.
  • Jones, David Wyn (2009a)The Life of Haydn. Oxford University Press. Focuses on biography rather than musical works; an up-to-date study benefiting from recent scholarly research on Haydn's life and times.
  • Jones, David Wyn (2009b)Oxford Composer Companions: Haydn. Oxford University Press. A one-volume encyclopedia with detailed contributions from many Haydn scholars.
  • Landon, H.C. Robbins (1976–1980).Haydn: Chronicle and Works. Bloomington, IN: Indiana University Press.ISBN 0-253-37003-5. An extensive compilation of original sources in five volumes.
  • Landon, H. C. Robbins; Jones, David Wyn (1988).Haydn: His Life and Music. Indiana University Press.ISBN 978-0-253-37265-9.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) Biography chapters by Robbins Landon, excerpted from Robbins Landon (1976–1980) and rich in original source documents. Analysis and appreciation of the works by Jones.
  • Larsen, Jens Peter (1980). "Joseph Haydn".New Grove Dictionary of Music and Musicians.{{cite encyclopedia}}:Invalid|ref=harv (help) Published separately asThe New Grove: Haydn. New York: Norton. 1982.ISBN 0-393-01681-1.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
  • Webster, James; Feder, Georg (2001). "Joseph Haydn".The New Grove Dictionary of Music and Musicians. Published separately as a book:The New Grove Haydn. New York: Macmillan. 2002.ISBN 0-19-516904-2. Careful scholarship with little subjective interpretation; covers both life and music, and includes a very detailed list of works.
  • Geiringer, Karl; Irene Geiringer (1982). Haydn: A Creative Life in Music (3rd ed. ed.). University ofCalifornia Press. pp. xii, 403.ISBN 0-520-04316-2.
Kuhusu kazi zake
  • Brendel, Alfred (2001). "Does classical music have to be entirely serious?". Katika Margalit, Edna; Margalit, Avishai (whr.).Isaiah Berlin: A Celebration. Chicago: University of Chicago Press. ku. 193–204.ISBN 0-226-84096-4.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) On jokes in Haydn and Beethoven.
  • Celestini, Federico (2010). "Aspekte des Erhabenen in Haydns Spätwerk". Katika Celestini, Federico; Dorschel, Andreas (whr.).Arbeit am Kanon. Vienna: Universal Edition. ku. 16–41.ISBN 978-3-7024-6967-2.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) On the sublime in Haydn's later works; in German.
  • Clark, Caryl, mhr. (2005).The Cambridge Companion to Haydn. Cambridge: Cambridge University Press.ISBN 0-521-83347-7. Covers each of the genres Haydn composed in as well as stylistic and interpretive contexts and performance and reception.
  • Griffiths, Paul (1983).The String Quartet. New York: Thames and Hudson.ISBN 0-500-01311-X.
  • Hughes, Rosemary (1966).Haydn String Quartets. London: BBC. A brief (55 page) introduction to Haydn's string quartets.
  • Rosen, Charles (1997).The classical style: Haydn, Mozart, Beethoven (tol. la 2nd). New York: Norton.ISBN 0-393-31712-9.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) First edition published in 1971. Covers much of Haydn's output and seeks to explicate Haydn's central role in the creation of the classical style. The work has been influential, provoking both positive citation and work (e.g., Webster 1991) written in reaction.
  • Sisman, Elaine (1993)Haydn and the classical variation. Cambridge: Harvard University Press.ISBN 0-674-38315-X.
  • Sutcliffe, W. Dean (1989). "Haydn's Musical Personality".The Musical Times.130 (1756): 341–344.doi:10.2307/966030.JSTOR 966030.{{cite journal}}:Invalid|ref=harv (help)
  • Sutcliffe, W. Dean (1992).Haydn, string quartets, op. 50. Cambridge: Cambridge University Press.ISBN 0-521-39103-2. Covers not just Op. 50 but also its relevance to Haydn's other output as well as his earlier quartets.
  • Webster, James (1991).Haydn's "Farewell" symphony and the idea of classical style: through-composition and cyclic integration in his instrumental music. Cambridge: Cambridge University Press.ISBN 0-521-38520-2.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help) This book focuses on a single work, but contains many observations and opinions about Haydn in general.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  1. REDIRECTTemplate:EB9 poster

Rekodi za kazi zake

[hariri |hariri chanzo]
  • Joseph Haydn ame orodheshwa katika International Music Score Library Project


Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Joseph_Haydn&oldid=1317515"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp