Alitawala Urusi kamadikteta kwa unyama na kusababisha vifo vyamamilioni yawatu. Vifo vingi vilisababishwa na kufuta mali ya wakulima na kuwalazimisha kulima kama makundi, iliyosababisha njaa na kuua watu milioni 6 au zaidi.[3] Mnamo 1935 Stalin aliagiza katiba mpya iliyoweka mamlaka yote mkononi mwa Kamati Kuu(politbureau) ya chama alichoongoza. Pamoja na mabadiliko hayo alianza kempeni za "kusafisha" chama. Kuanzia mwaka 1935 raia elfu nyingi, pamoja na wanachama wa chama cha Kikomunisti na hata wajumbe wa Halmashauri Kuu(Central Committee) walikamatwa; wakibahatika waliamriwa kuhamia mji katika sehemu mbali na Moscow; wengine walihukumiwa na maelfu kuuawa. Katika kipindi cha "utakaso mkuu" viuongozi wengi wa zamani pamoja na viongozi wengi wa jeshi waliuawa. Katika kipindi hiki, takriban milioni 1.6 walikamatwa, watu 700,000 walipigwa risasi na idadi isiyojulikana ilikufa kutokana na mateso katika magereza ya polisi ya siri.[4]
Stalin alikubaliwa kama kiongozi wa nchi zote za kikomunisti pamoja naChina,Vietnam naKorea ya Kaskazini hadi kifo chake.
Stalin alikufa baada ya mshtuko wa ubongo; alikutwa kwenye nyumba yake tarehe 1 Machi 1953 akilala chini na kushindwa kuongea. Lavrentiy Beria, mkuu wa ujasusi na mwanachama wa Kamati Kuu ya Chama alidai baadaye kwamba alimsumisha Stalin[5].
Joseph Stalin alikuwa na wake wawili kwa vipindi tofauti: mke wa kwanza aliitwa Ekaterine Svanidize (1906-1907), na wa pili aliitwa Nadezhda Alliluyeva (1919-1932). Pia alikuwa nawatoto watatu walioitwa Yakov Dzhugashvilli, Vasily Dzhugashvilli na Svetlana Alliluyeva.
↑Conquest, Robert (1991). Stalin: Breaker of Nations. New York and London: Penguin. ISBN 978-0-14-016953-9, uk 64
↑Service, Robert (2004). Stalin: A Biography. London: Macmillan. ISBN 978-0-333-72627-3, uk 276
↑Khlevniuk, Oleg V. (2015). Stalin: New Biography of a Dictator. Translated by Nora Seligman Favorov. New Haven and London: Yale University Press. ISBN 978-0-300-16388-9, uk 110-111, 116
↑Felix Chuev: Molotov Remembers: Inside Kremlin Politics. Ed. Albert Resis. Ivan R. Dee, Chicago 1993, ISBN 1-56663-027-4, uk
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuJosef Stalin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.