Jiometria inajulisha ukubwa wa pembetatu. Jiometri (pia:Jiometria , kutokaneno laKigiriki γεωμετρία,geometria , linaloundwa na geo- "dunia " na -metron "kipimo ", kwa kupitiaKiingereza geometry ) nitawi lahisabati linalochunguzaukubwa ,mjao ,umbo na mahali paeneo augimba .
Tawi la jiometri linalochunguzapembetatu hasa huitwatrigonometria .
Maumbo huwa nanyanda (dimensioni)mbili yakiwa bapa, autatu kama ni gimba. Kwa mfanomraba ,pembetatu naduara ni bapa na kuwa na nyanda 2 zaupana naurefu . Kumbetufe (kamampira ) aumchemraba huwa na nyanda 3 za upana, urefu nakimo (urefu kwenda juu).
Maumbo ya jiometri yalionekana kwanza nchiniMesopotamia naMisri katikamilenia ya pilibaada ya Yesu Kristo . Maumbo haya yalikuwa na urefu, uwanda ambazo zilitumika katika kupimaardhi na kuzurusayari nyingine.
Jiometri hutumiwa kupima eneo namzingo waumbo bapa . Inaweza kupima piamjao na eneo la uso wa gimba.
Katikamaisha ya kilasiku jiometri inasaidia kujua vipimo vya vitu vingi kama vile:
Chanzo cha jiometri kilikuwaelimu ya kupima ukubwa wa eneo fulani, kwa mfano eneo lamashamba yakijiji kwa kusudi la kuligawa kati yawatu wake.
Mtaalamu waUgiriki ya Kale aliyeitwaEuklides alitungakitabu cha kwanza kinachofahamika kuhusu jiometri.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo yahisabati bado nimbegu . Je, unajua kitu kuhusuJiometri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari .