Jina nineno au maneno ambayo wanapewawatu,wanyama,nchi,vitu n.k. kwa ajili ya utambulisho.
Utamaduni, kwa njia yasheria audesturi, ndio unaoratibu namna ya kupanga na kutumia majina ya watu, kwa kawaida tangukuzaliwa.
Mara nyingi, pamoja na jina binafsi,mtu anatumia pia majina mengine kama vile laukoo mzima, au lababa na lababu.
Katika nchi namakabila mbalimbali jina linaweza kubadilishwa, kwa mfano wakati waibada ya kuingizwa katikadini fulani au katikautawa, au kuongezewa, kwa mfano kutokana nandoa.
Wasanii kamawaimbaji auwaandishi mara nyingi hutumiajina la kisanii badala ya jina la kawaida.
Mara nyingine jina linafupishwa, hasa kama ni refu mno, au linapambwa kama kwa kumbembeleza mwenye nalo.
Kila aina ya wanyama inapewa jina maalumu la kuwatofautisha na wengine. Mfano:tembo akitajwa jina lake humtofautisha natwiga.
Kila nchiduniani lina jina lake maalumu ambalo huitambulisha nchi husika pamoja naraia wake.