Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Jeshi Jekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Jeshi Jekundu
Leon Trotsky (wa tatu kutoka kushoto) alianzisha Jeshi Jekundu

Jeshi Jekundu (kwaKirusi Красная армияKrasnaya armiya, kwaKiingerezaRed Army) lilikuwajina lamajeshi yaUmoja wa Kisovyeti tangu kuanzishwa kwake hadimwaka1946.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Asili ya jina hilo ni kipindi baada yamapinduzi ya Urusi ya 1917 ambapo vikundi vilivyoongozwa naWakomunisti viliitwa "Wekundu" wakipigana na wapinzani wao walioitwa "Weupe" katikavita ya wenyewe kwa wenyewe yaUrusi. Chanzo cha jeshi hilo kilikuwawanamgambo kutokawafanyakazi waviwandani, pamoja naaskari kutoka vikosi vya Jeshi la Urusi vya wakati waVita Kuu ya Kwanza ya Dunia.Mwanasiasa mkomunistiLeon Trotsky alipanga vyanzo hivyo katika jeshi moja na kuanzisha Jeshi Jekundu. Tangu mwanzochama cha Kikomunisti kililenga kusimamia Jeshi Jekundu kwa njia yamakamisaa wa siasa kwenye kila ngazi ya jeshi hilo.

Baada ya kushinda wapinzani "Weupe" wa ndani Jeshi Jekundu lilishindwa katikavita dhidi yaPolandi mnamo19191921.

Baada yaushindi wa Wakomunisti jeshi lote la Urusi naUmoja wa Kisovyeti lilitwa "Jeshi Jekundu".

Kabla yaVita Kuu ya Pili ya Dunia jeshi hilo liliathiriwa na takasa ya kisiasa, ambakomajenerali wengi walishtakiwa kuwa wasaliti na kuuawa. Ukosefu wa viongozi bora ulionekana wakati wamashambulio dhidi ya Ufini ya miaka1939-1940 ambako Stalin alipaswa kukubali amani bila kufikia shabaha zake zote.

Wakati Umoja wa Kisovyeti ulishambuliwa naUjerumani mwaka1941, Jeshi Jekundu lilikuwa na matatizo makubwa kutetea nchi na uhaba waviongozi wenye uzoefu umetajwa kama sababu mojawapo. Lakini kwa jitihada kubwa Jeshi Jekundu lilifaulu kusimamisha Jeshi la Ujerumani na kuteteamji mkuuMoscow najiji kubwa la pili,Leningrad (leo: Sankt Peterburg). Baada ya kupokea msaada wateknolojia kutokaMarekani, hali ya jeshi ilikuwa afadhali likafaulu kurudisha Wajerumani polepole hadi mwaka1944, ambapoMarekani naUingereza zilishambulia Wajerumani upande wamagharibi kwa uvamizi waUfaransa.

Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia jina lilibadilishwa kuwa Jeshi la Kisovyeti (rus. Советская армия (СА)/sovjetskaya armiya).

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Jeshi_Jekundu&oldid=1427554"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp