Jasi (ing.gypsum) ni madini yanayoptikana mahali pengi ambayo kikemia nisulfati ya kalsi .Fomula yake ni CaSO4·2H2O. Ni madini laini sana yakiwa na ugumu wa 2 kwenyeskeli ya Mohs. Inaweza kukwaruzwa kwakucha.
Kiasili inapatikana mara nyingi kama fuwele; jasi safi haina rangi lakini ikichanganywa na madini mengine kuna fuwele za rangi kadhaa. Kwa matumizi ya kibinadamu huchomwa ikipatikana baadaye kama unga nyeupe. Unga wa jasi unaweza kuchanganywa na maji ukipokea umbo lolote baada ya kukauka tena.
Jasi imetumiwa tangu kale katika ujenzi, hasa kwenyelipu. Katika ujenzi wa kisasa bao za jasi na matofali ya jasi hutumiwa kujenga kuta za ndani zisizobeba mzigo. Kuta hizi za jasi huzuia au kuchelewesha moto ndani ya nyumba[1]. Hutumiwa pia kama dawa la kilimo na chalki ya ubao shuleni. Wasanii hutumia jasi kwa sanamu.
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuJasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.