Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Japani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Japani
日本国Nihon-koku auNippon-koku (Kijapani)
Wimbo wa taifa:君が代
Kimigayo ("Utawala wa Mtukufu wa Kifalme")
Mahali pa JapaniMahali pa Japani
Mji mkuu
na mkubwa
Tokyo
Lugha rasmiKijapani
Lugha ya taifaAinu (inayotambuliwa), Kiryukyuan, Hachijō (hazijatambuliwa)
  Mfalme
Naruhito
  Waziri Mkuu
Shigeru Ishiba
Historia
  Katiba ya Meiji
29 Novemba 1890
  Katiba ya sasa
3 Mei 1947
Eneo
  Jumlakm2 377,975(ya 62)
  Maji (asilimia)1.4%
Idadi ya watu
  Kadirio la 2025123,400,000
  Msongamano330/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $6.741 trilioni
  Kwa kila mtu $54,678
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumladecrease $4.186 trilioni(ya 5)
  Kwa kila mtudecrease $33,956
HDI (2023) 0.925juu
Gini (2018)33.4
SarafuYen ya Kijapani (¥)
Majira ya saaUTCUTC+09:00 (JST)
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+81
Jina la kikoa.jp

Japani, ninchi yavisiwa katikaAsia ya Mashariki, iliyoko kwenyeBahari ya Pasifiki. Inapakana kwa maji naChina,Korea Kusini,Korea Kaskazini, naUrusi. Ina idadi ya watu takriban milioni 123, ikiwa ya 11duniani. Jiji lake kubwa zaidi namji mkuu niTokyo, moja yamiji yenye watu wengi zaididuniani. Japani imegawanyika katikamikoa 47, Inajulikana kwateknolojia yake ya hali ya juu,utamaduni wake wa kale na wa kisasa kamaanime na samurai, pamoja namiundombinu ya kisasa kama treni za mwendo kasi (Shinkansen).

Japani ni mojawapo yanchi zilizoendelea zaidikiuchumi duniani, ikiwa na mojawapo yapato la taifa kubwa zaidi kwa viwango vya kimataifa.Uchumi wake unaegemea hasa katikaviwanda vyateknolojia ya hali ya juu,magari, vifaa vya kielektroniki, naroboti. Makampuni makubwa kamaToyota,Sony, na Panasonic yanatoka Japani na yana ushawishi mkubwa duniani. Licha yarasilimali chache za asili, Japani imefanikiwa kukuzauchumi wake kupitiaubunifu,elimu ya juu, na nidhamu ya kazi miongoni mwa wananchi wake.

Katikahistoria, Japani iliwahi kuwamilki yakifalme iliyojitenga namataifa ya nje kwakarne nyingi, hadi ilipofunguka kwa dunia wakati wa kipindi cha Meiji mnamokarne ya 19. Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia, ambapo ilishambuliwa vikali ikiwemo mabomu ya atomiki mjiniHiroshima naNagasaki, Japani ilijengwa upya na kuwa taifa lakidemokrasia. Leo, ni mwanachama wa mashirika makubwa kamaUmoja wa Mataifa,G7, naG20, na ina ushawishi mkubwa katikasiasa,uchumi, nautamaduni wa kimataifa.

Jiografia

Japani nifunguvisiwa lenyevisiwa 14,125 mbele yapwani yaUchina,Korea naUrusi (Siberia).

Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu; ndivyoHonshu,Hokkaido,Shikoku naKyushu.Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababishamsongamano mkubwa wa wakazi katikamiji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutokasakafu ya bahari na vilele vyamilima yake huonekana juu ya uso wabahari kama visiwa vikubwa au vidogo.

Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambakomabamba ya gandunia yaUlaya-Asia,Pasifiki naUfilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwavolkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwamatetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu yapete ya moto ya Pasifiki inayozunguka bamba la Pasifiki.

Japani inapatwa kila mwaka nadhoruba kali aina yataifuni. Hatatsunami (ni neno laKijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari.

Nyumba ya kimapokeo.

Miji

Makala kuu:Miji ya Japan

Wajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa niTokyo,Yokohama,Nagoya,Osaka,Kyoto,Kobe,Hiroshima,Fukuoka,Kitakyushu,Sendai naSapporo.Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni yaShinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani.

Mikoa

Makala kuu:Mikoa ya Japani
Map of the prefectures of Japan inISO 3166-2:JP order and theregions of Japan

Japan ina mikoaarubaini na saba. Kila mkoa unasimamiwa nagavana mmoja,bunge na urasimu utawala. Kila mkoa umegawanyika katika miji na vijiji.


1. Hokkaidō


2. Aomori
3. Iwate
4. Miyagi
5. Akita
6. Yamagata
7. Fukushima


8. Ibaraki
9. Tochigi
10. Gunma
11. Saitama
12. Chiba
13. Tokyo
14. Kanagawa


15. Niigata
16. Toyama
17. Ishikawa
18. Fukui
19. Yamanashi
20. Nagano
21. Gifu
22. Shizuoka
23. Aichi


24. Mie
25. Shiga
26. Kyoto
27. Osaka
28. Hyōgo
29. Nara
30. Wakayama


31. Tottori
32. Shimane
33. Okayama
34. Hiroshima
35. Yamaguchi


36. Tokushima
37. Kagawa
38. Ehime
39. Kōchi


40. Fukuoka
41. Saga
42. Nagasaki
43. Kumamoto
44. Ōita
45. Miyazaki
46. Kagoshima
47. Okinawa

Kwa sasa manispaa za Japani zinaundwa upya kwa kuunganisha mikoa, miji na baadhi ya vijiji. Mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya miji nchini Japani.[1]

Historia

Visiwa vilikaliwa nabinadamu tangu miaka30,000 KK.

Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili (kamaWaainu) naWakorea waliovamia visiwa hivyo.

Uchumi

Japani ni nchi ya tatuduniani kwa ukubwa wauchumi.

Dini

Wajapani wanaweza kushirikiibada zadini mbalimbali kadiri wanavyojisikia, lakiniasilimia 60 hawana dini maalumu.Wabuddha ni asilimia 34, wafuasi wamadhehebu yaShinto ni asilimia 4,Wakristo sanasana ni asilimia 2.3.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Mabuchi, Masaru (2001)."Municipal Amalgamation in Japan (PDF)"(PDF). World Bank. Iliwekwa mnamo2006-12-28.{{cite web}}:Unknown parameter|month= ignored (help)

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Utalii
Taarifa za jumla
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaJapani bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuJapani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Japani&oldid=1423133"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp