Usimbishaji hutofautiana katika kanda mbalimbali ya kisiwa. Milima ya kaskazini-mashariki hupokea zaidi yamm. 5.000 lakini Kingston ina mm 813 pekee.Mvua inanyesha hasaMei,Juni,Oktoba naNovemba. Miezi yaSeptemba na Oktoba inaonadhoruba kali zatufani mara kwa mara.
Miji muhimu ikomwambaoni kwa sababu ya milima ya ndani.
Kingston ni mji mkubwa wenye wakazi karibulaki sita. Nimji mkuu na mahali pachuo kikuu kikubwa cha Jamaika. Mji ulikuwa na matatizo makubwa yausalama katika miaka ya nyuma.
Wakazi wa kwanza wa Jamaika walikuwaWataino ambao nikabila mojawapo laWaarawak kutokaAmerika Kusini. Walikuwawakulima nawavuvi. Wamepotea kamautamaduni wa pekee baada ya kufika kwa Wazungu kutokana na magonjwa mageni yaliyofika na Wahispania na mauaji wakati wa vita. Waliobaki waliingia katikandoa na Wazungu au Waafrika waliofika baadaye na kuwa sehemu ya wakazi chotara kisiwani.
Mwaka1655 Waingereza waliteka kisiwa wakaanzishauchumi wa mashamba makubwa yamiwa. Jamaika imekuwa mahali pakuu pa kutengenezasukari duniani kote. Watumwa wengi Waafrika walipelekwa kisiwani kamawafanyakazi kwenye mashamba hayo. Ndio mababu wa 90% wa wakazi wa leo wa Jamaika.
Wakazi asilia walikuwaWaarawak naWataino ambao hawako tena kama vikundi vya pekee; wengi walikufa kutokana namagonjwa yaWazungu auvita vya miaka ya kwanza baada ya kufika kwaWahispania. Wengine walichanganyikana na vikundi vingine.
Mbali ya wakazi, Wajamaika au wenye asili ya kisiwa kama 2,500,000 wanaishi nje ya nchi.
Muziki ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa Jamaika. Hasa muziki yaReggae umejulikana kote duniani.Mwanamuziki mashuhuri hasa wa Jamaika alikuwaBob Marley na kikundi chake cha "The Wailers".
Pia Wajamaika wana mafanikio makubwa katikariadha, hasa ya masafa mafupi.
Hall, D. Bounties European Immigration with Special Reference of the German Settlement at Seaford Town, Parts 1 and 2. Jamaica Journal, 8, (4), 48–54 and 9 (1), 2–9.
Makala hii kuhusu maeneo yaBahari ya Karibi bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuJamaika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.