J ni herufi ya 10 katikaalfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko waKiswahili cha kisasa. Asili yake niIota yaalfabeti ya Kigiriki.
Historia ya herufi J ni pamoja naI.
Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha mkono. Wafinisia walikuwa rahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la mkono "yad" (au: yod). Wakaitumia kama alama ya sauti "y" na pia ya "i" ndefu. Wagiriki wakaipokea kama "Iota" na kurahisisha umbo lake zaidi hadi kuwa mstari tu. Wakaitumia kwa sauti ya "i".
Alama ikaendelea hivyo katika alfabeti zaWaetruski na zaKilatini. Katika Kietruski ilimaanisha yote vokali ya "i" na konsonanti ya "y" na Waroma wakapokea vile katika Kilatini.
Katika Ulaya wa karne watu hasa Wajerumani walianza kuona haja ka kutofautisha kati ya sauti ya "i" na sauti ya "y" wakaanzisha kutofautisha kati ya "i" na "j" (kwa matamshi ya y). Lakini kwa muda mrefu hadi karne ya 19 mwandishi wa I na J haukufuata utaratibu uliokubaliwa.
Wasemaji wa lugha kamaKiingereza naKifaransa walitumia "J" kwa sauti ya "j" jinsi ilivyoingia katika Kiswahili.