Israel (kwaKiebrania:מדינת ישראל -Medinat Yisra'el; kwaKiarabu:دَوْلَةْ إِسْرَائِيل -dawlat Isrā'īl) , rasmiDola la Israel, ni nchi iliyoko Magharibi mwaAsia. Iko katika eneo la Kusini mwa Levant katika Mashariki ya Kati; na inapakana naLebanoni naSyria upande wa kaskazini, Ukingo wa Magharibi naJordan upande wa mashariki, Ukanda waGaza naMisri upande wa kusini-magharibi, na Bahari ya Mediterranean upande wa magharibi. Israel pia ina pwani ndogo kwenyeBahari ya Shamu kwenye pointi yake ya kusini kabisa, na sehemu yaBahari ya Chumvi inapatikana kando ya mipaka yake ya mashariki. Mji wake mkuu niYerusalemu, wakatiTel Aviv ni eneo kubwa la mijini na kituo cha kiuchumi cha nchi hiyo.
Takriban 74.9% za wakazi niWayahudi ambao wengi wao wanafuatadini yaUyahudi, na 20.7 % niWaarabu ambao wengi niWaislamu (16%) lakini piaWakristo (2% za raia wote: kati ya Wakristo hao karibu 80% ni Waarabu).Wahamiaji wengi wasiopata uraia ni Wakristo.
1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuIsrael kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.