Kaaba nikibla ya Waislamu wote duniani wakati waswala.
Uislamu (kwaKiarabu: الإسلامAl-Islām) nidini inayotokana na mafunzo yaMtumeMuhammad. Wafuasi waimani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwamilioni 1,800 hivi. Hivyo ni dini ya piliduniani yenye wafuasi wengi baada yaUkristo wenye wafuasi milioni 2,400.
Uislamu ni ile imani kuwamuumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake.Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani yaMungu mmoja wa kweli, imani juu yamaisha baada yakifo, imani juu yaMalaika wa Mungu,vitabu vyake nakudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni:Sala,Zakah,Saumu naHija.
Imani na kitabu chake
Imani katika Uislamu ni kumwaminiMungu mmoja tu peke yake anayeitwaAllah, ambaye hajazaa wala hajazaliwa na hafanani na yeyote yule. Kitabu kitakatifu cha Waislam niQur'an ambayo inaaminiwa ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad kutoka kwa Mwenyezi Mungu mbinguni kupitiamalaikaJibrili; ni kawaida kusema Qurani "iliteremshwa" kwa Muhammad. Kwa imani hiyo, kabla yake walioteremshiwa kitabu niMusa (Torati),Daudi (Zaburi) naIsa (Injili).
Pamoja na Qurani kuna mafundisho yaSunna naHadith ambayo ni maneno ya mtume Muhammad na masimulizi juu ya matendo yake ambayo pengine hutazamiwa kama mwongozo katika Uislamu.
Qurani inasisitiza kwamba Allah hana mshirika, hana baba wala mwana, hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mwanzo wala mwisho.
Pamoja na amri mbalimbali kuna mfumo wa sheria za kidini zinazoitwa kwa jumla "sharia"; inajumlisha maagizo kuhusu mambo mengi ya maisha ya kila siku,uchumi nasiasa.
Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu malaika Jibril alimtokea alipokuwa na umri wa miaka 40 yaani mnamo mwaka610. Kutoka kwa malaika alipokea maneno ya Kurani naufunuo huu uliendelea hadi mwisho wa maisha yake.
Mtume alitangaza yale aliyosikia kwa wafuasi wake na maneno haya yalianza kukusanywa tayari wakati wa maisha ya mtume. Baada ya kifo chake mwaka 632khalifa wa tatuUthman ibn Affan alikusanya muswada na kumbukumbu zote na kuziweka pamoja na kuwa kitabu kamili.
Ujumbe uliohubiriwa na Muhammad huko Maka ulipata wasikilizaji wachache, lakini viongozi wengi waKikuraishi, waliokuwa kabila kubwa Maka, waliwaona kama hatari kwa Maka na mwaka622 Waislamu walipaswa kutoka Maka wakahamiaYathrib mji wa jirani uliojulikana baadaye kama Madina.
Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye "madinat an-nabi"" ikajulikana kwa kifupi kamaMadina.
Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuzaWayahudi wa Yathrib.
Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu liliingia mjini Maka.
Mtume alipoaga dunia mwaka 632 sehemu kubwa ya Bara Arabu ilikuwa chini ya Uislamu tayari.
Mafunzo ya Uislamu
Uislamu unawafunza wafuasi wake mambo mengi yanayohusiana na maisha, ikiwa yale yanayohusuibada kama Sala, Zakat, Saumu na Hija; ambazo pamoja na kauli yaShahada ("Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake") huitwa nguzo za Uislamu au yale yanayohusu maingiliano baina ya wanadamu, yakiwa maingiliano ya kijamii kamandoa natalaka naujirani mwema, au ya kiuchumi kamabiashara, au ya kisiasa kama kawaida za kumchagua kiongozi wadola, au ya uhusiano baina ya mataifa mbali mbali ulimwenguni.
Waislamu wanatazama Uislamu kuwa mfumo kamili wa maisha yabinadamu, kiimani, kimaisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Ibada katika Uislamu
Ibada katika Uislamu ni vile vitendo ambavyo Muislamu anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, kwani ibada yoyote haitakikani iwe na ushirikina ndani yake, na wakati itakapokuweko aina yoyote ya shirki basi ibada ile inakuwa haina maana wala thawabu wala ujira wowote, ni kazi ya bure.
Kwa hiyo, kila Muislamu anatakikana wakati anapofanya ibada yake afanye kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba akampa kila aina yaneema na kumtukuza kuliko viumbe vingine vyovyote, kwa kumpaakili,fahamu naelimu.
Kuna matendo kadhaa ambazo zinaitwa "Nguzo za Uislamu". Kwa kawaida ni tano zinazofundishwa katikamadhehebu yaWasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.
Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi kwa nguzo tano halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano.
Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili:Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.
Salat: (Kiarabu: صلاة) nisala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanyawudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti nadua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
Zakat: (Kiarabu: زكاة) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mweziRamadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
Hajj (Kiarabu: الحجّalhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijjaMaka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.
Maingiliano katika Uislamu
Uislamu umeweka kawaida mbali mbali katika maisha wakati watu wanataka kuweka uhusiano fulani baina yao ili mambo yaende vizuri na uhusiano uzidi kuwa mwema baina yao. Katika maingiliano yaliyowekewa kawaida na nidhamu katika Uislamu ni mambo yanayohusu:
Nikaha au ndoa baina ya Waislamu
Biashara na mambo yanayohusu uchumi
Uhusiano wa kijamii baina ya watu katika mtaa au kijiji au mji au nchi
Uhusiano wa kimataifa baina ya madola mbali mbali, yakiwa ya kiislamu au yasiyokuwa ya kiislamu.
Vikundi na madhehebu
Kuna mielekeo mikubwa miwili ndani ya Uislamu ambayo ni vikundi vyaWasunni 85-90% naWashia 10-15%.
Kundi kubwa ni Wasunni waliopata jina kutokana na Sunna ("kawaida") ya mtume; takriban asilimia 85-90 ya Waislamu wote huhesabiwa humo. Kati yao kuna madhehebu 4 ambao ni Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafii. Tofauti katika mafundisho si kubwa, zinahusu hasasharia nafikh.
Kundi dogo zaidi ni Washia ambao wamegawanyika kati yao katika vikundi vingi. Washia walijitenga na Wasunni baada ya makhalifa wanne wa kwanza kuhusu swali ni nani anayefaa kuongoza Waislamu. Washia ni wale waliosisitiza sharti awe mtu kutoka ukoo wa Muhammad kupitia binti yakeFatima. Vikundi vya Washia vinatofautiana juu ya viongozi hawa. Jumuiya kubwa ya Washia niIthnashara walio wengi hukoUajemi,Irak naLebanoni.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.