Kuhusu kundi la kigaidi linaloitwa ISIS, angaliaDaish
Isis
Isis alikuwa mmoja wamiungu katikadini yaMisri ya Kale. Alikuwa mungu wa kike aliyeabudiwa na Wamisri wengi katika maisha ya kila siiku kwa sababu aliaminiwa kuhusika na shughuli za uzazi na kujifungua, na kutoka hapa maombi mengi ya uponyaji yalilengwa kwake.
Kama mungu wa uhai na uchawi, Isis aliwalinda wanawake na watoto, na kuwaponya wagonjwa. Alitazamiwa kama mama wa kimungu wa kilafarao (mfalme).
Katika mitholojia ya Misri aliunganishwa hasa naOsiris (mume wake wa kimungu) naHorus (mwana wa Osiris na Isis). Ibada ya Isis iliendelea muda mrefu hadi kipindi cha utawala wa Kiroma, ikaenea pia nje ya Misri katika Dola la Roma.
Alama zake zilikuwaankh, mabawa yake, nataji lilionyesha kiti cha kifalme.