Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Indonesia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Indonesia
Republik Indonesia (Kiindonesia)
Kaulimbiu:Bhinneka Tunggal Ika (Kijava cha Kale)
"Umoja katika Tofauti"
Wimbo wa taifa: "Indonesia Raya"
Eneo la Indonesia katika ASEANEneo la Indonesia katika ASEAN
Indonesia katika duniaIndonesia katika dunia
Mji mkuu
na mkubwa
Jakarta
Lugha rasmiKiindonesia
SerikaliJamhuri ya kirais ya muungano
  Rais
Prabowo Subianto
  Makamu wa Rais
Gibran Rakabuming Raka
  Uhuru kutangazwa
17 Agosti 1945
  Kutambuliwa rasmi
27 Desemba 1949
Eneo
  Jumlakm2 1,904,569(ya ya 14)
  Maji (asilimia)4.85%
Idadi ya watu
  Kadirio la 2024 284,973,643
  Msongamano143/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $4.98 trilioni
  Kwa kila mtu $17,520
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $1.49 trilioni
  Kwa kila mtu $5,248
HDI (2023)0.728juu
Gini (2024)37.9
SarafuRupia ya Indonesia (Rp)
Majira ya saaUTCUTC+7, +8, +9 (WIB, WITA, WIT)
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu++62
Jina la kikoa.id

Indonesia ninchi ya visiwa katikaAsia ya Kusini-Mashariki. Iko upande waKusini-Mashariki kati yaBahari ya Hindi naPasifiki.Visiwa vyake ni sehemu yaFunguvisiwa la Malay, ingawa Guinea Mpya kwa kawaida haihesabiwi katika fungu hilo. Indonesia imepakana naPapua Guinea Mpya kwenye kisiwa chaGuinea Mpya, pia naTimor ya Mashariki kwenye kisiwa chaTimor, halafu naMalaysia kwenye kisiwa chaBorneo. Nchi nyingine zilizo karibu niAustralia,Singapuri naUfilipino.

Indonesia nitaifa lenye wakazi wengi waKiislamuduniani, likiwa na watu wanaozidimilioni 280, na hivyo kuifanya kuwa nchi ya nne kwa idadi ya watuduniani.Mji mkuu wake niJakarta,jiji kubwa lenye shughuli nyingi zakisiasa,kiuchumi nakitamaduni.Lugha rasmi niKiindonesia (Bahasa Indonesia): ingawa kuna zaidi yalugha 700 zinazozungumzwa nchini humo, lugha hiyo inatumika kama chombo cha kuunganisha wananchi wamakabila mbalimbali.

Historia ya Indonesia imeathiriwa na mchanganyiko wadini,biashara naukoloni. Kabla ya ukoloni, Indonesia ilikuwa nyumbani kwafalme mbalimbali zenye ushawishi mkubwa kama vileSrivijaya naMajapahit. Katikakarne ya 16,Wareno na baadayeWaholanzi walifika na kudhibiti maeneo mengi, hasa kupitia Kampuni ya Kiholanzi ya India ya Mashariki. Indonesia ilijipatiauhuru kutoka kwaUholanzi mwaka1945 chini yauongozi waSukarno. Tangu wakati huo, nchi imepitia vipindi mbalimbali vya kisiasa, ikiwa ni pamoja nautawala wa kijeshi, hadi kuanzishwa kwademokrasia ya kisasa mwishoni mwakarne ya 20.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Indonesia ni nchi ya visiwa karibu 18,000 ilhali zaidi ya 6,000 kati ya hivyo vinakaliwa nawatu.

Visiwa vikubwa vyenye wakazi wengi ni hasa vitano:

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Visiwa vya Indonesia viliathiriwa nautamaduni waUhindi.Kisiasa kulikuwa nafalme nyingi.

Tangukarne ya 17Waholanzi walianza kujenga vituo na kuenezautawala wao. Waliitakoloni lao "Uhindi wa Kiholanzi" ("Nederlands-Indie").

Wakati waVita Kuu ya Pili ya DuniaJapani ikatwaa visiwa na kuwafukuza Waholanzi.

Mwisho wa vitakiongoziSukarno akatangaza Indonesia kamanchi huru. Waholanzi walijaribu kurudisha utawala wao lakini walilazimishwa naMarekani kukubaliuhuru wa nchi.

Demografia

[hariri |hariri chanzo]

Nchi ina wakazi 270,203,917 (2020) hivyo ina nafasi yanne kati yamataifa makubwaduniani. Ni nchi yenyeWaislamu wengi kuliko nyingine zote duniani.Makabila asili ni 300 hivi; kubwa zaidi niWajava (40.2%).

Lugha rasmi ni Bahasa Indonesia (Kiindonesia) iliyoundwa katikakarne ya 20 kamalugha ya taifa kutokana nalahaja yaKimalay. Nchini kote kunalugha za asili zaidi ya 700 (angaliaorodha ya lugha za Indonesia). Jawa pia inasanaa yamwandiko wa kipekee maarufu kama mwandiko waBatiki (Batik Tulus) unaochorwa kwajora zanguo.[1]

Idadi kubwa ya wakazi (87.1 %) wanahesabiwa kuwa Waislamu (karibu woteWasuni), 10.45 % kamaWakristo (Waprotestanti 7.38 %,Wakatoliki 3.07 %), 1.7 % kamaWahindu (hasa kwenye kisiwa chaBali) na 0.7 % kamaWabuddha. Hizo zote nidini zilizotambulika rasmi pamoja na ile yaKonfusio (0.05 %).

Mandhari

[hariri |hariri chanzo]
  • National Museum of Indonesia, Central Jakarta
    National Museum of Indonesia,Central Jakarta
  • Wisma 46, jengo refu kuliko yote ya Indonesia, likiwa Jakarta
    Wisma 46, jengo refu kuliko yote ya Indonesia, likiwa Jakarta
  • Jalan Thamrin, barabara muhimu zaidi ya Central Jakarta
    Jalan Thamrin, barabara muhimu zaidi ya Central Jakarta
  • Treni katika stesheni ya Gambir, Central Jakarta
    Treni katika stesheni yaGambir,Central Jakarta
  • Bung Karno Stadium inaweza kupokea watazamaji 100,000
    Bung Karno Stadium inaweza kupokea watazamaji 100,000
  • Ramani ya Indonesia
    Ramani ya Indonesia
  • Wilaya za Indonesia
    Wilaya za Indonesia
  • Malioboro, barabara muhimu zaidi huko Yogyakarta
    Malioboro, barabara muhimu zaidi huko Yogyakarta
  • Trans Jogja Bus, mwendokasi wa Yogyakarta
    Trans Jogja Bus, mwendokasi wa Yogyakarta
  • Mapishi ya Kiindonesia: Soto Ayam (chicken soup), sate kerang (shellfish kebabs), telor pindang (preserved eggs), perkedel (fritter) na es teh manis (sweet iced tea)
    Mapishi ya Kiindonesia:Soto Ayam (chicken soup),sate kerang (shellfish kebabs),telor pindang (preserved eggs),perkedel (fritter) naes teh manis (sweet iced tea)
  • An Indonesian Army infantryman participating in the U.N.'s Global Peacekeeping Operation Initiative
    An Indonesian Army infantryman participating in the U.N.'s Global Peacekeeping Operation Initiative
  • Pindad Panser "Anoa" shown during Indo Defense and Aerospace Expo 2008
    Pindad Panser "Anoa" shown during Indo Defense and Aerospace Expo 2008
  • B-25 Mitchell bombers of the AURI in the 1950s
    B-25 Mitchell bombers of the AURI in the 1950s
  • A Javanese engineer closes one of the gun bay doors on a Dutch Buffalo, Januari 1942.
    AJavanese engineer closes one of the gun bay doors on a DutchBuffalo, Januari 1942.
  • GE U20C in Indonesia, #CC201-05
    GE U20C in Indonesia, #CC201-05
  • GE U20C "Full-Width Cabin" in Indonesia, #CC203-22
    GE U20C "Full-Width Cabin" in Indonesia, #CC203-22
  • GE U20C full computer control locomotive in Indonesia, #CC204-06
    GE U20C full computer control locomotive in Indonesia, #CC204-06

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Batik S128."Handwriting Batik (Batik Tulis) and Cities In Indonesia That Produce It".Toko Batik Online 2019. Iliwekwa mnamo2019-05-11.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Serikali
Taarifa za jumla
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Indian OceanPapua New Guinea
  Indonesia   
Indian Ocean
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Indonesia&oldid=1456292"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp