Indochina ni jina la kijiografia linalojumlisha maeneo ya kibara yaAsia ya Kusini-Mashariki (bila visiwa) upande wa kusini yaChina na upande wa mashariki yaUhindi.
Kiutamaduni nchi hizi ziliathiriwa na Uhindi na China kwa viwango tofauti. Kwa jumla athira ya Uhindi ilikuwa kubwa lakini Vietnam imepokea mengi zaidi kutoka China.
Dini kuu niUbuddha hasa dhehebu yaTheravada. Ubuddha yaMahayana iko zaidi Vietnam. Malaysia ina Waislamu wengi. Wahindu si wengi kwa sababu kihistoria Ubuddha ilichukua nafasi ya Uhindu.
Wakristo si wengi kwa jumla lakini makabila kadhaa yamepokea Ukristo kama sehemu za utamaduni wao.