Msalaba wa Ijumaa Kuu kwenyeMonasteri yaUtatu Mtakatifu ,Meteora ,Ugiriki .Picha takatifu yakarne ya 16 ikionyesha tendo la kumsulubuYesu kadiri yaTheophanes wa Krete (Stavronikita Monastery ,Mlima Athos ,Ugiriki ).Siku ya Ijumaa KuuWakatoliki wanapokeaekaristi ingawaMisa haiadhimishwi (Our Lady of Lourdes,Philadelphia ,Marekani ). Njia ya Msalaba ikiadhimishwa kwenyeColosseum mjiniRoma siku ya Ijumaa Kuu. Mwishoni,Papa anatoa neno.Picha yaEl Greco ikimuonyeshaYesu akibeba msalaba ,1580 .Epitafyo yaKiorthodoksi ikionyeshamwili wa Yesu ukizikwa.Epitafyo ikichukuliwa katikamaandamano . Ijumaa Kuu nisiku yaIjumaa kabla yaPasaka ambapoWakristo wengiduniani wanaadhimishakifo chaYesu Kristo msalabani .
Kufuatana na taarifa zaInjili nne katikaBiblia ya Kikristo ,Yesu alisulubiwa siku kabla yaSabato (auJumamosi ), yaani Ijumaa. Mahali pa kumsulubisha palikuwakilima chaGolgotha kilichokuwepo wakati ule nje yakuta zamji waYerusalemu .
Kadiri yaInjili yaMtume Yohane , kesho yake ilikuwaSabato na piaPasaka , jambo lisilotokea kila mwaka. Kwa sababu hiyowataalamu mbalimbali wameweza kukadiria ilikuwatarehe 7 Aprili 30 .
Sikukuu hii haina tarehe thabiti katikakalenda ya kawaida. Ilhali hutangulia Pasaka inafuata pia mabadiliko ya tarehe za Pasaka. Pamoja namapokeo yaliyo tofauti kati yaUkristo wa Magharibi (Wakatoliki naWaprotestanti wengi) naUkristo wa Mashariki (makanisa ya Kiorthodoksi naWakatoliki wa Mashariki ), kuna tarehembili tofauti za Pasaka, na hivyo pia kila mwaka kuna tarehe mbili tofauti za Ijumaa Kuu.
Mwaka Ukristo wa Magharibi Ukristo wa Mashariki 2018 30 Machi 06 Aprili 2019 19 Aprili 26 Aprili 2020 10 Aprili 17 Aprili 2021 02 Aprili 30 Aprili 2022 15 Aprili 22 Aprili
Ijumaa kuu ni sehemu yaJuma Kuu linaloanza kwa adhimisho laYesu kuingia mji huo akishangiliwa kamamfalme wa Wayahudi (yaaniMasiya auKristo ). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwawiki , yaaniJumapili ya matawi .
Ijumaa kuu ni pia sehemu yasiku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso nakifo chake (Ijumaa ), kulalakaburini (Jumamosi ), na hatimayekufufuka kwautukufu (Jumapili ), kwa ufupi:
Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka. Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu . Je, unajua kitu kuhusuIjumaa Kuu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari .