Kwa ujumlahali ya hewa ni baridi nabarafuto zinafunika sehemu kubwa ya nchi. Hasanyanda za juu ni baridi mno, hivyo hakunamimea. Karibu makazi yote ya watu ni karibu na pwani.
Kusini mwa kisiwa haikuwa baridi mno kwa sababu yamkondo wa ghuba linaloendelea kusukumamaji yaghuba ya Meksiko hadi Atlantiki ya kaskazini.Mkondo huo unapofikia Isilandi si yamoto tena lakinivuguvugu kidogo hivyo inazuia baridi kali sana.
Volkeno zimesababisha kuwepo kwamaji ya moto mahali pengi. Waisilandi wanapenda kuogelea nje katika mabwawa hata wakati watheluji katika maji ya moto kutokana najoto la kivolkeno. Joto hilo linatumika kidogo hata kwakilimo; linapasha motonyumba za kioo na kuwezesha mimea kuzaa matunda mwaka wote, hata wakati wa baridi kali. Kwa njia hiyo Isilandi inavunandizi na machungwa yake!
Hakika waliofika wengi kidogo walikuwaWaviking au Wanorwei wa kale katikakarne ya 9. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwajina alikuwaFlóki Vilgerðarson.
Waviking waliofika walikuja pamoja nafamilia nawatumishi auwatumwa wao. Mnamo mwaka930 machifu na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina yakatiba kwa Isilandi. Walianzishabunge laAlthing. Ulikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa nacheo cha kuunganishamadaraka yachifu,hakimu nakuhani. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Isilandi ni nchi ya pekee ambako utaratibu wakidemokrasia wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi yawafalme auwatawala wengine iliongezeka na kumezahaki zote za watu wa kawaida.
Mwaka985 Mwisilandi aligundua njia ya kufika Grinilandi na baadayeAmerika ya Kaskazini. Mviking "Erik Mwekundu" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwamwuaji. Alielekeamagharibi kwajahazi yake na kufika kwanza Grinilandi halafupwani yaKanada ya leo. Aliita bara jipya "nchi yamzabibu" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila matunda.
Tangu1262 uhuru wa Isilandi ulikwisha kwa sababu viongozi walijiunga naUfalme wa Norwei. Isilandi iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali - hasa kwa sababuusafiri uliendelea kuwa mgumu - lakini mabwana wakuu walikuwa sasa wafalme waSkandinavia, kwanza Wanorwei, baadayeWadeni.
Mwaka1918Udeni ilirudisha madaraka yote yaserikali kwa Waisilandi wenyewe isipokuwa mfalme wa Udeni aliendelea kama Mkuu wa nchi.
Wakati waVita Kuu ya Dunia ya Pili Udeni ilivamiwa naUjerumani na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka1944 Isilandi ilipatauhuru kamili.
Baada yavita kwisha Isilandi ilipata kuwa nchi mwanachama yaNATO lakini hainawanajeshi hadi leo. Ilifanyamkataba naMarekani ya kuwa Wamarekani wanapewahaki ya kutumia kituo chandege kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Isilandi.
Watu wa Isilandi karibu wote (92.61%) niWaskandinavia. Kati ya wengine,Wapolandi ndio wengi (3.36%).
Lugha ya Kiisilandi bado inafanana sana na ile yaKinorwei cha kale kilicholetwa kisiwani na wakazi wa kwanza miaka 1000 iliyopita. Watu bado wanaelewa mashairi yaliyotunzwa tangu zamani ile.
Kanisa la kitaifa la Kilutheri nidini rasmi ya nchi. Hivyo Waisilandi wengi (73.8%) wanahesabiwa kuwaWakristoWalutheri, ingawa wengi hawafuatidini. Wakristo wamadhehebu mengine, kama vileWakatoliki, wanafikia 11.7%. Kuna wafuasi wachache sana waimani nyingine mbalimbali. Kwa jumla Isilandi ni kati ya nchi ambazo zina wakazi wengi wasiomuaminiMungu.
Hadi leo Waisilandi hawana majina ya pili au yafamilia. Kilamtoto anapewajina lake la kwanza halafu jina lababa - wakati mwingine pia jina lamama. Kama mtoto ni wa kiume "-son" (=mwana) itaongezwa, kama ni binti "-dottir" (binti).
Kwa mfanomwimbaji mashuhuri wa kikeBjörk Guðmundsdóttir alipewa jina la "Björk". Baba yake alikuwa Guðmund hivyo anatumia jina hili pamoja na "-dottir": Guðmundsdottir: "Björk binti Guðmund". Kama mwenyewe atamzaabinti anaweza kuitwa "Björkdottir" lakini mara nyingi jina la baba hutumiwa.Wanawake wanaendelea na jina hili, hawaliachi wakati wa kuolewa.
Jonsson, Asgeir (2008).Why Iceland? How One of the World's Smallest Countries Became the Meltdown's Biggest Casualty. McGraw–Hill Professional.ISBN978-0-07-163284-3.
Jonsson, Ivar (2012) 'Explaining the Crisis of Iceland – A Realist Approach' in Journal of Critical Realism, 11,1.
Heiðarsson, Jakob Oskar (2015) 'Iceland - My Small Island'.
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuIsilandi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.