Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ibuti la Jauza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mshale wa rangi ya pinki unaoelekeza nyota upande wa kulia yenye alama yaα unaonyesha Ibuti la Jauza (Betelgeuse) katika kundinyota ya Jabari (Orion)
Ibuti la Jauza (Betelgeuze) nijitu jekundu; kushoto: inavyoonekana kwa darubini; kulia:Ibuti la Jauza (Betelgeuze) ni nyota angavu juu kushoto kwenyekundinyota yaJabari (Orion) mara nyingi huonekana nyekundu kwa macho matupu.

Ibuti la Jauza (jina la kisayansiAlpha Orionis, kwaKiingerezaBetelgeuse) ninyota ya aina yajitu jekundu inayoonekana katikakundinyotaJabari (Orion).

Jina

Jina la Ibuti la Jauza lilijulikana tangukarne nyingi kati yamabaharia Waswahili waliotumia nyota hii kama msaada wa kukutanjia yaobaharini wakati wausiku.Asili ya jina niKiarabuإبط الجوزاء (ibt al jauza) . Ibuti inamaanisha "kwapa" na Jauza ni ni jina la zamani kwa Jabari, kwa maana ya "katikati" maana kuna majira ambako nyota hizo ziko katikati kwenye anga. Jina la Kirabu lilipokewa pia nawanaastronomia waUlaya wakati wakarne za kati na kwa matamshi ya kigeni kutoka "i-bt-al-geusa" kuwa "Bet-el-geuse".[1]

Jina la kitaalamu la kisasa ni "Alpha Orionis" (α Orionis) kwa sababu ilionekana kuwa nyota angavu zaidi katika kundiyota yake.[2]. "Betelgeuse" ilikubaliwa na kuthibitishwa naUKIA kuwa jina maalum.[3].

Uangavu na umbali

Ni nyota angavu yatisa kati ya nyota zote zinazoonekanaangani na nyota angavu ya pili kwenye Sayadi (Orion). Uangavu wake unachezacheza kati ya vipimo vya 0.2 na 1.2.[4]

Umbali wake nadunia ulikadiriwa mnamo mwaka2008 kuwamiakanuru 640[5]

Hali ya nyota

Umri wa Ibuti la Jauza haukutimiza miakamilioni 10 lakini umeendelea haraka kutokana namasi yake kubwa.[6]

Ibuti la Jauza imeshaendelea kufikia ngazi za mwisho zamageuzi ya nyota (stellar evolution). Katika kipindi cha miaka milioni 1 ijayo inakadiriwa kutimiza mageuzi yake hadi kulipuka kamanyota nova.[7]

Tazama pia

Marejeo

  1. Jan Knappert, "The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations", katika jarida la The Indian Ocean Review, 6-1993, uk 5-7
  2. Hata hivyo Ibuti la Jauza ilipewa jina la "alfa Orionis" katikaorodha ya Bayer inayomaanisha ni nyota angavu kushinda nyingine katika kundi la nyota; inawezekana Bayer aliiona wakati iling'aa zaidi, maanamwangaza wake unachezacheza, lakini kwa kawaidaRijili Kantori (Rigel) inang'aa zaidi.
  3. Naming Stars, tovuti yaUmoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia|UKIA), iliangaliwa Novemba 2017
  4. Davis, Kate (AAVSO Technical Assistant, Web) 2000. Variable star of the month: Alpha Orionis.American Association of Variable Star Observers (AAVSO).[1]
  5. Harper, Graham M.et al. 2008. A new VLA-Hipparcos distance to Betelgeuse and its implications.The Astronomical Journal135 (4): 1430–40.[2]
  6. Levesque E.M. 2010. The physical properties of red supergiants.Astronomical Society of the Pacific. 425 Hot and Cool: Bridging Gaps in Massive Star Evolution ASP Conference Series:103.[3]
  7. "Betelgeuse braces for a collision". ESA. 2013-01-22. Iliwekwa mnamo2013-01-23.


Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Mars and Orion Over Monument Valley Skyscape showing the relative brightness of Betelgeuse and Rigel.
  2. Orion: Head to Toe Breathtaking vista the Orion Molecular Cloud Complex from Rogelio Bernal Andreo.
  3. The Spotty Surface of Betelgeuse A reconstructed image showing two hotspots, possibly convection cells.
  4. Simulated Supergiant Star Freytag's "Star in a Box" illustrating the nature of Betelgeuse's "monster granules".
  5. Why Stars Twinkle Image of Betelgeuse showing the effect of atmospheric twinkling in a telescope.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ibuti_la_Jauza&oldid=1327337"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp