Ibn Khaldūn (jina kamili kwa Kiarabu ni أبو زيد عبد الرحمن بن محمد بن خلدون الحضرميAbū Zayd ‘Abdu r-Raḥman bin Muḥammad bin Khaldūn Al-Hadrami; mara nyingi kamaAbdul Rahman Ibn Khaldun) alikuwa mtaalamu Mislamu kutokaAfrika ya Kaskazini alyieishi wakati wa karne ya 14.Alizaliwa mjiniTunis mnamo1332 akaishi baadayeFez naGranada na miaka ya mwisho alikaaKairo alipokufa 1406.
Kimaitaifa anajulikana hasa kam mtaalamu bora wa historia. Lakini anatazamiwa pia kama mtangulizi muhimu katika fani kama falaki, uchumi, fiq-hi, hisabati, elimu ya jamii.
Aliandika mwenyewe kitabu cha "at-ta'rif bi-Ibn Chaldun wa-rihlatuhu gharban wa-scharqan / التعريف بابن خلدون ورحلته غربا وشرقا / taarifa ya Ibn Khaldun juu ya safari zake za magharibi na mashariki". Hasemi mengi juu ya maisha yake ya binafsi lakini anajieleza aliposoma, walimu wake na vitabu alivyosoma.Alikuwa mtoto wa familia ya makabaila walioitwa "banū chaldūn" walioishi miaka mingi hukoAndalusia (Hispania ya Kiarabu). Kiasili walitoka katikaYemeni. Wakati wa rekonkista yaani kipindi ambako Wahispania wenyewe walianza kuwasukuma Waarabu kutoa maeneo mengi ya nchi yao akina banu khaldun walihamia Afrika ya Kaskazini. Hapa mababu kadhaa wa Ibn Khaldun walipata vyeo muhimu chini ya watawala Waislamu. Babu na baba yake waliacha siasa wakajiunga natarikat yaWasufi.
Alifuata mapokeo ya familia akitafuta ajira serikalini kwa watawala malimbali wa Afrika ya Kaskazini. Nia hii ilimpeleka katika maisha ya hatari yingi kwa sababu wakati wake watawala walibadilika haraka wakiangushana na kuwa na vita kati yao. Kwa hiyo Ibn Khaldun alipata vvyeo vikuu vilivyofuatwa na vipindi katika jela na miaka alipopaswa kukimbia nchi yake.
Ajira ya kwanza ilikuwa kwenye ikulu ya mtawala waTunis alipokuwa na miaka 20. Alipewa cheo cha kātib al-ʿalāma كاتب العلامة yaani karani na mwandishi aliyetoa amri na matangazo rasmi yasultani kwa maandishi mazuri. 1357 alitupwa jela kwa miezi 22 hadi sultani alikufa na mfuasi wake alimrudishia cheo chake. Alipanda ngazi hadi kuwa katibu mkuu wa mtawala. Sultani huyu alipopinduliwa aliondoka Tunis akaenda Granada ya Andalusia alipopokelewa vema na amiriMuhammad V aliyemfanya balozi wake kwa mfalme Mkristo waKastiliaPedro I akafaulu kupatana na mfalme a kupata mkataba wa mani kati ya Kastilia na Granada. Baada ya kurudi Granada alionewa mafanikio yake na waziri wa amiri akapaswa kuondoka tena akarudu Afrika ya Kaskazini.
Hapa alitumikia watawala mbalimbali wa madola madogo ya Kiislamu katika eneo laAlgeria ya leo. Baada ya kuchoka siasa akaenda kuishi katika eneo laWaberber waliojitegemea akaanza kuandika kitabu cha historia ya dunia kati ya 1374–1377. Lakini hapa porini alikosa vitabu vya marejeo alivyohitaji kwa kazi yake akahamia tena Tunis.
Sultani mpya wa Tunis alimwajiri lakini Ibn Khaldun alikuwa na wasiwasi juu ya siasa zake akaomba rukhsa ya kwendahajj ya Maka kama mbinu wa kuondoka Tunis akapanda jahazi ya kwendaAleksandria katika Misri.
Misri ilikuwa dola tulivu iliyokuwa na kipindi cha tawala imara na maendeleo ya kiuchumi chini ya nasaba yaMamaluki. Tena Aleksandria ilikuwa kitovu cha elimu na hapa aliendelea na masomo na utafiti wake. Lakini hata hapo alishindwa kukaa mbali na siasa kwa sababu mwaka 1384 sultani Barkuk alimteua kama profesa wa fiq-hi naqadi mkuu kwa dhehebu lamaliki. Majaribio yake ya kuleta matengenezo katika fiq-hi jinsi Wamisri walivyozoe yaligonga ukuta aliona upinzani na kujiuzulu bada ya mwaka mmoja pekee.
Hapo aliamua kutekeleza nia ya awali akaenda kuhiji Maka. Baada ya kurudi kutoka Maka akaendelea kufundisha kwenye vyuo vya Aleksandria akarudishwa tena kama qadi kwa Wamaliki; alirudia kujiuzlu akarudishwa tena mara kadhaa kutokana na sifa zake za utaalamu katika cheo ambacho hakupenda.
Mwaka 1401 aliamriwa kushiriki katika vita ya sultani mpyaal-Nasir Faraj dhidi yaWamongolia chini yaTamerlan hukoSyria kama mshauri wa mtawala. MjiniDameski Ibn Khaldun alijikuta akifungwa ndani ya mji ulioshambuliwa na jeshi la Tamerlan. Ibn Khaldun aliteuliwa na watu wa Dameski kwenda kama mbalozi wao mbele ya mtawala wa Wamongolia na kuomba radhi kwa mji. Hapa alikutana mara kadhaa na Tamerlan na kujadiliana naye juu ya mengi akaokoa mji mbele ya hasira yake.
1401 aliweza kurudi Misri alipoandika taarifa ndefu juu ya Wamongolia akaendelea kukamilisha vitabu vyake juu ya maisha yake mwenyewe na juu ya historia ya dunia.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuIbn Khaldun kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.