Baada ya kushindwa naWajerumani mwaka955 walibaki katika makazi yao na mnamo mwaka1000 mfalme Ishtvan (Stefano wa Hungaria) alipokeaubatizo akaongoza taifa lake kuingia katikaUkristo.
Wakati wauvamizi waWamongolia baada yaChingis Khan katikakarne ya 13 nchi iliangamizwa, na nusu ya wakazi wakauawa.
Baadaye wafalme Wahungaria waliwakaribishawalowezi kutokaUjerumani walioanzisha vijiji vingi na pia miji.
Wakati wakarne ya 15WaturukiWaosmani walianza kuenea kwenye Balkani, wakaingia katika Hungaria kutoka upande wa mashariki. Katikamapigano ya Mohacs mwaka1526 Hungaria ilishindwa na sehemu kubwa ikawa chini ya Waosmani. Magharibi ya nchi ikaendelea kuitwaufalme wa Hungaria lakini ufalme uliingia mikononi mwa nyumba yaHabsburg yaani chini ya watawala waAustria.
Katika karne zilizofuata watawala wa Habsburg walirudisha Waosmani nyuma na ufalme wa Hungaria ukawa sehemu ya milki ya Habsburg yaani Austria.
Katikakarne ya 19 mnamo1848 Wahungaria waliasi dhidi ya watawala lakini walishindwa. Hata hivyoKaisariFranz Joseph I alibadilishasiasa yake akatafuta usaidizi wa Wahungaria katika utawala wa ufalme. Katiba mpya iliunda cheo cha sawa kati ya Austria na Hungaria chini ya mtawala yeye yule mwenye vyeo vya Kaisari wa Austria na Mfalme wa Hungaria na milki ikaitwa "Austria-Hungaria".
Austria-Hungaria ilikuwa milki kubwa katika Ulaya ya Kati na Mashariki kuanzia mwaka1867 hadi1918.