Hong Kong (Kichina: 香港; pinyin: Xiānggǎng) niMkoa Maalum wa Utawala (SAR) wa China. Upo kusini mwa pwani ya nchi, kando yaBahari ya Kusini ya China. Inajumuisha Kisiwa cha Hong Kong, Rasi ya Kowloon, na New Territories. Jiji la Hong Kong, lililopo kwenye Kisiwa cha Hong Kong, ndilo jiji kubwa na idadi ya watu katika mkoa.Hong Kong lina takriban milioni 7.5 katika eneo la kilomita za mraba 1,110
Hong Kong ilikuwakoloni laUingereza katika pwani ya China kwa zaidi ya miaka 99. Hong Kong ilirudishwa kwaChina kutoka Uingereza mnamo Julai 1, 1997, chini ya makubaliano ya "nchi moja, mifumo miwili," ikiruhusu Hong Kong kudumisha uhuru wake wa kisiasa na kiuchumi kwa miaka 50. Hata hivyo, kwa muda, China imeongeza udhibiti wake, hasa kupitia maandamano ya kupinga muswada wa kukabidhi wahalifu wa 2019 na Sheria ya Usalama ya Kitaifa ya 2020, ambayo ilipunguza uhuru na haki za Hong Kong.
Kuelekea mwishoni mwamiaka ya 1970, Hong Kong ikawa imara kama mlango mkuu kati yadunia nzima na China.
Kama matokeo yamazungumzo kati ya China na Uingereza, Hong Kong ilirudishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China chini ya Azimio la Pamoja la mwaka1984. Mji ukawa wa kwanza kati ya Mikoa yenye utawala maalumu nchini China tarehe1 Julai 1997 chini ya kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili". Siku hiyo inaitwa 香港回歸 (xiāng gǎng huí guī), kwa Kiswahili "unganisho jipya la Hong Kong". Jina lingine ni 香港回歸祖國 (xiāng gǎng huí guī zǔ guó), kwa Kiswahili "Hong Kong kurudishwa kwa nchi mama".
Hong Kong ni maalumu kwa ajili ya mandhari yake pana,bandari asili yakina namsongamano wa watu (milioni saba na nusu juu ya nchi yaKm² 1108 (sq mi 428).
Sehemu kubwa ya wakazi wanazungumza Kichina cha Canton (Kikantoni), Hong Kong ikiwa jirani na jimbo la Guangdong, ambalowafanyakazi wenyeujuzi walikimbia baada ya serikali yaKikomunisti kuchukua China mwaka1949 na baadaye husafishwa idadi ya watu mwaka1960.
Mji wa kumi kwakipato cha juu cha kila mwananchi katika dunia, lakini pia inaongozaongoza miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa kwa kukosa usawa wa kipato cha wakazi.
Hong Kong ni ya tatu kama kituo cha biashara muhimu zaidi baada ya New York na London. Huduma uchumi, kwakodi ya chini nabiashara huria, imekuwa huru sana, nafedha yake,dola ya Hong Kong, ni ya 13 kutumika zaidi duniani.
Udogo wa eneo ulileta haja ya miundombinu mingi jirani, na mji ukawa katikati ya vielelezo vyausanifu wa kisasa upande wa majengo, na kuipa Hong Kongmandhari ya mji unaoelekea juu wima.
Hong Kong ina maendeleo makubwa hata upande wausafiri wa umma duniani ukiwa na mtandao wa asilimia 90, kiwango cha juu zaidi duniani, na inategemea wingi wa watu kupita kwa njia yabarabara aureli.
Ingawa Hong Kong ina watu wengi wamatabaka mbalimbali, chakula kwa kawaida huwa kimetokana na utamaduni wa Cantonese au Guangdong cuisine.Wali huliwa kwa wingi pamoja nakuku namboga zilizotokamashambani. Chakula huliwa maratano kwa siku yaani:staftahi, chakula chamchana,chai yaadhuhuri, chakula chajioni nasiu yeh ambacho ni chakula cha kuliwa kabla uende ukalale.
Mambo ya kuona Hong Kong ni kama vileKisiwa chaLantau ambapo kivutio kikubwa niGiant Buddha,mchongo ulio mkubwa sana waBuddha, The Peak ambapo utaona Victoria Harbour, Hong Kong Disney Land Resort na Ocean Park Theme.
1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaChina bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuHong Kong kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.