Mara nyingi homa husababishwa naugonjwa; nidalili ya kwambakingamwili inapambana navijidudu auvijimea vinavyosababisha ugonjwa fulani.
Homa si ugonjwa wenyewe bali dalili ya magonjwa mbalimbali. Katikalugha ya kilasikumalaria mara nyingi huitwa "homa" ingawa kupanda kwa halijoto ya mwili wakati wa malaria ni dalili ya mapambano dhidi ya vijidudu vyaplasmodium tu. KatikaKenya "homa" hutumiwa kumaanisha mafua,mafua ya kawaida hasa.
Hadi kiwango cha sentigredi 39 homa sihatari sana, lakini ikipanda juu ya 40°C inaanza kudhoofishaumbile lamtu hadi kuwa hatari yenyewe.
Inashauriwa kumwonadaktari na kutumiamadawa ya kutuliza homa. Kufikia 42°C homa inaweza kumwua mtu kwa kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani vya mwili.