Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Holmi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Holmi(Holmium)

Jina la Elementi
Holmi(Holmium)
AlamaHo
Namba atomia67
Mfululizo safuLanthanidi
Uzani atomia164.930
Valensi2, 8, 18, 29, 8, 2
Densiti8.79 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka°K 1734
Kiwango cha kuchemka°K 2873

Holmi(Holmium) nielementi yakimetali yenyealamaHo nanamba atomia 67, maana yakekiini cha Holmi kinaprotoni 67 ndani yake.Uzani atomia ni 164.930[1]. Katikajedwali la elementi inahesabiwa kati yalanthanidi na metali zaardhi adimu.

Holmi ilitambuliwa kama elementi ya pekee nchiniUswidi namwanakemiaPer Theodor Cleve kwenyemwaka1878. Aliikuta kama taka ndani yaoksidi yaErbi, pamoja naThuli. Cleve alichaguajina la Holmi kwa heshima yamjiStockholm alikozaliwa.[2][3][4]

Holmi safi ni metali laini. Kiasili Holmi haipatikani kwa hali safi kwa sababu inatendana kirahisi nakemikali nyingine. Lakini inapatikana ndani yamadinimonaziti nagadoliniti.[5] Maeneo makuu ya madini niChina,Marekani,Brazil,Uhindi,Sri Lanka, naAustralia naakiba ya holmi inakadiriwa kuwatani 400,000.[6]

Baada ya kusafishwa inakaa katikahewa kavu kwahalijoto ya kawaida. Ikifikianyuzijoto°C 150 inawaka.

Holmi huwa na nguvu kubwa yausumaku, na hapo inapita elementi zote nyingine. Kwa sababu hiyo hutumiwa kuzalisha sumaku zenye nguvu kuu.[7]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Meija, Juris; et al. (2016). "Atomic weights of the elements 2013 (IUPAC Technical Report)". Pure and Applied Chemistry. 88 (3): 265–91. doi:10.1515/pac-2015-0305
  2. Marshall, James L. Marshall; Marshall, Virginia R. Marshall (2015)."Rediscovery of the elements: The Rare Earths–The Confusing Years"(PDF).The Hexagon: 72–77. Iliwekwa mnamo30 Desemba 2019.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Holmium".Royal Society of Chemistry. 2020. Iliwekwa mnamo4 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Stwertka, Albert (1998).A guide to the elements (tol. la 2nd). Oxford University Press. uk. 161.ISBN 0-19-508083-1.
  5. Hudson Institute of Mineralogy (1993–2018)."Mindat.org".www.mindat.org. Iliwekwa mnamo14 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. John Emsley (2001).Nature's building blocks: an A-Z guide to the elements. US: Oxford University Press. ku. 181–182.ISBN 0-19-850341-5.
  7. R. W. Hoard; S. C. Mance; R. L. Leber; E. N. Dalder; M. R. Chaplin; K. Blair; D. H. Nelson; D. A. Van Dyke (1985)."Field enhancement of a 12.5-T magnet using holmium poles".IEEE Transactions on Magnetics.21 (2): 448–450.Bibcode:1985ITM....21..448H.doi:10.1109/tmag.1985.1063692.{{cite journal}}:Unknown parameter|displayauthors= ignored (|display-authors= suggested) (help)

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuHolmi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Holmi&oldid=1152175"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp