Historia ya Pakistan inahusu eneo ambalo leo linaundajamhuri yaKiislamu yaPakistan.
Binadamu walifikaBara Hindi kutokaAfrika kabla ya miaka 55,000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kamawawindaji-wakusanyaji waliozagaabarani, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande waurithi wa kibiolojia, ambayo inapitwa na Waafrika tu.
Makazi ya kudumu yalianzamagharibi, katikabeseni lamto Indus, miaka 9,000 iliyopita, hata kuzaaustaarabu maalumu (Indus Valley Civilisation) katikamilenia ya 3 KK.
Kufikiamwaka1200 KK,Kisanskrit cha Kale, mojawapo kati yalugha za Kihindi-Kiulaya, kilikuwa kimeenea India kutokaKaskazini-Magharibi, kikawalugha yaRigveda, mwanzoni mwadini yaUhindu. Hivyolugha za Kidravidi zikakoma kaskazini.
Kufikia mwaka400 KK,matabaka ya kudumu katikajamii yalikuwa yamejitokeza katika Uhindu. Hapo dini zaUbuddha naUjaini zilitokea, zikipinga taratibu hizo za kibaguzi.
Katikarne za kwanza baada yaKristo, dini zaUkristo,Uislamu,Uyahudi naUzoroastro pia zilitia mizizi katikajamii.
Majeshi kutokaAsia ya Kati yalivamia kwakwikwi mabonde ya India, hata kuundausultani waDelhi na kuingiza India Kaskazini katikaumma wa Kiislamu.
Pakistan ilikuwa sehemu yaUhindi wa Kiingereza hadimwaka1947.
Mwaka1857Wahindi walipingautawala waKampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa naserikali yenyewe yaUingereza kamakoloni (1858).
Mwisho wakarne ya 19harakati za Wahindi kutafutauhuru zilianza upya. Mwaka1885chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa naWahindu naWaislamu pamoja waliodai uhuru.
Mwaka1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".
Mwaka1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini yauongozi waMahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasaumoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenyeitikadi kali wa pande zote mbili.
Baada yaVita Vikuu vya Pili vya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Tarehe 14/15 Agosti1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili zaUhindi na Pakistan.Mgawanyo wa Uhindi ulikuja navita na kumwaga kwadamu nyingi.
Tarehe30 Januari1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Mhindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitakausawa wa Waislamu na Wahindu.
Wakati ule ilikuwa nchi moja pamoja naBangla Desh ya leo, lakini mwaka1971 hizo pande mbili zilitengana baada yavita kati yao.
 | Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuHistoria ya Pakistan kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |