Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Hidrojeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Hidrojeni (Hydrogenium)
Jina la ElementiHidrojeni (Hydrogenium)
AlamaH
Namba atomia1
Mfululizo safuSimetali
Uzani atomia1.00794
Valensi1
Densiti2700kg/m3
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka14.02K (−259.12°C)
Kiwango cha kuchemka20.27 K (−252,88 °C)
Asilimia zaganda la dunia0.88

Hidrojeni (kwaKiingereza:hydrogen) nielementi yakikemia yenyenamba atomia 1 nauzani wa atomi 1.00794.Alama yake niH. Niatomi nyepesi zaidi kati ya elementi zote, hivyo ina nafasi ya kwanza katikamfumo radidia.

Mtihani wa wigo wa hidrojeni

Hidrojeni ni elementi inayopatikana kwa wingi kabisaulimwenguni lakini siduniani. Iko ndani yamaji na katikamolekuli zote zamaadahai.

Muundo wa atomi

[hariri |hariri chanzo]

Atomi za H zinaelektroni moja tu inayozungukakiini cha atomi. Hidrojeni ya kawaida inaprotoni moja tu. Hii ni zaidi yaasilimia 98 yaisotopi zote za hidrojeni. Kuna pia isotopi yenyenyutroni moja au mbili katikakiini lakini zinatokea mara chache tu.

Kuna isotopi mbili zinazoitwaDuteri(deuterium) naTriti(tritium).

Kupatikana kwake ulimwenguni

[hariri |hariri chanzo]

Duniani kwa kawaida hakuna hidrojeni ya atomi mojamoja hutokea kamagesi yenye molekuli za H2.

Masi yajua letu ni hasa hidrojeni lakini pia sehemu kubwa ya masi zasayari kubwa yaaniMshtarii,Zohali,Uranus naNeptun. Kwa jumla asilimia 93 za atomi zote na asilimia ya masi katikamfumo wa jua letu ni H.

  • Muundo wa atomi ya hidrojeni. Elektroni yenye chaji ya hasi yazunguka kiini chenye chaji ya chanja. Kiini cha kawaida kina protoni moja to; ni isotopi ya kudumu ya pekee kati ya elementi zote isiyo na nyutroni.
    Muundo wa atomi ya hidrojeni. Elektroni yenye chaji ya hasi yazunguka kiini chenye chaji ya chanja. Kiini cha kawaida kina protoni moja to; ni isotopi ya kudumu ya pekee kati ya elementi zote isiyo na nyutroni.

Matumizi

[hariri |hariri chanzo]

Kiasi kikubwa cha hidrojeni hutumika katika:

  • viwanda vya kusafisha mafuta kwa ajili ya hidrodesulfurinaztion[1][2], hidrodealkylation,hidroisomerization
  • usanisi wa methanoli na amonia
  • hidrojeni ya michanganyiko ya kikaboni isiyoshiba

Hidrojeni kwa ajili ya michakato hii hutengenezwa kila wakati mahali hapo, kwa kupasuka kwa mvuke na gesi asilia. Hidrojeni mbadala inaweza kutengenezwa kwa kutumia maji kwa kutumia nishati ya jua na upepo. Kwa sababu ya eneo lake la kijiografia, Afrika ina uwezo mzuri wa kuzalisha hidrojeni mbadala na amonia ili kupunguza utegemezi wake kwa uagizaji wa mbolea;[3][4].

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Gheorghe, Catalina Gabriela; Dragomir, Raluca-Elena (2025-10-01)."Optimization of diesel fuel quality and production by hydrotreated gasoil mixtures using Co-Mo/γAl2O3 catalysts".Reaction Kinetics, Mechanisms and Catalysis (kwa Kiingereza).138 (5): 2759–2776.doi:10.1007/s11144-025-02913-0.ISSN 1878-5204.
  2. Linares, Carlos F.; Brunet, Sylvette (2023-02)."Hydrodesulfurization of dibenzothiophene on Ni–Co alloy boride catalysts supported on alumina".Reaction Kinetics, Mechanisms and Catalysis (kwa Kiingereza).136 (1): 47–68.doi:10.1007/s11144-023-02356-5.ISSN 1878-5190.{{cite journal}}:Check date values in:|date= (help)
  3. Skills development workshop for hydrogen and ammoniahttps://www.igb.fraunhofer.de/en/reference-projects/ptx-skills-development-in-tunisia.html;
  4. Green Ammonia – Production of green ammonia in Moroccohttps://www.igb.fraunhofer.de/en/reference-projects/green-ammonia.html
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuHidrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Hidrojeni&oldid=1484590"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp