Haiti, rasmi kamaJamhuri ya Haiti, ni nchi iliyoko katika Karibi, inayochukua theluthi ya magharibi ya kisiwa chaHispaniola. Inapakana naBahari ya Karibi naBahari ya Atlantiki, na inapakana naJamhuri ya Dominika. Ina idadi ya watu takriban milioni 11.7, ikiwa ya 81 duniani. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi niPort-au-Prince. Haiti imegawanyika katika mikoa 10 ya kiutawala. Inajulikana kwa kuwa nchi ya kwanza ya watu weusi kupata uhuru mwaka 1804 baada ya mapinduzi dhidi ya utawala waKifaransa, na kwahistoria yake tajiri yakiutamaduni, pamoja na changamoto zakisiasa na za majanga ya asili kama vile matetemeko ya ardhi.
Haiti inahistoria ya kipekee inayohusisha mapambano ya muda mrefu yauhuru,ukoloni, na mabadiliko yakijamii. Baada ya kuongoza mapinduzi ya watumwa yaliyofanikiwa dhidi yaUfaransa, Haiti ikawataifa la kwanza lawatu weusi kujitawala, jambo lililokuwa na athari kubwaduniani kote. Hata hivyo, tangu wakati huo nchi imekumbwa na mfululizo wa matatizo yakisiasa, mapinduzi ya kijeshi, na ukosefu wa uthabiti waserikali, hali ambayo imeathiri maendeleo yakijamii nakiuchumi.
Katikakarne ya 21, Haiti imekumbwa na majanga kadhaa ya asili, ikiwa ni pamoja na tetemeko kubwa la ardhi la mwaka 2010 lililosababishavifo vya zaidi ya watu 200,000 na kuacha mamilioni bila makazi. Mifumo yaafya,elimu namiundombinu imeendelea kuwa dhaifu, hukuuchumi ukitegemea misaada ya kimataifa, uhamishaji wa fedha kutoka kwa watu waishio nje ya nchi, na sekta ndogo yakilimo. Licha ya hayo, watu wa Haiti wanaonyesha uthabiti mkubwa, wakihifadhi tamaduni zao tajiri,muziki,sanaa, na lugha yao yaKrioli ya Haiti.
Katikakarne ya 17Wafaransa walifikakisiwani wakanunuatheluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujengauchumi wa mashamba makubwa, hasa yamiwa.Koloni la Saint-Domingue lilikuwa koloni tajiri la Ufaransa katikaAmerika.
Wazungu, hasa Wafaransa, waliokuwa mabwana lakini walikuwa na tofauti kubwa kati yao: wenginetajiri sana wenginemaskini - jumla takriban watu 32,000
machotara na Weusi huru ambao walikuwaraia wa daraja ya pili; wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa - jumla watu 28,000
watumwa wenye asili ya Kiafrika - jumla watu 500,000
Wamaroni walikuwa watumwawakimbizi walioishimlimani katikapori - idadi yao haijulikani lakini hawakuwa wengi.
Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwahaki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya machotara wenyemali ya kukubaliwa kama raia kamili wenyehaki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.
Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada waUingereza na Hispania wakichukiamapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na Weusi huru wenyeelimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hao bilasheria za Ufaransa utakuwa mbaya kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza mapinduzi.
Kiongozi wao alikuwaToussaint L'Ouverture aliyefaulu kushikaserikali ya koloni tangu mwaka1798. Awali alipiganiajeshi la Ufaransa; baada yabunge laParis kutangaza mwisho wa utumwa alishirikiana na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye mashamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.
Toussaint L'Ouverture alishinda piaWaingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa waParis na mwaka1801 akatekakaskazini mwa kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawalaHispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.
Lakini mnamo mwaka1802siasa ya Paris ilibadilika na mtawalaNapoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola katika hali ya awali akatuma jeshi kubwa laaskari 40,000. L'Ouverture alikamatwa alipokubali kushauriana najenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakinimakamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia kuhusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianzavita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Dessalines alitangazauhuru wa koloni tarehe1 Januari1804 kwajina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi".
Makala hii kuhusu maeneo yaBahari ya Karibi bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuHaiti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.