Gukurahundi nineno lalugha yaKishona linalozungumzwa nchiniZimbabwe linalomaanisha "kufyeka, kusafisha".
Neno hilo lilitumiwa pia kisasa katikahistoria yachama chaZANU kwa kumaanisha takaso la kisiasa ambakokada wa chama waliotazamwa hawakubali na uongozi waliondolewamadarakani na wakati mwingine kuuawa.
Baada yauhuru wa Zimbabwemwaka1980 kulikuwa na hali ya kutoelewana baina ya wafuasi wa vyama vilivyowahi kupigania uhuru, ZANU naZAPU. Vyote viwili vilikuwa naasili moja, ila vilifarakana kuhusu mbinu za kupambana nautawala wakikoloni. Tofauti za kisiasa ziliongezewa ukali na tofauti zakabila maana kada wengi wa ZANU walikuwaWashona ilhaliZAPU chini yaJoshua Nkomo ilikuwa hasa naWandebele.
Waziri mkuuRobert Mugabe wa ZANU alihofiaupinzani upande wa ZAPU, hivyo aliandaa kikosi cha pekee katikajeshi jipya la Zimbabwe lililokuwa maarufu kama Brigedi ya Tano lililofundishwa na walimu wa kijeshi kutokaKorea Kaskazini. Mugabu alituma brigedi hiyo mwaka1982 katika nchi ya Wandebele ili watafute kada za ZAPU na jeshi lakeZIPRA. Katika kampeni hiyo watu 20,000 waliuawa hovyo. Nkomo alikimbiliaUingereza.
Baada ya mapatano ya amani na maungano ya vyama vya ZANU na ZAPU kwenye mwaka1987mauaji ya Gukurahundi yalichunguliwa lakini matokeo ya utafiti yalifichwa.
Baada ya kupinduliwa kwa Mugabe mwaka2019rais mpyaEmmerson Mnangagwa alitangaza majadiliano ya kitaifa kuhusu kipindi cha Gukurahindi[1]. Makaburi ya makundi ya wakati ule yamefunguliwa na maiti kuzikwa upya[2].
![]() | Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuGukurahundi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |