Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Grigori Rasputin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Rasputin.

Grigori Yefimovich Rasputin (kwaKirusi: Григо́рий Ефи́мович Распу́тин,22 Januari1869 -30 Desemba1916) alikuwamkulima na mponyaji waimani waUrusi.[1] Hakuwamtawa aliyeishi katikanyumba ya watawa, bali ni mhiji wa kidini. Alianza kupata sifa kama "mtumtakatifu" katikamazingira yaSiberia akaendelea kuwarafiki wa wakuu waKanisa la Kiorthodoksi.

Mnamo1904 alifika katikamji mkuu waSankt Peterburg akakutana na wakuu wa jamii, watu kutokatabaka lamakabaila. Hatimaye aliweza kukutana hata naTsar (mfalme)Nikolai II namalkia wakeAleksandra. Walimwomba amwombeemtoto waoAleksei aliyekuwa naugonjwa wahemofilia (ugonjwa wa kutokwadamu; ulisababishamaumivu kwenyekinena namiguu kila alipoanguka) wakaona mtoto alipata nafuu akiombewa na Rasputin. Hivyo alifika kwenye nafasi ya kuwa mshauri wa kiroho kwa tsar namke wake.[2] Malkia Aleksandra aliamini kwamba Rasputin ndiye mtu pekee ambaye anaweza kumponya mtoto wake kwa maombi yake.

Kwa sababu hiyo, Tsar nafamilia yake walianza kumwamini Rasputin zaidi na maamuzi muhimu juu yasiasa. Rasputin hakuunga mkono Tsar alipoamua kuiongoza nchi yake katikaVita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mnamo Agosti1915, Tsar aliamua kuongozajeshi la nchi mwenyewe, na kuchukua nafasi yabinamu yake Mtemi Nikolai.Wanasiasa wengi wa Urusi na wakuu walipata wasiwasi sana juu ya ushawishi mkubwa wa Rasputin. Wakati Tsar alikuwa pamoja na wanajeshi wake, Alexandra na Rasputin walichukua maamuzi yaliyoongeza wasiwasi katikaserikali. Walipendekeza kwa Tsar kubadilishamawaziri kadhaa na kuteua wengine waliounga mkonoamani.

Hivyo wapinzani wa Rasputin waliamua kumwondoa katika mazingira ya tsar kwa kumwua.

Usiku wa Desemba 30, 1916, Rasputin alipigwarisasi mara mbili na Felix Yusupov aliyekuwakijana wa familia ya tsar. Wauaji walimtupa katikamto Neva mjini Sankt Peterburg.[3]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Maria Aprelenko (2011)."Prominent Russians: Grigory Rasputin". Russiapedia. Iliwekwa mnamo16 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. http://russiapedia.rt.com/prominent-russians/history-and-mythology/grigory-rasputinIlihifadhiwa 13 Novemba 2021 kwenyeWayback Machine. Prominent Russians: Grigory Rasputin
  3. http://russiapedia.rt.com/prominent-russians/history-and-mythology/grigory-rasputinIlihifadhiwa 13 Novemba 2021 kwenyeWayback Machine. Prominent Russians: Grigory Rasputin
Picha ya Grigori Rasputin (1910).
Makala hii bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Grigori_Rasputin&oldid=1205669"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp