Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Gregori wa Nisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Gregori wa Nisa
(picha ya ukutani wakarne ya 14t,Chora Church,Istanbul,Uturuki.)

Gregori wa Nisa (Neocaesarea,335Nisa,395) alikuwaaskofu wa Nisa miaka372 -376, halafu378 hadikifo chake.

Gregori, pamoja na kaka yakeBasili Mkuu na rafiki yaoGregori wa Nazianzo wanatajwa kamaMababu wa Kapadokia.

Gregori hakuwa na kipaji cha uongozi cha kaka yake Basili, wala hakuathiriKanisa kama Gregori wa Nazianzo, lakini alikuwa naakili naelimu kubwa zilizomwezesha kuchangia sanateolojia kuhusuUtatu namaisha ya kiroho. Kwa sababu ya kushikaimani sahihi,kaisariValens, mfuasi waArio, alimfukuzajimboni[1].

Anaheshimiwa kamamtakatifu naKanisa Katoliki,Waorthodoksi,Waorthodoksi wa Mashariki,Walutheri naWaanglikana siku tofautitofauti.

KatikaKanisa la Kilatini nitarehe10 Januari[2].

Sala yake

[hariri |hariri chanzo]

Ee Mchungaji mwema, unakwenda wapi kuchunga,wewe unayebeba mabegani kundi lako lote?

Kwa kuwakondoo yule pekeeanawakilisha ubinadamu wote uliobeba mabegani mwako.

Unionyeshe mahali pa pumziko,unifikishe kwenye majani mema ya kunilisha,uniite kwa jina, ili mimi pia, niliye kondoo, niweze kusikia sauti yakona kwa hiyo niweze kupatauzima wa milele:“Unionyeshe mpenzi wa roho yangu”.

Ndivyo ninavyokuita, kwa kuwa jina lako liko juu ya kila jina na uelewa,wala ulimwengu wote wa viumbe wenye akili hauwezi kulitaja nakulielewa.

Basi, jina lako, ambamo wema wako unajitokeza,unawakilisha upendo wa roho yangu kwako.

Kwa kuwa ningewezaje kutokupenda, baada ya wewe kunipenda mno?Ulinipenda hivi hata ukatoa uhai wako kwa kundi la malisho yako.

Haiwezekani kufikiria upendo mkuu kuliko huo.Umelipa wokovu wangu kwa uhai wako.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Maandishi yake

[hariri |hariri chanzo]
De virginitate

Maandishi yake yote katikalugha asili yaKigiriki pamoja na ufafanuzi wa Kilatini yanapatikana katika mfululizoGregorii Nysseni Opera:

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo mengine

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Gregori_wa_Nisa&oldid=1371203"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp