Google Play ni jukwaa la kujipatia programu au apps zamfumo wa uendeshaji waGoogleAndroid. Ni duka la mtandaoni kwa ajili ya muziki, vitabu, filamu na progamu zote za Android.
Mnamo tarehe 7 Machi, 2012, Google walitangaza ya kwamba wataziweka huduma hizi zote 4 katika sehemu moja, Google Play.
Programu zilizoko katika Google play huwa za kulipa ama za kuchukua bure. Programu hizi huweza kupakuliwa kwa simu au kifaa kinachotumia mfumo wa Android kama vile Tablet.
Kupata programu au vipengele vilivyotajwa hapo juu, mtumiaji afaa kulipa kwa kutumia njia zifuatazo:
Paypal au malipo kwa kutumia kadi ya debit au ya mikopo (credit card)
Gift cards: Kutoka mwaka wa 2012 kulikokuwa na fununu kuwa kuna Google play gift cards, kampuni ya Google iliamua kuweka hizi gift cards kirasmi. Kwa sasa, waweza kupata gift cards kwa zaidi ya nchi 20.
Subscriptions: Pia kuna kulipa kwa subscriptions ambapo mtumiaji apata kutumia programu kwa mwezi au wakati fulani hadi wakati ule uishe alipe tena
Makala hii kuhusu mambo yateknolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.