Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Global Positioning System

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Satelaiti za GPS zinazozunguka Dunia; rangi ya buluu inaonyesha kupatikana kwa satelaiti kwa kipokeaji kwenye kaskazini ya Dunia, rangi nyekundu inaonyesha satelaiti zinazopotea nyuma ya upeo ambako hazipokelewi tena na kipokeaji

Global Positioning System (kifupi:GPS, maana yake:Mfumo wa uongozaji kote duniani) ni mfumo wa Marekani wa kupima na kutambua kwa makini kila mahaliduniani ukitumiasatelaiti. Nimfumo wa uongozaji kwa satelaiti unaotumika zaidi duniani.

Misingi

Satelaiti kama 30 zinazunguka Duniamuda wote kwenyenjia maalum katikaanga-nje ya karibu. Zinakaakilomita 20,000 - 25,000 juu ya uso wa ardhi na kutumiasaa 12 hivi kuzunguka Dunia. Zinatuma muda woteishara zaredio duniani. Kipokeaji duniani kinapokea ishara hizo.Majiranukta za mahali pa satelaiti hujulikana kwa kiladakika na kilasekunde, maana zinafuata njia thabiti. Kipokeaji kikiwa na ishara redio za angalau satelaititatu kinaweza kukadiria majiranukta ya mahali pake penyewe kwa umakini. Kama kipokeaji kinapata ishara ya satelaiti nyingi zaidi umakini huongezeka.

Hali halisi umakini wa GPS unategemeakifaa ulichonacho. Kama si vizuri tofauti zamita 100 zinaweza kuonyeshwa. Matumizi katika mazingira yamajengo marefu, ndani ya majengo au penyemilima mikali inaathiri umakini pia kwa sababu vizuizi hivyo vinaweza kuzuia ishara ya satelaitimoja au zaidi.

Vifaa vya GPS havihitajiintaneti kwa sababu ishararedio za satelaiti zinapokewa moja kwa moja. Hata hivyo vifaa vingi hutumia intaneti pia kwa kuboresha huduma.

Mwongozo wa safari

Kifaa cha GPS kwenye gari kinaonyesha ramani pamoja na njia ya kuelekea

Vipokezi vya GPS vinapatikana katikasimujanja na vifaa vingine vinavyotumiwa katikamagari,eropleni nameli. Vifaa hivyo ni kamakompyuta ndogo ambayo inatumia piaramani ya nchi au Dunia pamoja na habari zabarabara na hali zake. Kwa njia hiyoprogramu za GPS zinazounganishwa na kipokeaji huonyesha mahali pa mtumiaji kwenye ramani. Inaweza kukadiria muda unaohitajika kufika kutoka mahali ulipo hadi mahali pengine ama kwamiguu au kwa gari kwa kutumiakasi yawastani. Pale ambakoratiba zausafiri wa umma zinapatikana kifaa kinaonyesha pia muda wausafiri kwatreni aubasi. Ilhali majiranukta ya kifaa chenyewe kinajulikana muda wote, ni lazima kupata majiranukta ya mahali unapolenga. Hapa mtumiaji anaweza kudokeza kwenye ramani anapoenda au kuingizaanwani kamili maana programu za GPS huwa nadata nyingi zenyemajina na majiranukta za barabara,mitaa na hata majengo maalumu.

Mifumo mbalimbali ya GPS

Marekani ilikuwa nchi ya kwanza iliyopeleka satelaiti za GPSangani na mwanzoni shabaha lilikuwa la kijeshi. Baadayekampuni za kiraia ziliruhusiwa pia kutumia data na ishara za redio kutoka satelaiti zinazopatikana sasa kwa kila mtu mwenye kifaa. Mfumo wa Marekani unaitwa "NAVSTAR GPS", upo tangumwaka1985 na tangu mwaka2000 umepatikana pia kwa watumiaji raia. Lakini ishara zake hazipatikani kwa umakini mkuu kwa vifaa vya watu raia ambao huchezacheza kwa mita 10 hivi. Kwa vifaa vya kijeshi vya Marekani umakini unafikiasentimita ambao ni muhimu kwa kulengeshasilaha.

Nchi nyingine zimejenga pia mifumo yao kwa sababu hawataki kutegemea GPS ya Marekani inayoweza kuzimishwa muda wowote. Hivyo kuna mifumo ifuatayo:

Kila mfumo unatumia satelaiti zake za pekee angalau 24, hadi 32. Jina laKiingereza kwa jumla ya mifumo hii ni "global navigation satellite system " (GNSS) lakini jina la GPS limekuwa kawaida katika nchi nyingi kwa zote.

Viungo vya Nje

Habari za mifumo tofauti

Mamlaka na shirika zinazohusiana na huduma za GPS

Tovuti zenye maelezo ya teknolojia husika

Makala hii kuhusu mambo yateknolojia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Global_Positioning_System&oldid=1218930"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp