Kabonati ya kalisi inatengenzwa naviumbehai vinavyojenga kiunzi cha kujikinga au kuimarisha miili yao, kama kiunzi chamatumbawe ausifonji, lakini piakiunzi cha mifupa ya wanyama wakubwa. Matumbawe hujenga matabaka manene ya mwamba chokaa, mabaki ya viumbe vingine katika maji hutiririka chini ambako yanajenga matabaka ya kalsiti inayokandamizwa na shinikizo ya mata inayokaa juu yake, jinsi ilivyo na mwamba mashapo wote.
Matabaka ya gange yalitokea chini yabahari katika muda wa kiaka mamilioni hata mabilioni. Yalikua hadi kuwa na unene wa kilomita kadhaa. Gange ni takriban silimia 10 ya miamba mashapo yote duniani.
Pale ambako gange iliathiriwa na joto na shinikizo kubwa sana imebadilika kuwamwamba metamofia, kwa mfanomarumaru.
Gange ni muhimu sana kwa jamii za binadamu kama kifaa chaujenzi. Gange si ngumu mno hivi iliwahi kukatwa tangu miaka mielfu na kutumiwa kwa majengo.Piramidi za Misri zilijengwa kwa kutumia gange.
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuGange kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.