Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Gamma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa1Ν ν Ni50
Β β Beta2Ξ ξ Ksi60
Γ γ Gamma3Ο ο Omikron70
Δ δ Delta4Π π Pai80
Ε ε Epsilon5Ρ ρ Rho100
Ζ ζ Dzeta7Σ σ ς Sigma200
Η η Eta8Τ τ Tau300
Θ θ Theta9Υ υ Ipsilon400
Ι ι Iota10Φ φ Phi500
Κ κ Kappa20Χ χ Khi600
Λλ Lambda30Ψ ψ Psi700
Μ μ Mi40Ω ω Omega800
Herufi za kihistoria1
Digamma6San90
Stigma6Koppa90
Heta8Sampi900
Yot10Sho900
1 Viungo vya nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_nje

Gamma ni herufi ya tatu katikaAlfabeti ya Kigiriki. InaandikwaΓ (herufi kubwa ya mwanzo) auγ (herufi ndogo ya kawaida). Zamani ilikuwa pia alama kwanamba3.

Asili ya gamma ni herufi yaKifinisia ya gimel (tazama makala ya G). Matamshi yake ni kamaG ya Kiswahili.

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katikahesabu nafizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya tatu katikapembetatu.

Katika fizikia gamma ni alama kwa fotoni hasa mnururisho mkali ainamiali ya gamma.

Katikaastronomia inatumiwa kuanza hesabu yanyota katikakundinyota. Katikamfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya tatu katika kundinyota fulani.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Gamma&oldid=1059826"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp