Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Fumbwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fumbwe
Dume la Fumbwe mkia-mrefu (manyoya ya majira ya kuzaa)
Dume laFumbwe mkia-mrefu (manyoya ya majira ya kuzaa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli:Aves (Ndege)
Oda:Passeriformes (Ndege kamashomoro)
Familia ya juu:Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia:Viduidae (Ndege walio na mnasaba nafumbwe)
Cabanis, 1841
Jenasi:Vidua
Stresemann, 1914
Ngazi za chini

Spishi 19:

Fumbwe nindege wadogo wajenasiVidua katikafamiliaViduidae ambao wanatokeaAfrika tu.Spishi bila mkia mrefu na yenye rangi yanili wanaitwakinili pia. Wakati wa kuzaa madume wana rangi ya nyeusi na nyeupe na pengine rangi nyingine au rangi ya nili tu, na spishi kadhaa zina mkia mrefu. Lakini wakati wengine wana rangi za majike, kahawia na nyeupe, wenye michirizi miwili kwa utosi, na mkia wao una urefu wa kawaida. Hulambegu zamanyasi hasa lakiniwadudu pia,kumbikumbi aghalabu.

Ndege hawa hawajengi tago lao lenyewe lakini huyatagamayai yao katika matago ya ndege wa familiaEstrildidae (udusio wa kiota, Kiing.brood parasitism). Kilaspishi inadusia spishi yake ya Estrildidae. Vinili wadusiamitolondo,mshigi tombo aumshigi kidari-machungwa, na fumbwe wengine wadusiatunguridi,tunguhina aumishigi mbalimbali. Kinyume nakekeo fumbwe hawaharibu mayai ya mwenye tago. Huyataga mayai 2-4 kwa kuzidi yaliyomo. Mayai ya fumbwe ni meupe kama yale ya mwenyeji lakini wakubwa zaidi. Ndani ya domo la makinda inafanana na ile ya makinda ya mwenyeji na dume anaiga wimbo wake.

Spishi

[hariri |hariri chanzo]

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Dume la kinili-kaya
    Dume la kinili-kaya
  • Jike la kinili-kaya
  • Dume la fumbwe mkia-njano
    Dume la fumbwe mkia-njano
  • Dume la kinili mweusi
    Dume la kinili mweusi
  • Dume la fumbwe buluu
    Dume la fumbwe buluu
  • Dume la fumbwe mgutaji
    Dume la fumbwe mgutaji
  • Dume la fumbwe mkia-mwembamba (manyoya ya majira ya kuzaa)
    Dume la fumbwe mkia-mwembamba (manyoya ya majira ya kuzaa)
  • Dume la fumbwe mkia-mwembamba (nje ya majira ya kuzaa)
    Dume la fumbwe mkia-mwembamba (nje ya majira ya kuzaa)
  • Jike la fumbwe mkia-mwembamba
    Jike la fumbwe mkia-mwembamba
  • Dume la fumbwe mkia-mpana (manyoya ya majira ya kuzaa)
    Dume la fumbwe mkia-mpana (manyoya ya majira ya kuzaa)
  • Jike la fumbwe mkia-mpana
    Jike la fumbwe mkia-mpana
  • Jike la fumbwe mkia-mrefu
    Jike la fumbwe mkia-mrefu
  • Dume la kinili miguu-myeupe
    Dume la kinili miguu-myeupe
  • Fumbwe mfalme
    Fumbwe mfalme
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Fumbwe&oldid=1087351"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp