Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Firenze

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Firenze
Firenze is located in Italia
Firenze
Firenze

Mahali pa Firenze katika Italia

Majiranukta:43°47′00″N11°15′00″E /43.78333°N 11.25000°E /43.78333; 11.25000
NchiItalia
MkoaToscana
WilayaFirenze
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla360,000
Tovuti:  http://www.comune.fi.it/
Mji wa Firenze

Firenze (kwaKiingerezaFlorence) nimji katikaItalia ya Kati namakao makuu yamkoa waToscana. Kati yamwaka1865 hadi1870 ilikuwa piamji mkuu waUfalme wa Italia.

Mji uko juu yamto Arno.Idadi ya wakazi ni mnamo 360,000 na pamoja narundiko la mji ni takriban 1,100,000.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Katikakarne za kati Firenze ilikuwa kituo muhimu chabiashara,uchumi nautamaduni kwaUlaya nzima. Kwa mfano, ni kati ya miji ambako uchumi wabenki ulijitokeza.

Firenze hutajwa mara nyingi kamachanzo cha kipindi cha "Renaissance" yaani kuzaliwa upya kwaustaarabu wa kale waUlaya. Wakati ule ulitawaliwa nafamilia yaMedici. Mji umepambwa kwamajengo mazuri sana yaliyojaapicha za kupendeza.Wasanii wengi walio muhimu katikautamaduni wa Ulaya waliishi Firenze kama vileDonatello,Botticelli,Michelangelo naLeonardo da Vinci. Pia watu kamamwanafalsafa wasiasaMachiavelli,mpelelezi waAmerikaAmerigo Vespucci namwanasayansiGalileo Galilei waliishi Firenze.

Sehemu ya mji imo katika orodha yaurithi wa dunia waUNESCO.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Firenze inavyoonekana kutoka "campanile" (mnara wa kanisa kuu)
    Firenze inavyoonekana kutoka "campanile" (mnara wakanisa kuu)
  • Kitovu cha mji wa kale
    Kitovu cha mji wa kale
  • Ponte Vecchio (daraja la kale)
    Ponte Vecchio (daraja la kale)

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo yaItalia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuFirenze kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Firenze&oldid=1179130"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp